Boti ya Royal Express ikiwa katika Bandari ya Zanzibar , ikisubiri ruhusa ya kutowa huduma baada ya kufanyiwa ukaguzi na Mkaguzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Bahari ZMA. Boti hiyo imeaza Safari zake hivi karibuni baada ya Uzinduzi wake hii.
Kampuni inayomiliki Boti ya Royal Express ya Ocean Enteprises Co. Ltd, ambayo boti yake jana ilipata hitilafu za kiufundi wakati ikitokea Dar- es-Salaam ikiwa katika safari zake za kawaida kati ya Dar-es-Salaam na Znzibar ilipata matatizo ya Kiufundi ikiwa karibu na kisiwa cha Chumbe,Zanzibar jana.
Oporesheni Meneja wa Kampuni hiyo, Yakub Abdalla Said, amesema wakati akizungumza na waandishi wa habari kutokana na tatizo hilo la kiufundi kutokea kwa kila chombo, Tatizo lilikuwa ni katika mafuta na ilibidi kupunguza mwendo wake baada ya kutowa alam ya kuonesha mafuta yakiwa na matatizo.
Amesema boti yao haikuwa na matatizo yoyote ya mashine zake ilikuwa ni mafutayalikuwa yamechanganyika na maji tu, na kuendelea na safari yake kwa mwendo mdogomdogo hadi bandarini ya Zanzibar ilifika salama bila ya matatizo yoyote kwa abiria wake.
Na leo tumeifanyia uchunguzi na kugunduwa kulikuwa na maji katika mafuta ndio ilikuwa sababu ya kwenda kwa mwendo huo mdogo mdogo na kusababisha kuleta alamu katika moja ya Kadi yake ya kutowa tahadhari katika njia ya mafuta.
Amesema leo wamesafisha tangi la mafuta na kuweka mafuta mapya kwa ajili ya kutowa huduma hiyo, katika matengenezo hayo yaliofanyika katika boti hiyo na kukaguliwa na Mkaguzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini na kutoa ripoti yake kwa matengenezo hayo, na kuikabidhi kwa Mkurugenzi wa ZMA, ili kutowa ruhusa ya kuanza safari zake kwa kutowa huduma hiyo
Amesema leo wamekuwa wamekatisha tiketi kwa ajili ya kuanza kwa safari yake kwenda Dar -se- Salaam na kuzuiliwa na Mkurugenzi mpaka wapate idhini na Mkaguzi wa ZMA amefanya ukaguzi na kusubiri ruhusa kutoka kwa Mkurugenzi wa ZMA, baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo na mkaguzi wake ilikuweza kuanza safari zake kama kawaida.
No comments:
Post a Comment