Habari za Punde

ZFA yaanza kutimiza ahadi wilayani

 
Na Salum Vuai, Maelezo
CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), leo kinaanza utekelezaji wa ahadi zake ilizozitoa kwa timu bingwa za wilaya mbalimbali Unguja na Pemba.
Katibu Mkuu wa chama hicho Kassim Haji Salum, amesema kwa kuanzia, baadhi ya wajumbe wa chama hicho watakuwa kisiwani Pemba leo na kesho, kukutana na viongozi wa klabu hizo ili kuwakabidhi zawadi zao za ubingwa.
Haji amesema kiasi cha shilingi milioni 27,550,000 zimetumika kununulia zawadi hizo zikiwemo pia fedha taslim zitakazotolewa kwa mabingwa na washindi wa pili wa kila ngazi.
Akitoa ufafanuzi, Katibu huyo alisema mabingwa wa ligi daraja la pili wilaya, watazawadiwa shilingi laki tano, na washindi wa pili shilling laki tatu.
Aidha, kutakuwa na zawadi za fedha viwango tafauti kwa mabingwa wa daraja la tatu, na la nne, Central, Junior na Juvenile kwa wilaya zote Unguja na Pemba.
Mbali na fedha, Haji alisema timu hizo zitapewa vifaa tafauti vya michezo, zikiwemo seti za jezi na vikombe.
Alisema vifaa vyengine ni pamoja na nyavu, nguo za waamuzi, kadi za njano na nyekundu, soksi, vibendera na mipira.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.