Habari za Punde

Maadhimisho ya wiki ya chanjo yaendelea

Mratibu wa Chanjo ya Kinamama na Watoto Yussuf Haji Makame alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichan) kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Chanjo kwa upande wa Bara la Afrika yanayoendelea nchini kote..Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
 
 
NA MAELEZO ZANZIBAR----22/04/2013
Wananchi wametakiwa kuwapeleka Watoto wao kupata Chanjo za kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Barani Afrika.
Wito huo umetolewa na Mratibu wa Chanjo ya Kinamama na Watoto Yussuf Haji Makame alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Chanjo kwa upende wa Bara la Afrika yanayoendelea nchini kote.
Amesema Chanjo zinasaidia kuokoa maisha ya Wanadamu na kuwataka wazazi waitumie Wiki hii kuwapeleka Watoto wao ambao hawajapata chanjo na wale waliokuwa hawajamaliza ili kukamilisha Chanjo hiyo.

Amefahamisha kuwa zaidi ya Vifo vya Watu Milioni tatu Duniani kote hukingwa kupitia Chanjo za Magonjwa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na Waratibu wa Chanjo hizo Mahospitalini.
Ameongeza kuwa Zanzibar imepiga hatua nzuri katika utoaji wa Chanjo ambapo zoezi la chanjo dhidi ya magonjwa mbali mbali limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90.
Aidha amewataka Wazazi kutobweteka na Takwimu hiyo nanakuomba waendelee kutoa ushirikiano kila inapostahiki ili kuwaweka Watoto katika mazingira mazuri ya kuepukana na hatari ya magonjwa.
Ameongeza kuwa katika Wiki hii ya Chanjo Vituo 156 vya kutolea huduma hiyo Unguja na Pemba vitakuwa wazi kwa muda wote wakazi kuanzi saa Moja na nusu hadi Tisa na nusu za jioni.
Aidha amebainisha kuwa kutokana na Wananchi kujua umuhimu wa Chanjo kumepelekea kwa kiasi kikubwa Magonjwa ya Kifaduro, Polio na Donda koo kupungua kwa kiasi kikubwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
Katika maadhimisho hayo ujumbe wa mwaka huu utakuwa ni Okoa Maisha, Kinga Ulemavu na toa Chanjo.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.