Habari za Punde

Ziara ya Rais wa China kuleta neema Zanzibar


 Balozi Mdogo wa China Zanzibar Quiman Chen akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusi ziara ya Rais Mpya wa China Tanzania wiki iliopita, na miradi alosaini kusaidia Zanzibar katika sekta mbalimbali na kutowa mualiko wa Rais wa Zanzibar kutembelea China.mazungumzo hayo yamefanyika katika jengo la Ofisi ya Ubalozi wa China Mazizini Zanzibar. . 

Waandishi wa habari wakimsikiliza Balozi Mdogo wa China Zanzibar  akizungumzia ujio wa Rais wa China Tanzania wiki iliopita.,
Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 04/04/2013
Imeelezwa kuwa ziara ya Rais wa China nchini Tanzania imeleta mafanikio mengi kwa Zanzibar ikiwa ni pamoja na Makampuni ya Kichina kupanga kuwekeza katika sekta tofauti Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China anayefanya kazi Zanzibar Bi Chen Qiman ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Mazizini kuhusiana na matokeo ya ziara ya Rais Jinping aliyofanya karibuni nchini Tanzania.
Amesema Zanzibar imeweza kunufaika moja kwa moja na ziara hiyo ikiwa ni pamoja na kusainiwa Miradi mitatu ya maendeleo kwa ajili ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Bi Chen amesema Rais wa China pia amemualika Rais Shein kwenda China kwa ziara ya kikazi ambapo pia atapata fursa zaidi ya kupanga mambo mengi ya kimaendeleo nchini huko.
Ameongeza kuwa Ziara hiyo inayotarajiwa kufanyika mwaka huu itakuwa fursa adhimu kwa Rais Shein kujifunza mengi na kukuza mahusiano zaidi kati ya Zanzibar na Jamhuri ya China.


Akizungumzia mikakati iliyowekwa na China ya kuisadia Zanzibar Bi Chen amesema Ofisi yake itaendelea kuitangaza Zanzibar katika nchi yake ili kuwavutia Wananchi wa China kuja kutembelea Zanzibar na kuimarisha Sekta ya Utalii.
katika kufanikisha hilo Bi Chen ameshauri Wazanzibari kuijifunza Lugha ya Kichina ili kurahisisha mawasiliano iwapo Wageni hao watakuja kutalii nchini hapa.
Mikakati mingine waliyoipanga ni pamoja na kuyahamasisha Makampuni kufanya uwekezaji katika Viwanda vya kusindika Matunda na kuwekeza katika Bahari jambo ambalo litasaidia sana maendeleo na kupunguza ukosefu wa Ajira.
Ziara ya Rais Jinping nchini Tanzania aliyoifanya karibuni imezidi kuimarisha mahusiano mema kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya China ambapo katika ziara hiyo jumla ya Miradi 17 ya kimaendeleo iltiwa saini.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

2 comments:

  1. unajua huwa sielewi sijui kwa kuwa sijaenda shule, nyinyi mmefanya mapinduzi ili tupate maendeleo ,lakini naona kila siku zikienda tunategemea ufadhili kutoka nje , so bora tungeendelea kutawaliwa na wakoloni tu huenda na sisi maisha yetu yangekuwa bora kama ya afrika kusini? angalau mahitaji muhimu kama maji , umeme , elimu na afya yangekuwa katika hali bora. Hivi ndugu na ndugu huwa hawatakiani heri katika dunia hii , vipi tutategemea wafadhili watuletee maendeleo ? serikali za SMZ inatawala watu wasiozidi milioni mbili , lakini waajiri wa mawizara , wanasiasa ni wengi mno, hamuoni kuna haja kuwa na serikali ndogo, kuna haja gani kuwa na mbunge, mwakilishi, mkuu wa wilaya, wa mkoa , makamishna nk hivi huu si uharibifu wa fedha za walalahoi? mkipungumza haya matumizi feki , tutapunguza utegemezi wa ufadhili ndugu zangu , sikio la dawa............

    ReplyDelete
  2. Naungana mkono kwa asilimia mia moja na mdau aliyechangia hapo juu,hujenda shule hali hii;jee kama ungekwenda shule. Sio tu kama kuna hao wote uliowataja katika eneo moja (diwani,mwakilishi,mbunge,mkuu wa wilaya na mkoa pamoja na makamishna)cha kusikitisha ni kwamba hata masuala simpe kama kuweka mazingira katika hali ya usafi pia yanashindikana. Leo unapita majimboni unapata kichefuchefu kwa uchafu. Lakini tusisahau kwamba kuna Meya na Mkurugenzi wa manispaa kwa upande wa majimbo ya mjini. Lakini pia ile manispaa ipo chini ya wizara kwa hiyo kuna waziri husika lakini pia yupo katibu. Allah tusaidie.......!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.