Na Raya Hamad, OMKR
Naibu
Katibu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dk Islam Seif amekiomba Kitengo kinachosimamia huduma za Afya ya Akili kusimamia
vyema zoezi la usambazaji wa dawa za wagonjwa
wa akili ili ziwafikie walengwa kwa wakati.
Dk
Islam ameeleza hayo Ofisini kwake
Migombani mara baada ya kupokea dawa mbali mbali za wagonjwa wa akili na
matatizo mchanganyiko kutoka kampuni ya PISAM 2008 Investiment limited ambayo ilishinda na kupata kazi ya
kununua dawa na vifaa visaidizi kupitia bodi ya zabuni ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais .
Jumla
ya aina 12 za dawa mbali mbali
zimekabidhiwa kwa wataalamu wa
kitengo cha huduma za afya ya akili
kwa ajili ya uhifadhi na maelekezo ya matumizi kwa wagonjwa wa akili na matatizo mchanganyiko
zikiwemo dawa za kutuliza maradhi ya kifafa,maradhi ya wasiwasi na sonona .
Nae
mratibu wa huduma za wagonjwa ya akili Nd Suleiman kwa niaba ya Wizara ya Afya ameishukuru
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kutoa dawa hizo ambazo zinaendana na
mahitaji ya wagonjwa waliopo.
Aidha
Suleiman amesema watakaofaidika zaidi na dawa hizo ni watu walioko vijijini ambao mara nyingi
wamekuwa wakisumbuka kwenda na kurudi kufuata dawa katika Hospitali ya wagonjwa wa akili.
Hata
hivyo mratibu huyo amewahakikishia wananchi kuwa dawa hizo ni salama hazina
matatizo na bado hazijapitwa na wakati .
Jumla ya shilingi Milioni 300 zilitengwa na
Serikali ya Mapinduzi Zanzaibar kupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
katika kipindi cha Bajeti ya 2012-2013 kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa
visaidizi za walemavu wa akili .
Dawa
zilizokabidhiwa zimegharimu
shilingi Milioni thamanini na saba na
hamsini na nane elfu
No comments:
Post a Comment