Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mwakilishi wa Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners ya Mjini Salala Nchini Oman Bwana li Omar Al-Sheikh wakibadilisha mawazo katika masuala ya uwekezaji hapa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Viongozi watano wa Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners ya Mjini Salala Nchini Oman uliofika ofisini kwake mapema asubuhi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Viongozi watano wa Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners ya Mjini Salala Nchini Oman baada ya mazungumzo yao yaliyohusu suala la uwekezaji hapa Nchini.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Na Othman Ame OMPR.
Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na masuala ya Kibiashara ya Shanfar & Partners Co. L.L.C yenye Makao makuu yake Mjini Salala Nchini Omar imeonyesha nia ya kutaka kuwekeza vitega uchumi vyake hapa Zanzibar.
Nia hiyo imekuja kufuatia Visiwa vya Zanzibar kubarikiwa kuwa na rasilmali kadhaa ambazo bado hazijatumika katika kusaidia kuendeleza uchumi wa Taifa sambamba na kuongeza vipato kwa wananchi.
Mwakilishi wa Kampuni hiyo Bwana Ali Omar Al–Sheikh akiuongoza ujumbe wa Viongozi watano wa Kampuni hiyo alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Ali Omar alisema ujumbe wake umeridhika na rasilmali kadhaa zilizomo ndani ya Visiwa vya Zanzibar baada ya kupata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali Mijini na Vijijini.
Alifahamisha kwamba Taasisi yao itaangalia maeneo inayoweza kuwekeza baada ya kufanya uchambuzi wa kina wakilenga zaidi katika Sekta ya Utalii ambayo Zanzibar tayari imeshafikia hatua kubwa katika kuimarisha miundo mbinu ya sekta hiyo.
“ Zanzibar tayari imeshafanikiwa vyema katika uwekezaji wa Hoteli za daraja linalokubalika Kimataifa. Kinachohitajika kwa wakati huu ni namna gani wanaweza kushajiisha makampuni ya kitalii kuweza kuitumia zaidi fursa hiyo “. Alifafanua Bwana Ali Omar.
“ Tumeliangalia hata zao la karafuu linalotegemewa kwa Uchumi wa Zanzibar ambalo pia linaweza kuimarishwa mauzo yake katika soko la Kimataifa kwa kutumiwa zaidi utaalamu wa kisasa “. Aliendelea Kusisitiza Mwakilishi huyo wa Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Salala.
Naye Ofisa Mkuu wa Kampuni hiyo ya Shantar & Partners Bwana S. Srihar alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba katika jitihada za kusaidia maendeleo ya Zanzibar Kampuni yao ina uwezo wa kuyashawishi mashirika na Makampuni ya Kimataifa ya watembezaji Watalii kulitumia soko la Zanzibar la Utalii katika kutembeza wateja na wageni wao.
Bwana Srihar alisema kufanikiwa kwa mpango huo kunaweza kutoa nafasi ya ajira kwa wazalendo waliowengi Nchini hasa lile kundi kubwa la vijana wanaomaliza masomo yao.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliueleza Ujumbe huo wa Kampuni ya Shanfar & Partners ya Salala Nchini Oman kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inaendelea na juhudi za kuimarisha miundo mbinu katika sekta mbali mbali za Kiuchumi hapa Nchini.
Balozi Seif alifahamisha kwamba uimarishaji wa kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Zanzibar ni miongoni mwa hatua hizo kwa lengo la kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Ujumbe huo wa Kampuni ya Kibiashara ya Shanfar & Partners kuitumia fursa hiyo ili isaidie uchumi wa Zanzibar sambamba na kuimarisha uhusiano wa Kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na Oman.
Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners Co. L.L.C ya Salala Nchini Oman imekuwa na ubia wa kibiashara na zaidi ya Makampuni saba ya Kimataifa katika Nyanja za Viwanda, Usafiri wa Anga, Utalii, huduma za Umeme, ujenzi na Uchapishaji.
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
5/5/2013.
ReplyDeleteh
Huu ujumbe sawa umeonana na mheshimwi lakini jemazingara ya hapaetu yanarizisha tunaona urasimu na ubinaps,uchoyo,ugoigoi, wa kiutendaji ktk serekali yetu umejaa
Makampuni mingi ya kibiashara tumeyaona ya kipiga picha na viongozi wetu baada ya muda ukiuliza vipi hupatijibu makini na hawa isejekuwa kama wale wabaishaji wengime walio wahikuja haa zanzibar
ReplyDelete@ Tatizo Ni Huyu Sefu Mweusi hataki kuiona Nchi yetu inaendelea. Nakumbuka Maalim Seif alikwenda Oman na Timu yake mwaka jana kuitangazia Zanzibar.. Lakini Kutokana na UV-CCM wanavoanza kuafanya fujo chini ya Amri ya Seif Ali Iddi na Wahafidhuna wengine. Ndio tukaona Wanakuja watu wengi kuangalia Opportunity yakufanya investment nabaadae Wanakimbia.
ReplyDeleteKwasababu Kiongozi aliekuwako mdarakani SieHafai hata kidogo. Ati leo ameturejeshea Mbio za Mwenge. Mbona alipokuweko Amani Karume hatukusikia upuuzi huo... Huyu Raisi Bwege Kweli. Lakini hizo ndio fadhila zakupewa Uraisi.
nakubaliana na anony 12.35 , na kuongezea wakija kuwekeza hawa hawa viongozi wetu dhalili wala hawaoni aibu hudai vijipasenti kama vile na wao wametoa fedha zao katika hio miradi , badala ya kudai wananchi kushirikishwa katika kuajiriwa wao hujipigia madebe wao na ndugu zao , halafu tunaambiwa tuwe wazalendo kwenye nchi , vipi wakati viongozi ni majambazi yakikubuhu na mahiri, na wakati wa ramazani na kwenye ibada hujisogeza karibu kuidai kufuturisha watu kwa edha za haramu , subirini tu shenzi mkumbane na mbabe wa wababe katika siku ambayo si kikwete , kimkapa , kimwinyi au kinyerere watakusaidieni, umri wenu ushafika mahali mrudi mjirekebishe lakini , dunia mmeikumbatia , haya yetu sisi macho , kila mtu atabeba zigo lake mwenyewe
ReplyDelete