Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi tawi la Fumba, kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la tawi hilo, ikiwa ni moja ya ziara zake katika Mkoa wa Magharibu kutembelea matawi ya CCM.
Makamu Mwenyekiti akipanda Mti baada ya kuweka jiwe la msingi la Tawi la CCM Fumba.
Msoma Quran Ussi Khamis Ussi akisoma Quran katika sherehe hizo huko Bweleo.
Mwenyekiti wa Tawi la CCM Bweleo Maryam Makungu Mzee, akisoma risala ya Wanachama wa Tawi hilo kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipofika kutembelea Tawi laohuko Bweleo, katika ziara yake ya kutembelea matawi ya CCM Zanzibar.
Vijana wa Tawi la CCM Bweleo wakimshangila Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa CCM Abdalla Omar, katika tawi la CCM Bweleo.
Katibu wa Tawi la CCM Mwenge Haji Mrisho akitowa maelezo kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein,alipofika tawini hapo kuweka jiwe la msingi kuangalia uimarishaji wa Chama ngazi ya Matawi Zanzibar.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Mwenge Mwanakwerekwe wakishangilia baada ya Makamu Mweyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, kuweka jiwe la msingi la tawi lao.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akiwasili katika viwanja vya Shina No 18kwa ajili ya kupandisha bendera na kutowa kadi kwa Wanachama Wapya waCCM na Jumuiya zake.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akipandisha bendera ya Shina No 18 Kinuni Jimbo la Magogoni Unguja, akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Magharibi Unguja kuimarisha Chama cha Mapinduzi ngazi ya Matawi.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanachama wa CCM kinuni baada ya kupandisha bendera katika shina lao No 18 katika Jimbo la Magogoni Unguja, kutowa Kadi kwa Wanachama wapya wa CCM katika tawi hilo.
Mweyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Yussuf Mohammed Yussuf, akiwahutubia Wanachama wa CCM Tawi la Kinuni, kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti Dk. Ali Mohamed Shein, kuwahutubia Wanachama wa CCM Kinuni.
Msoma Risala ya Wanachama wa Tawi la CCM Kinuni Mwanjaha Nahoda akisoma risala ya tawi lao kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar baada ya kuwapandishia bendera katika Shina lao No 18 Kinuni Jimbo la Magogoni.ikiwa ni ziara ya Makamu Mwenyekiti kuimarisha Chama ngazi ya Matawi.
No comments:
Post a Comment