WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu amesema
miongoni mwa changamoto anazokabiliana nazo ni kukosa rasilimali za kumwezesha
kuwafikia watu hasa wa vijijini na kuwaelewesha dhana nzima ya Muungano.
Waziri Sululu alitoa kauli hiyo mjini hapa alipotembelewa ofisini kwake na
Balozi wa Uingereza nchini, Diana Melrose, ambaye alitaka kujua changamoto
anazokutana nazo katika nafasi aliyonayo.
Waziri huyo alisema kuwa watu wa vijijini wengi hawaelewi Muungano, hivyo
kumuomba balozi huyo kuzungumza na wafadhili wengine, ili wawapatie rasilimali
za kufanikisha lengo hilo.
Aidha, Balozi Melrose alipenda kufahamu zaidi kuhusu maoni ya waziri juu ya
Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar na pia changamoto zitokanazo na
muungano huo.
Waziri Suluhu alisema kwa upande wake anaona ni bora kuendelea na Muungano
kuliko kuuvunja na kushauri mabadiliko yafanyike ili kuuboresha.
Pia alisema yapo makundi yenye ushawishi mkubwa katika jamii hivyo hutumia
nafasi waliyonayo kuwashawishi wananchi kuwa Muungano uvunjike sababu hauna
maana.
Alitoa mfano wa baadhi ya makundi hayo ni wanasiasa na viongozi wa dini
akisema sababu wao wanao ushawishi mkubwa katika jamii.
Akijibu swali la Balozi Melrose ambaye alitaka kujua kwamba inasemekana watu
wa Zanzibar hawana furaha sababu ya Muungano hivyo ndiyo maana wanashauri
uvunjwe, alikiri kuwapo kwa watu hao na kusema hali hiyo anafikiri inatokana na
ubinafsi
Chanzo - Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment