Habari za Punde

Beki Zanzibar Heroes atua Simba

 
Na Salum Vuai, Maelezo
MCHEZAJI wa klabu ya Miembeni SC na timu ya taifa ya Zanzibar, ‘The Zanzbar Heroes’ Adeyoum Saleh Ahmed, ni mionhoni mwa wanasoka wapya waliojiunga na timu ya Simba SC ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuichezea msimu ujao.
Tayari nyota huyo ambaye ni mtoto wa kocha wa makipa wa Miembeni SC Saleh Ahmed ‘Machupa’, yuko jijini humo akijaribiwa katika mazoezi ya kikosi cha wekundu hao kinachonolewa na Abdallah Kibaden aliyemrithi Mfaransa Patrick Liewig ambaye amerejeshwa kwao.
Simba wanafanya mazoezi katika uwanja nwa Kinesi Urafiki jijini Dar es Salaam, ambapo Adyoum ni miongoni mwa wanandinga vijana wanaofanya majaribio ili kumridhisha Kibaden, ambaye alikuwa mshabuliaji mahiri wa timu hiyo miaka ya nyuma.
Akizungumza na gazeti hili jana, baba mzazi wa beki huyo wa kushoto Saleh ‘Machupa’, alithibitisha kuwa, mwanawe alikuwa katika orodha ya wanasoka wanaotakiwa na wekundu hao tangu walipomuona kwenye mashindano ya Chalenji mwishoni mwa mwaka jana nchini Uganda.
Adeyoum amekuwa beki tegemeo katika kikosi cha Miembeni, akiisaidia sana kurudi ligi kuu ya Zanzibar baada ya kuuza nafasi yake kwa Mundu msimu uliopita, na pia alichangia Zanzibar Heroes kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Chalenji yaliyopita mjini Kampala, Uganda.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.