Habari za Punde

Dk Shein : Serikali zetu zinatilia mkazo utoaji huduma kwa wananachi

Na Said Ameir, Nanjing China
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatilia mkazo utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wake na ndio maana mpango yake maendeleo imejikita katika utoaji wa huduma hizo zenye ubora na kwa ufanisi.

Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya Pili ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma yanayofanyika mjini Beijing China Dk. Shein amewaeleza washiriki wa maonyesho hayo kuwa ili Serkali iweze kutoa huduma bora na kwa ufanisi katika sekta za afya,maji,elimu na huduma za kiuchumi inahaji kufahamu na upatikanaji wa tekinolojia na nyenzo za kufanikisha utoaji wa hudma hizo.

Kwa hiyo ameipogeza Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuandaa maonesho haya ambayo yamewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi mbali mbali pamoja na watoa huduma ambapo wanatoa fursa ya kuona kubadilishana uzoefu kwa kuonyesha huduma na namna ya matumizi yake.

Ameeleza kuwa sekta za huduma ambazo zimeainishwa na Shirika la Biashara Duniani (WTO) zikiwemo za mawasiliano, fedha, mzingira,utalii na usafiri zina umuhimu mkubwa kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Kutokana na umuhimu wake huo alieleza Dk. Shein kuwa ndio maana Tanzania imeweka mkazo katika maendeleo ya tekinolojia ya habari na mawasiliano kwa kuwa  inatoa nyenzo za utoaji wa huduma katika afya, elimu, kilimo na mahitaj mengine ya msingi ya wananchi.

Kwa hiyo“Nimefurahishwa kuona sekta ya Tekinolojia ya habari na mawasiliano imewakilishwa vyema katika maonesho haya” Dk. Shein alieleza.

Aliwaeleza washiriki katika uzinduzi wa maonesho hayo wakiwemo viongozi wa nchi mbalimbali zikiwemo Fiji, Sri Lanka, Singapore pamoja na Katibu Mkuu Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Biashara- UNCTAD kuwa Zanzibar imejikita katika kutangaza na kuimarisha sekta ya utalii ambapo katika maonesho hayo huduma zinazoambatana na sekta hiyo hasa za kifedha na kibiashara zimewakilishwa.  

“Utalii ni sekta mama katika uchumi wetu hivyo tunaweka milango wazi kwa wawekezaji katika sekta hii pamoja na kuwakaribisha watalii kuja nchini kwetu kujionea vivutio vyetu vya utalii” Dk. Shein alisema.

Ameongeza kuwa ili kurahisisha uwekezaji Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar-ZIPA na Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC vinatoa huduma zote kwa wawekezji na pia wawekezaji wanaweza kupata taarifa hizo kupitia balozi za Tanzania nchi za nje..

Alifafanua kuwa Serikali imeanzisha Mpango wa Utalii kwa Wote ambao unalenga kumshirikisha kila mwananchi kwa kuwa mbali ya kuwa utalii unahitaji mchango wa kila mwananchi kuendelea lakini pia faida za utalii zinawafikia wananch wote.

Maonesho hayo yalifunguliwa na Waziri Mkuu wa China Bwana LI Keqiang.

Dk. Shein yuko nchini China kwa ziara ya siku saba kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Bwana Xi Jinping

Katika ziara hiyo amefuatana na mke wake mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yusuf Mzee, Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdillah Jihad Hassan, Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar-ZIPA Salum Khamis Nassor.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.