HOTUBA YA
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, MHESHIMIWA MATHIAS
M. CHIKAWE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI
MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI
YA FEDHA KWA
MWAKA 2013/2014
A.
UTANGULIZI
1. Mheshimiwa
Spika, kutokana na taarifa yangu niliyoiwasilisha kwenye
Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala tulipokutana kwa lengo la kujadili na
hatimaye kupitisha maombi ya Mpango na Bajeti ya Wizara yangu, naomba kutoa
hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea Mpango na Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya fedha ya Wizara Katiba na Sheria, uliopitishwa na Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kwa Mwaka wa fedha 2013/2014.
Muundo wa Wizara na Majukumu
Yake
2.
Mheshimiwa Spika,
kulingana na Muundo wa Wizara yangu, majukumu yanayotekelezwa yanajumuisha;-
kuratibu mfumo wa utoaji haki nchini, kusimamia mambo ya katiba na utawala wa
sheria, kuendesha mashtaka na kuitetea Serikali mahakamani ,na kusimamia
utaratibu wa kutoa huduma ya msaada wa sheria kwa jamii. Majukumu hayo
yanatekelezwa na Taasisi zifuatazo:-
i.
Mahakama ya Tanzania;
ii.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
iii.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora;
iv. Tume ya
Kurekebisha Sheria Tanzania;
v.
Tume ya Utumishi wa Mahakama;
vi. Wakala
wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA); na
vii. Taasisi
ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania)
B.
MAPITIO
YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA MALENGO KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
Malengo ya Mwaka 2012/2013
3. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2012/2013, Wizara ilipanga kutekeleza
malengo ya Muda wa Kati kwa kuzingatia maeneo ya kipaumbele kama ifuatavyo:-
i.
Uratibu wa Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba;
ii. Usimamizi wa Usikilizaji na
Uendeshaji wa Mashauri;
iii. Uimarishaji wa Shughuli za Usajili, Ufilisi na Udhamini;
iv.
Uimarishaji na Uboreshaji wa Vyuo vya Mafunzo ya Sheria;
v.
Uimarishaji wa Utoaji wa Ushauri wa Kisheria Nchini;
vi.
Kufanya tafiti, mapitio, uandishi wa Sheria, Kanuni na
Hati Mbalimbali; na
vii.
Usimamizi wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Uratibu wa Mchakato wa
Mabadiliko ya Katiba
4.
Mheshimiwa
Spika,
katika Mwaka wa Fedha 2012/2013 Wizara yangu imeendelea kuratibu Mchakato wa
Mabadiliko ya Katiba. Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeanza kazi rasmi tarehe 01
Mei, 2012. Madhumuni ya kuanzishwa kwa Tume ni kuratibu, kukusanya, kuchambua
na kutathmini maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya Katiba. Kwa kuzingatia
muda ambao Sheria imeelekeza, Tume imeweka malengo ya kuwezesha kupatikana kwa
Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ifikapo Aprili 26, 2014.
5.
Mheshimiwa
Spika, katika
kipindi cha Mwaka wa Fedha 2012/2013, Tume ilitekeleza shughuli zake kama ifuatavyo:-
(i)
Kutoa elimu kwa umma na kuhamasisha wananchi
kushiriki katika hatua zote za mchakato wa mabadiliko ya Katiba kupitia vyombo vya
habari (Redio, Luninga, Magazeti, Tovuti) machapisho mbalimbali na katika mikutano;
(ii)
Kuandaa na kusambaza nakala 1,700,000 za Katiba ya Jamhuri
ya Muungano ya Tanzania, nakala 400,000 za
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83, Katiba ya Zanzibar nakala 19,000, Vipeperushi 800,000
vinavyoeleza majukumu ya Tume, Vipeperushi 670,000 vyenye maswali yanayoulizwa mara kwa mara na majibu yake nakala
588,600 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba sura ya 83 kwa lugha nyepesi;
(iii)
Kuandaa mifumo/njia mbalimbali ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi
kama vile mikutano ya hadhara katika Wilaya zote nchini, mikutano ya Makundi Maalum,
tovuti na mitandao ya kijamii, barua kwa njia ya posta, barua pepe, nukushi, ujumbe wa simu, makala, kujaza fomu maalum
za Tume pamoja na magazeti;
(iv)
Kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba katika Wilaya
zote nchini na kuyachambua maoni hayo;
(v)
Kuandaa, kuchapisha na kusambaza nakala 50,000 za Mwongozo kuhusu Muundo na Utaratibu
wa kuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya (Mamlaka ya Serikali za Mitaa);
(vi)
Kutoa elimu kwa umma kuhusu utaratibu wa uundwaji wa Mabaraza ya Katiba, majukumu ya Mabaraza
hayo na kuandaa ratiba ya uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba (Mamlaka ya
Serikali za Mitaa);
(vii)
Kuunda Mabaraza ya Katiba ya Wilaya (Mamlaka
ya Serikali za Mitaa;
(viii)
Kusimamia uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya (Mamlaka ya Serikali za Mtaa);
(ix)
Kuandaa Mwongozo wa Mabaraza ya Katiba ya Asasi,
Taasisi na Makundi ya Watu; na
(x)
Kuandaa Ripoti ya Awali na Rasimu ya Katiba.
6.
Mheshimiwa
Spika, Tume hii pia, inalo jukumu kubwa la
kusimamia Mabaraza ya Katiba. Tume imeyagawa Mabaraza ya Katiba katika Makundi mawili;
kundi la kwanza ni Mabaraza yatakayosimamiwa na Tume (Mabaraza ya Katiba ya Wilaya – Ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa)
na kundi la pili ni Mabaraza ya Katiba ya
Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye malengo yanayofanana.
Hadi sasa Tume imeweza kuwapata Wajumbe
wa Mabaraza ya Katiba katika Ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kupitia chaguzi
na taratibu mbalimbali ambapo jumla ya Wajumbe 10,932 wamepatikana katika Mikoa 17. Katika kufanikisha kupatikana kwa Wajumbe, Tume ilitumia Mfumo wa Serikali za Mitaa na taratibu za Mikutano katika
ngazi za Serikali za Mitaa zilizopo sasa (Vijiji, Mitaa na Kata).Utaratibu huu ndio
ulioainishwa kwenye Sheria zinazosimamia Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Aidha, kwa mujibu wa Ratiba ya
shughuli za Tume, mikutano ya Mabaraza ya Katiba itaanza mwezi Juni, 2013 na itaendelea
hadi mwezi Agosti, 2013.
7.
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa Kifungu cha 10 cha
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayo
mamlaka na uhuru katika utekelezaji wa majukumu yake. Aidha, Tume imekuwa na
utaratibu wa kutoa taarifa kuhusu jambo lolote linalopangwa kutekelezwa na kutoa
taarifa baada ya utekelezaji wake kupitia mikutano na vyombo vya habari,
magazeti, majadiliano katika redio, luninga na majarida ya kijamii.
Usikilizaji
wa Mashauri nchini
8.
Mheshimiwa
Spika,
katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 Mahakama ya Tanzania imesikiliza mashauri
katika ngazi mbalimbali kama ifuatavyo:-
i.
Mahakama
ya Rufani ilianza Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi
ya mashauri 1,743 yaliyosalia kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakama ya
Rufani ilipokea mashauri mapya 450 na hivyo kuwa na jumla ya mashauri 2,193.
Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2012 hadi Machi, 2013 Mahakama imesikiliza na
kuyatolea maamuzi jumla ya mashauri 275 sawa na asilimia 13 ya
jumla ya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri 1,918.
Aidha, uwezo wa wastani wa uondoaji wa mashauri (Clearance Rate) katika
Mahakama ya Rufani kwa tathmini ya kipindi cha miezi sita iliyopita ni asilimia
61. (Jedwali Na.1)
ii.
Mahakama
Kuu ilianza Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi
ya mashauri 9,737 yaliyosalia kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakama Kuu
ilipokea mashauri mapya 7,547 na hivyo kuwa na jumla ya mashauri 17,284.
Katika kipindi cha kuanzia Julai 2012 hadi Machi 2013 Mahakama Kuu
imesikiliza na kuyatolea maamuzi jumla ya mashauri 5,191 sawa na
asilimia 30 ya jumla ya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya
mashauri 12,093. Aidha, uwezo wa wastani wa uondoaji wa mashauri (Clearance
Rate) katika Mahakama ya Kuu kwa tathmini ya kipindi cha miezi sita iliyopita
ni asilimia 70. (Jedwali Na.2)
iii.
Mahakama
Kuu Divisheni ya Biashara, ilianza Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi ya mashauri 285
yaliyosalia kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakama ilipokea mashauri
mapya 118 na hivyo kuwa na jumla ya mashauri 403. Katika kipindi
cha kuanzia Julai, 2012 hadi Machi 2013 Mahakama ya Biashara imesikiliza
na kuyatolea maamuzi jumla ya mashauri 74 sawa na asilimia 18
ya jumla ya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri 329.
Aidha, uwezo wa wastani wa uondoaji wa mashauri (Clearance Rate) katika
Mahakama ya Biashara kwa tathmini ya kipindi cha miezi sita iliyopita ni
asilimia 64.(Jedwali Na.3)
iv.
Mahakama
Kuu Divisheni ya Kazi, ilianza Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi
ya mashauri 1,597 yaliyosalia kutoka miaka ya nyuma. Aidha,
Mahakama ilipokea mashauri mapya 674 na hivyo kuwa na jumla ya
mashauri 2,271. Katika kipindi cha kuanzia Julai 2012 hadi Machi 2013 Mahakama
ya Kazi imesikiliza na kuyatolea maamuzi jumla ya mashauri 491 sawa na
asilimia 22 ya jumla ya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya
mashauri 1,780. Aidha, uwezo wastani wa uondoaji wa mashauri (Clearance
Rate) katika Mahakama ya Kazi kwa tathmini ya kipindi cha miezi sita iliyopita
ni asilimia 73. (Jedwali Na.4)
v.
Mahakama
Kuu Divisheni ya Ardhi, ilianza Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi
ya mashauri 5,393 yaliyosalia kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakama ya
Ardhi ilipokea mashauri mapya 427 na hivyo kuwa na jumla ya mashauri 5,820.
Katika kipindi cha kuanzia Julai 2012 hadi Machi, 2013 Mahakama ya Ardhi
imesikiliza na kuyatolea maamuzi jumla ya mashauri 427 sawa na asilimia 7
ya jumla ya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri 5,393.
Aidha, uwezo wa wastani uondoaji wa mashauri (Clearance Rate) katika
Mahakama ya Ardhi kwa tathmini ya kipindi cha miezi sita iliyopita ni asilimia 100.
(Jedwali Na.5)
vi.
Mahakama
za Hakimu Mkazi, ilianza Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi
ya mashauri 25,002 yaliyosalia kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakama
ilipokea mashauri mapya 980 na hivyo kuwa na jumla ya mashauri 25,982.
Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2012 hadi Machi 2013 Mahakama imesikiliza na
kuyatolea maamuzi jumla ya mashauri 612 sawa na asilimia 2 ya
jumla ya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri 25,370.
Aidha, uwezo wa wastani wa uondoaji wa mashauri (Clearance Rate) katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tathmini ya kipindi cha miezi sita iliyopita ni
asilimia 73. (Jedwali Na.6)
vii. Mahakama za Wilaya,
zilianza Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi ya mashauri 31,025 yaliyosalia
kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakama za Wilaya ilipokea mashauri mapya 94,872
na hivyo kuwa na jumla ya mashauri 125,897. Katika kipindi cha
kuanzia Julai 2012 hadi Machi 2013 Mahakama za Wilaya imesikiliza na kuyatolea
maamuzi jumla ya mashauri 104,359 sawa na asilimia 83 ya jumla ya
mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri 21,538. Aidha, uwezo
wa wastani wa uondoaji wa mashauri (Clearance Rate) katika Mahakama za
Wilaya kwa tathmini ya kipindi cha miezi sita iliyopita ni asilimia 110.
(Jedwali Na.7)
viii. Mahakama za Mwanzo,
zilianza Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 zikiwa na idadi ya mashauri 124,959 yaliyosalia
kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakama za Mwanzo zilipokea mashauri mapya 650,181
na hivyo kuwa na jumla ya mashauri 775,140. Katika kipindi cha
kuanzia Julai, 2012 hadi Machi 2013 Mahakama imesikiliza na kuyatolea maamuzi
jumla ya mashauri 577,425 sawa na asilimia 74 ya jumla ya
mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri 197,715. Aidha, uwezo
wa wastani wa uondoaji wa mashauri (Clearance Rate) katika Mahakama za
Mwanzo kwa tathmini ya kipindi cha miezi sita iliyopita ni asilimia 89.
(Jedwali Na.8)
Uendeshaji
wa Mashauri nchini
9.
Mheshimiwa
Spika,
katika kutekeleza jukumu la kuiwakilisha Serikali katika mashauri mbalimbali
ndani na nje ya nchi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imeendesha
mashauri ya Jinai, Madai na Katiba katika Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu na
Mahakama zilizo chini ya Mahakama Kuu isipokuwa Mahakama za Mwanzo. Aidha,
Ofisi pia imeendelea kuratibu mashauri ya usuluhishi (arbitration) ambapo manne (4)
ya Mahakama Kuu na 11 ya Tume ya
Usuluhushi (CMA). Hadi Machi, 2013
kulikuwa na jumla ya mashauri ya madai
682 yakijumuisha mashauri mapya 132.
Mashauri haya yote yalifunguliwa dhidi ya Serikali na Kesi moja (1) ya Madai ilifunguliwa na Serikali. Mashauri hayo yako katika hatua mbalimbali za
kusikilizwa na kutolewa maamuzi na Mahakama (Jedwali Na.11). Mashauri ya madai yaliyohitimishwa hadi mwezi
Machi, 2013 ni 40 na kubaki mashauri
642.
Aidha,
kulikuwa na jumla ya Maombi ya madai 285
yaliyofunguliwa yakiwemo mapya 89
yaliyopokelewa katika kipindi cha Julai 2012 hadi Machi 2013. Maombi haya ya
madai yalifunguliwa dhidi ya Serikali. Hadi Machi, 2013 maombi ya madai 63 yalihitimishwa na maombi 222 yanaendelea kusikilizwa. Vilevile,
palikuwepo na Rufani za madai 46
zikijumuisha mpya saba (7). Kati ya
hizi rufani mbili (2) zilihitimishwa
na kubaki na rufani 44 ambazo
zinazoendelea kusikilizwa. Vilevile, kuhusu masuala ya upatanishi (arbitration) mgogoro mmoja (1) unaohusu Serikali
ulishughulikiwa kati ya Mashauri yaliyobakia.
Hali
kadhalika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendelea kuendesha mashauri
ya rufani za uchaguzi yatokanayo na uchaguzi Mkuu wa 2010 ambayo ni kutoka
Kigoma (3), Tabora (2), Mara (1), Sumbawanga (1), Dar
es Salaam (1), Mtwara (3), Kagera (1) na Arusha (2). Kati
ya mashauri hayo, mashauri matano (5)
yamehitimishwa na mashauri tisa (9)
yanaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Rufani.
10.
Mheshimiwa
Spika,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Kurugenzi ya Mashtaka iliendelea
kutekeleza jukumu lake la kuendesha mashauri ya jinai katika Mahakama ya
Rufani, Mahakama Kuu na Mahakama zilizo chini ya Mahakama Kuu na pia iliendelea
kuratibu kazi za upelelezi unaofanywa na vyombo vya upelelezi isipokuwa
Mahakama za Mwanzo. Jumla ya mashauri 14,453
yaliyokuwepo na mengine mapya 13,487
ya Mwaka 2012/2013 yaliendelea kuendeshwa Mahakamani. Mashauri haya yanahusu
kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mashauri yaliyohusisha mauaji ya watu wenye
ulemavu wa ngozi, udanganyifu na utakatishaji wa fedha haramu. Hadi mwezi Machi
2013 mashauri 5,257 yalihitimishwa
na kubaki mashauri 22,683
yatakayoendelea kuendeshwa katika ngazi mbalimbali za Mahakama pamoja na
Mashauri mapya yatakayopokelewa (Jedwali
Na. 12).
Katika uendeshaji wa mashauri yanayohusu watu wenye
ulemavu wa ngozi, jumla ya matukio 60
yaliripotiwa na polisi nchi nzima. Mashauri 12 yanaendelea kusikilizwa, mashauri 14 yameondolewa mahakamani na mashauri 10 yameamuliwa ambapo Jamhuri imeshinda mashauri yote. Mashauri 24 yanaendelea kufanyiwa kazi.
11.
Mheshimiwa
Spika,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya upelelezi
vya TAKUKURU na Jeshi la Polisi ni mshiriki mkubwa katika mapambano dhidi ya
rushwa. Hadi kufikia Mwaka 2012/2013 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepokea
jumla ya majalada 317 yaliyohusu
rushwa kubwa na ubadhirifu kutoka vyombo vya upelelezi vya TAKUKURU na Jeshi la
Polisi. Kati ya Majalada hayo, 95
yaliandaliwa hati za Mashtaka na kupewa kibali cha kushtaki, jalada moja (1) lilifungwa na majalada 65 yalirudishwa kwa vyombo husika kwa
ajili ya kufanyiwa upelelezi zaidi na majalada 156 yanaendelea kufanyiwa kazi na Divisheni ya Mashtaka.
Vilevile, katika kuhakikisha kwamba mali zilizopatikana
kwa njia zisizo halali zinarejeshwa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
inasimamia urejeshwaji wa mali na fedha (Asset
Recovery and Forfeiture) katika mashauri mbalimbali. Katika kipindi hiki
mali zilizotaifishwa ni pamoja na magari manne (4) katika mikoa ya Morogoro (1),
Dar es Salaam (1) na Tanga (2) na nyumba tatu (3) pamoja na fedha Shilingi bilioni saba (7) zinazotakiwa
kurejeshwa baada ya watuhumiwa watano kutiwa hatiani katika shauri la madawa ya
kulevya. Watuhumiwa hao wamekata rufaa.
12.
Mheshimiwa
Spika,
katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
imeendelea kuendesha mashauri 14 yanayohusu
makosa ya wizi, kugushi na kutakatisha fedha ambayo yaliyobaki katika kipindi
cha mwaka 2011/2012 katika Mahakama mbalimbali nchini zikiwemo Mahakama ya
Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Arusha na Nzega. Mashauri haya yanahusu takribani
kiasi cha Shilingi Bilioni 48. Hadi
Machi, 2013 kulikuwa na jumla ya kesi tatu (3) zilizotolewa hukumu. Kesi moja (1) yenye kuhusisha kiasi cha takriban Shilingi Bilioni moja washtakiwa waliachiwa huru lakini Jamhuri
imekata rufaa na kesi mbili (2)
washtakiwa wametiwa hatiani na wanatakiwa kurudisha fedha zipatazo Shilingi Milioni 960. Vilevile, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendesha
mashauri yanayohusu madawa ya kulevya ambapo katika kipindi cha Julai 2012 hadi
Machi 2013 kesi moja (1) ya madawa
ya kulevya ilihitimishwa kwa Mahakama kuwatia hatiani watu watano kwa kila
mmoja kuhukumiwa kifungo cha miaka 25.
Utenganishaji wa jukumu la
Upelelezi na Mashtaka (Civilianisation of Prosecutions Service)
13.
Mheshimiwa
Spika,
katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
iliendelea na utekelezaji wa Mpango wa Kutenganisha Jukumu la Upelelezi na
Mashtaka (Civilianisation of
Prosecutions Service) ili kuondoa tatizo la haki kuchelewa kutendeka, kesi
kuchukua muda mrefu Mahakamani kwa sababu ya muda mrefu unaotumika katika
upelelezi. Hatua mbalimbali ziliendelea kuchukuliwa ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji, uelimishaji na uenezaji wa utaratibu huu katika Mikoa na Wilaya
zote za Tanzania Bara. Hatua hizi ni pamoja na kuajiri Mawakili wa Serikali na
kufungua ofisi katika Mikoa mitano (5)
ya Morogoro, Manyara, Kigoma, Njombe na Pwani pamoja na Wilaya za Monduli na
Temeke. Hadi sasa zipo Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mikoa 22 ya Tanzania Bara. Mikoa hiyo ni Dar
es Salaam, Arusha, Mbeya, Iringa, Singida, Dodoma, Mtwara, Lindi, Mara, Kagera,
Ruvuma, Rukwa, Mwanza, Kilimanjaro, Tanga, Tabora, Shinyanga, Morogoro, Pwani, Kigoma, Manyara
na Njombe. Aidha, lengo la kuwa na Ofisi
za Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mikoa mitatu iliyosalia ya Geita, Simiyu
na Katavi litakamilishwa katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.
Hadi
Machi, 2013, Divisheni ya Mashtaka ilikuwa inaendesha kesi katika Mahakama za
Wilaya 22 za Makao Makuu ya Mikoa na
Wilaya zilizotajwa hapo juu. Lengo ni kufikisha huduma za mashtaka karibu zaidi
na wananchi. Aidha, Mpango huu wa kutenganishwa kwa shughuli za upelelezi na
mashtaka umesaidia sana kupunguza idadi ya kesi zinazofunguliwa Mahakamani na
msongamano wa mahabusu na wafungwa magerezani. Idadi ya Mahabusu imepungua
kutoka 17,932 kwa mwezi Julai, 2012
hadi kufikia mahabusu 16,973 mwezi Machi 2013. Vilevile, idadi ya wafungwa
imepungua kutoka 17,868 kwa mwezi
Julai 2012 hadi kufikia wafungwa 17,497
mwezi Machi, 2013.
Lakini
la msingi zaidi ni kuwa, utenganishaji huu unafanywa kwa misingi ya utawala
bora. Si vyema kukipa chombo kimoja cha dola madaraka ya kuhisia, kutuhumu,
kukamata, kupeleleza na kushitaki bila udhibiti wa chombo kingine. Wataalam wa
utawala wanasema “Regulation is the hallmark of Government” ndiyo maana kuna
EWURA, TICRA, SSRA nk. Na ndani ya Serikali nako ni muhimu kuwa na utaratibu
huu wa “checks and balances”. Nchi
nyingi ambazo mifumo yao ya Sheria na Utawala inafanana na sisi wana utaratibu
huu. Marekani mashtaka huendeshwa na Mwanasheria Mkuu kupitia “District
Attorneys”. Uingereza kuna “Crown Prosecution Agency” nk. Na
hapa kwetu ndiyo tuna Mwanasheria Mkuu kupitia Ofisi ya DPP.
Uimarishaji wa Utoaji wa
ushauri wa Kisheria nchini
14.
Mheshimiwa
Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Wizara
yangu kwa kushirikiana na Asasi zisizo za Kiserikali, iliunda kikosi kazi kwa
ajili ya kufanya utafiti na kuwasilisha mapendekezo yatakayoisaidia Serikali
kubuni utaratibu wa utoaji wa huduma za
msaada wa kisheria kwa watu wasio na uwezo wa kulipia gharama za kisheria. Kikosi kazi hicho
kimefanya utafiti na tayari mapendekezo ya kutunga sheria itakayoratibu utoaji
wa huduma za msaada wa kisheria kwa umma
na kuwatambua watoa huduma za msaada wa kisheria kwa umma ikiwa ni pamoja na
wasaidizi wa kisheria (Paralegals) yameshawasilishwa
Serikalini. Taratibu za kupata Sheria
hiyo zinaendelea vizuri na ni matumaini yetu kwamba Rasimu ya Sheria hii
itawasilishwa katika Bunge hili tukufu katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa
2013/2014.
15.
Mheshimiwa
Spika,
katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2011/2012 Wizara yangu ilianzisha Kamati
ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari.
Kamati hii imeanzishwa kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Nchi
Zinazozunguka/za Ukanda wa Maziwa Makuu (The International Conference on the Great Lakes
Region-ICGLR). Nchi husika zilifikia makubaliano katika Mkataba
uliosainiwa na Nchi zote wanachama ya kuweka utaratibu wa kubaini viashiria vya
uvunjifu wa amani na kusababisha vita katika eneo la maziwa makuu. Tanzania imesaini “protocol for the prevention and
punishment of the crimes of Genocide, war crimes, crimes against humanity and
all forms of discrimination” ambayo pia yanaitaka Nchi wanachama
kuanzisha Kamati za Kitaifa za Kuzuia Mauaji ya Kimbari. Nchini Tanzania Kamati hiyo ilianzishwa mwezi
Februari 2012 na Kamati hii inajukumu la kubaini dalili/viashiria vya uvunjifu
wa amani ya Nchi yetu, kuishauri
Serikali pamoja na kujenga uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuzuia uvunjifu
wa Amani na mauaji na uhalifu dhidi ya binadamu nchini. Kamati hii ya kitaifa ina wajumbe wafuatao:-
i.
Ofisi ya Rais-Ikulu
ii.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
iii.
Ofisi ya Waziri Mkuu
iv.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
v.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
vi.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa
vii.
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
viii.
Wizara ya Vijana, Habari, Utamaduni na
Michezo
ix.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
x.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto
xi.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
xii.
Chuo Kikuu cha Dar es salaam
xiii.
Taasisi ya Wakfu ya Mwalimu Nyerere
Aidha,
mapema mwezi Disemba, 2012, Wizara kupitia Kamati hii imefanya Mkutano na
viongozi wa dini zote ambapo viongozi wa kidini walijadili nafasi yao katika
kulinda na kudumisha amani nchini.
Mikutano ya Kamati hii ni endelevu na ili iwe na tija hutumika kuishauri
Serikali na pia kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzuia mauaji na uhalifu
dhidi ya binadamu nchini.
16.
Mheshimiwa
Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 Wizara
yangu imeratibu na kuandaa Mkutano wa Kimataifa wa Kamati ya Umoja wa Mataifa
ya Kupambana na Ugaidi uliofanyika Dar es salaam kuanzia tarehe 26-28 Februari,
2013 na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Nchi 36 duniani. Ujumbe na mada kuu
katika Mkutano huo ulikuwa ni “Bringing Terrorists to Justice; Policy challenges
in the Prosecution and Prevention of Terrorism”.
17.
Mheshimiwa
Spika,
katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 Wizara yangu imekamilisha tafiti kuhusu hali ya watoto wanaokinzana na
Sheria na pia kuhusu upatikanaji wa haki sheria kwa watoto wenye umri wa chini
ya miaka 18 kwa kushirikiana na UNICEF.
Kutokana na utafiti huo, Wizara imeandaa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Haki
Sheria kwa watoto. Mpango Mkakati huu utaboresha mfumo mzima wa upatikanaji wa
ulinzi na haki kwa watoto nchini. Vilevile, Mpango Mkakati huu utasaidia kuweka
pamoja mikakati ya namna bora ya kushughulikia masuala ya haki sheria kwa watoto
nchini. Mpango Mkakati huu unaandaliwa Waraka wa Baraza la Mawaziri kwa ajili
ya kujadili na kupitisha Mpango Mkakati huu ili uweze kutumika.
18.
Mheshimiwa
Spika,
katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 Wizara yangu imeendelea kupokea
malalamiko ya aina mbalimbali toka kwa wananchi na yameshughulikiwa. Malalamiko
mengi yalielekezwa kwenye Taasisi na vyombo vya Serikali vinavyojishughulisha na
utoaji haki na usimamizi wa Sheria.
Malalamiko hayo yalishughulikiwa kwa kuwasiliana na vyombo/Taasisi
husika kama njia ya kuyatafutia utatuzi.
19.
Mheshimiwa
Spika,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendelea kutekeleza jukumu la
kuimarisha utoaji wa ushauri wa kisheria kuhusu masuala ya mikataba ya kibiashara,
Kimataifa, Katiba na Haki za Binadamu. Aidha, Ofisi pia imeshiriki katika
mikutano mbalimbali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Mataifa, Nchi
wanachama wa Kusini mwa Afrika (SADC)
na Nchi za Umoja wa Afrika kwa ajili ya kufanya majadiliano na kutoa ushauri wa
kisheria. Majadiliano ambayo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshiriki
ni ubia wa kibiashara kati ya Umoja wa Nchi za Ulaya na Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EPA); kuanzishwa kwa Itifaki
ya Umoja wa Fedha; Itifaki ya Mahakama ya Nchi
wanachama wa Kusini mwa Afrika; kuanzisha Soko Huru baina ya Nchi Wanachama
wa Afrika Mashariki, SADC na COMESA; kurekebisha Mkataba wa
kuanzisha Mahakama ya Umoja wa Afrika; kurekebisha Mkataba ulioanzisha Bunge la
Afrika; Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia kusambaa kwa silaha ndogo;
kurekebisha Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; na majadiliano ya mgogoro
wa mpaka baina ya Tanzania na Malawi. Vilevile, katika kipindi cha Mwaka wa
Fedha wa 2012/2013 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshughulikia na
kutoa ushauri wa kisheria katika mikataba (Contracts)
330. Kati ya Mikataba hii, mikataba 295
ilihusu manunuzi ya umma na Mikataba 35
ilihusu masuala ya uwekezaji. Vile vile, Mikataba ya Makubaliano (MOU) 58 ilishughulikiwa na makubaliano
baina ya Nchi na Nchi (Bilateral
Agreement) 21; mahudhurio ya vikao 185
vilivyohusu Majadiliano ya Mikataba na Mahusiano ya Kimataifa.
Mpango wa Serikali Wazi
20.
Mheshimiwa
Spika, kama nilivyoeleza mwaka jana katika
Bunge lako Tukufu, Serikali imeendelea kutelekeza Mpango wa Uendeshaji Shughuli
za Serikali kwa Uwazi (Open Government
Partnership-OGP) ambao ulianzishwa tarehe 21 Septemba, 2011. Mpango huu unasimamiwa
na Wizara yangu na kuratibiwa na Kamati ya Kitaifa chini ya uenyekiti wa Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu. Katika mwaka wa fedha 2012/2013 Mpango huu
umeendelea kutekelezwa na Sekta tatu za kipaumbele za huduma za jamii ambazo ni
Afya, Maji na Elimu. Mpango wa Serikali wazi unajikita katika maeneo ya kuweka
uwazi zaidi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali, Ushirikishwaji wa
wananchi katika mpango wa utekelezaji, Uwajibikaji na Uadilifu, Utawala Bora,
kupambana na Rushwa na matumizi ya teknolojia na ubunifu. Malengo ya Mpango huu
ni kuimarisha usimamizi wa matumizi ya rasilimali za umma kuboresha utoaji wa
huduma, kuongeza usalama wa nchi na kuongezeka kwa uwajibikaji wa kitaasisi.
21.
Mheshimiwa
Spika, katika kutekeleza Mpango huu
yafuatayo yamefanyika:-
i.
Mpango Kamili wa OGP
Tanzania umeandaliwa na kuwasilishwa Makao Makuu ya OGP katika Mkutano Mkuu wa
Mwaka wa viongozi wa nchi wanachama wa OGP uliofanyika Brasilia Brazili tarehe
17-18 Aprili, 2012;
ii. “Road
Map” na Bango kitita ya “Commitments” ya shughuli zitakazotekelezwa hadi
kufikia Juni, 2013 imeandaliwa na kusambazwa kwenye sekta husika;
iii. Wizara
nane (8) zimeandaa Mipango Kazi yao
na kuiwasilisha kwenye Kamati. Wizara hizi ni Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya
Rais Tume ya Mipango, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, Wizara ya Maji, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Fedha
Aidha, kwa hivi sasa Kamati imeandaa
Mkakati wa Mawasiliano kuhusu utekelezaji wa Mpango wa OGP Tanzania (Open Government Partnership Communication
Strategy) na vile vile Kamati inashirikiana
kwa karibu na Wakala wa Serikali Mtandao (e-Government Agency) kuhakikisha Tovuti ya wananchi (Citizen Portal) inaanza kazi mapema
iwezekanavyo ili iweze kuhudumia wananchi. Aidha, Waraka wa Mapendekezo ya
Kutunga Sheria ya Uhuru wa Habari (Freedom
of Information Law) unaandaliwa na Wizara husika ambayo ndiyo yenye dhamana
ya masuala ya habari nchini, na utawasilishwa kwenye ngazi za maamuzi na
hatimaye sheria kutungwa na kuletwa
katika Bunge lako Tukufu.
iv. Kuhudhuria
kikao cha Mawaziri wa Nchi zinazotekeleza Mpango wa Serikali Wazi (OGP)
kilichofanyika Mjini London kuanzia tarehe 22-25/04/2013.
22.
Mheshimiwa
Spika,
katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 Wizara yangu itaendelea kusimamia Mipango
Kazi ya Sekta za kipaumbele zinatekelezwa kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto
zinazoendelea kujitokeza katika utekelezaji wa Mpango wa Serikali Wazi.
Utafiti na Mapitio ya
Sheria
23.
Mheshimiwa
Spika, Wizara kupitia Tume ya Kurekebisha
Sheria Tanzania imekamilisha Taarifa ya Mfumo wa Haki za Madai (Civil Justice System Review) na
Taarifa ya Mapitio ya Tamko la Sheria za Mila zinazofuata mkondo wa ukoo wa
mama (Matrilineal Societies). Taarifa
hizi zimewasilishwa kwangu ili
ziweze kufanyiwa kazi zaidi na Mwanashera Mkuu wa Serikali na kutolewa kauli Bungeni
ya hatua zitazochukuliwa. Tume iko katika hatua za mwisho za kukamilisha
Taarifa ya Mapitio ya Sheria zinazosimamia Usuluhishi na Utatuzi wa Migogoro ya
Ardhi. Aidha, Rasimu ya Awali ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazosimamia
Huduma za Jamii kwa Wazee imeandaliwa ili kuwezesha kufanya utafiti katika
Mikoa 12 ya Tanzania ambayo ni Kagera,
Shinyanga, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Rukwa
Ruvuma na Pwani. Kwa upande wa Mapitio ya Mfumo wa Sheria unaosimamia Haki za
Walaji (Consumer Protection),
taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi zimeanza.
24.
Mheshimiwa
Spika,
katika kipindi cha Julai 2012 hadi Machi 2013 Tume imefanya uchambuzi wa hukumu
za kesi za Mahakama ya Rufani ya Tanzania zipatazo 100 ili kuainisha misingi ya Kisheria (Legal Principles) na kuweka misingi hiyo katika tovuti yake ili
kuwarahisishia wadau kuelewa tafsiri ya maamuzi ya Mahakama ya Rufani kuhusu
vipengele vya kisheria vilivyotumika. Vilevile Tume imewasilisha kwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Rasimu tano
(5) za tafsiri za Sheria katika lugha ya Kiswahili (Kiambatisho ‘E’). Pia Tume
imeendelea kutoa elimu ya Sheria kwa umma kupitia vipindi vya Redio na runinga
kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu haki, wajibu na masuala mbalimbali ya Kisheria.
Uandishi wa Sheria na Hati
Mbalimbali
25.
Mheshimiwa
Spika,
katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
iliendelea kutekeleza jukumu la kuandaa Miswada ya Sheria na kuiwasilisha mbele
ya Bunge kwa ajili ya kujadiliwa na hatimaye kupitishwa na kuwa Sheria za Nchi.
Hadi mwezi Machi, 2013 jumla ya Miswada sita (6) iliandaliwa kati ya hiyo, Miswada minne (4) ilipitishwa na kuwa Sheria, miswada miwili (2) bado haijapitishwa. Aidha, kazi ya kuzifanyia urekebu Sheria
zilizopitishwa na Bunge iliendelea kufanyika ambapo Sheria 14 zilifanyiwa urekebu, jumla ya Sheria Ndogo 260 zilitayarishwa na kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali na
Maazimio 11 yaliwasilishwa Bungeni. (Jedwali Na.13).
Vilevile,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilitekeleza jukumu la kutafsiri Sheria
kwa lugha ya kiswahili na kiingereza. Kwa mwaka wa Fedha wa 2012/2013 Ofisi
imetafsiri jumla ya Sheria saba (7)
katika lugha ya Kiswahili. (Kiambatisho
‘B’).
Usimamiaji wa Haki za
Binadamu, Utawala Bora na Masuala ya Katiba
26.
Mheshimiwa
Spika,
kwa upande wa masuala ya Katiba na Haki za Binadamu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali ilipokea maombi ya mashauri ya Kikatiba na Haki za Binadamu 73 na kuhitimishwa 17. Hivyo kubaki mashauri 56
yanayoendelea kusikilizwa. (Jedwali Na.14)
Aidha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliweza kushiriki vikao mbalimbali
kuhusiana na masuala ya haki za binadamu kama vile, Kikao cha Kamati ya Haki za
Binadamu inayosimamia Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na
Kiutamaduni ambapo Taarifa ya Nchi ya Mkataba huo ilijadiliwa Novemba, 2012
huko Geneva, Uswisi; Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Marekani; na
Kikao cha Tume ya Haki za Binadamu na Watu (African Commission on Human and
People’s Rights) kilichofanyika Gambia April, 2013.
Vilevile,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshiriki kwenye wiki ya Maadhimisho ya
Kitaifa ya Haki za Binadamu ambayo hufikia kilele chake tarehe 10 Desemba kila
mwaka kwa kushirikiana na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Wizara ya
Katiba na Sheria. Katika maadhimisho hayo taarifa mbalimbali za Nchi kuhusu
Haki za Binadamu na mapendekezo yanayotolewa na Kamati au Tume zinazosimamia
Mikataba husika ya Kimataifa ya Haki za Binadamu kuhusu Tanzania zilitolewa kwa
wananchi. Madhumuni ya maadhimisho hayo yalikuwa ni kuwawezesha wananchi kufahamu
hali halisi ya Kitaifa katika masuala ya Haki za Binadamu na jinsi Tanzania
inavyotekeleza shughuli za kulinda na kukuza Haki za Binadamu.
27.
Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa fedha wa 2012/2013, Wizara ya Katiba na
Sheria kupitia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ilipanga kudumisha
Utawala Bora nchini kwa kusimamia Utekelezaji wa Haki za Binadamu kama
zilivyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tamko la Umoja wa Mataifa na Tamko la Afrika
la Haki za Binadamu. Katika kutekeleza hili Tume imekamilisha kuandaa Mpango Kazi
wa Kitaifa wa Haki za Binadamu ambao umewasilishwa Serikalini kwa ajili ya
Kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri. Aidha, Tume iliendelea kushughulikia malalamiko ya
wananchi kwa kupokea na kufuatilia malalamiko, kutoa ushauri wa kisheria,
kufanya uchunguzi na utafiti juu ya masuala yanayohusu haki za binadamu na
utawala bora.
28. Mheshimiwa
Spika,
Tume iliendelea kupokea na kushughulikia malalamiko mapya na ya zamani
kulingana na uwezo uliokuwepo. Hadi kufikia mwezi Machi, 2013 Tume ilikuwa
imeshughulikia jumla ya malalamiko 8,350.
Kati ya malalamiko hayo 7,165 ni ya
miaka ya nyuma na 1,185 ni mapya.
Kati ya Malalamiko hayo 688 yalihitimishwa baada ya kupatiwa ufumbuzi na
kubakia na malalamiko 7,662 yanayoendelea kushughulikiwa. (Jedwali
Na.9)
29. Mheshimiwa
Spika,
Tume iliongeza juhudi za kuleta ufumbuzi
wa malalamiko ya wananchi na migogoro ya ardhi. Vilevile, Tume ilikamilisha
uchunguzi na kutoa mapendekezo kwa mamlaka husika kuhusu ukiukwaji wa haki za
watumishi wa mamlaka ya Maji Safi na Taka (DAWASCO), Mgogoro kati ya wafugaji
na wakulima wa Wilaya ya Rufiji, na Mgogoro wa Ardhi Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni. Aidha, Tume iliitisha na kuendesha
vikao vya kujadili taarifa za uchunguzi wa hadharani kuhusu migogoro ya ardhi
na uhamishwaji wa watu katika ardhi yao ulioshirikisha wadau mbalimbali kutoka
Taasisi za Serikali na Binafsi. Vile
vile Tume ilifanya kaguzi katika vituo 100
vya vizuizi (detention facilities) katika Wilaya 21 ili kupima na kutathimini hali na haki za watoto waliozuiwa
katika vituo hivyo.
30.
Mheshimiwa
Spika,
Wizara kupitia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imetoa elimu kwa umma
kuhusu haki za bindamu na utawala bora kupitia vipindi vya redio, luninga na machapisho
mbalimbali. Jumla ya machapisho 38,250
yalisambazwa na wananchi 1,594 walipatiwa
ushauri wa kisheria. Aidha, tume ilitoa mafunzo kwa waandishi wa habari 112 katika Mikoa sita (6) ya Tanzania bara ya Iringa,
Dodoma, Lindi, Morogoro, Mwanza, Tanga na Mjini Magharibi kwa upande wa
Zanzibar.
Uimarishaji wa Shughuli za
Usajili, Ufilisi na Udhamini
31.
Mheshimiwa
Spika,
Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini umeanza mazungumzo na wadau wa usajili wa
watoto ambao ni Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Ofisi ya
Waziri Mkuu TAMISEMI juu ya namna ya kuboresha shughuli za Usajili wa Watoto.
Rasimu ya Mkataba wa Makubaliano kati ya RITA,
Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
kuhusu namna ya kusogeza huduma za usajili wa vizazi na vifo kufikia ngazi ya
kata imekamilika, na rasimu hiyo
inatarajiwa kujadiliwa katika kikao cha
Wadau kitakachofanyika tarehe 3 Mei, 2013.
Utekelezaji wa mpango wa kusajili watoto chini ya umri
wa miaka Mitano unaojulikana kama “U5BRI –
Under 5 Birth Registration Initiative” ulianza kwa majaribio kwa kipindi cha
wiki sita yaliyofanyika kuanzia tarehe 4 Juni, 2012 katika Manispaa ya Temeke.
Jumla ya watoto 15,513 walio na umri
wa chini ya miaka mitano walisajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa. Wakala unaendelea kutekeleza Mpango huo ambao ni mkakati wa kupunguza mlundikano
wa vizazi ambavyo havijasajiliwa. Maandalizi ya kueneza mpango/mkakati huu
yamefanyika katika Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya kwa kufanya utafiti wa awali (Baseline Survey) na kutoa hamasa kwa
makundi mbalimbali ya viongozi kama vile kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), Wakurugenzi wa Halmashauri zote
za Mkoa wa Mbeya, vikao vya Madiwani na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.
Utekelezaji wa Mkakati huu unatarajiwa
kuanza mwezi Juni, 2013.
Sanjari na Mkakati huo wa kusajili
watoto walio na umri chini ya miaka mitano, Wakala pia unatekeleza Mkakati wa
kusajili watoto wa umri kati ya miaka 6 hadi 18 (6-18 Birth Registration Initiative) waliopo mashuleni ambao
umefanyiwa majaribio katika Wilaya ya Igunga. Katika majaribio hayo jumla ya
watoto 1,499 walisajiliwa katika
kipindi cha miezi miwili kuanzia tarehe 18 Februari, 2013 na kupatiwa vyeti vya
kuzaliwa.
32.
Mheshimiwa
Spika, Wakala wa RITA umeendelea kusogeza
huduma za usajili kwa wananchi, kwa kuendesha kampeni za uhamasishaji ambazo
zilipelekea kusajili vizazi 331,272,
vifo 59,099, ndoa 6,094, talaka 42, uasili wa Watoto 23
na kufunga mirathi mmoja, kuandika na kuhifadhi wosia 37.
33.
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu
ya Ufilisi Wakala pia uliteuliwa na Mahakama kuwa mfilisi wa muda ili kusimamia
mali za kampuni ya mitambo ya kufua Umeme ya IPTL. Katika shauri namba 49 la
mwaka 2003 lillilohusu IPTL. Mahakama ya Rufani ilitoa maamuzi ya kufuta amri
ya kuifilisi IPTL iliyotolewa tarehe 17 Disemba, 2012, hivyo Wakala kubaki na
jukumu la kuwa Mfilisi wa muda (Provisional
Liquidator) wa Kampuni hiyo hadi shauri hilo litakapomalizika.
34.
Mheshimiwa
Spika,
katika masuala ya Udhamini, Wakala unajukumu la kusimamia mali zisizokuwa na
uangalizi maalumu, mali zisizokuwa na mwenyewe na zile zinazopaswa kumilikiwa
na watoto walio chini ya umri wa miaka 18 ambao hawana waangalizi maalum (Guardians) kwa mujibu wa Sheria ya
Mdhamini wa Serikali ambapo Wakala (Administrator
General) huteuliwa na Mahakama kama Mdhamini wa Serikali (Public Trustee).
Pia,
Wakala husimamia mirathi baada ya kuombwa na ndugu wa marehemu au kuteuliwa na
Mahakama. Shughuli nyingine inayofanyika ni kusajili Miunganisho ya Wadhamini
ili kuwapatia nguvu ya kisheria ya kumiliki mali kwa niaba ya Taasisi zao. Wadhamini
wa Taasisi za kijamii, kidini, mifuko ya maendeleo ya kijamii, vilabu vya
michezo pamoja na vyama vya siasa husajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya
Muunganisho wa Wadhamini, Sura ya 318 toleo la 2002. Hadi kufikia Machi, 2013, Wakala umesajili Miunganisho ya
Udhamini 204 na kutoa elimu kwa
madhehebu ya dini mbalimbali na kutoa hati za usajili kwa Wadhamini wa Vyama
vya Siasa, Vikundi, Makanisa, Misikiti na Mali zipatazo151. (Jedwali na 10). Pia, Wakala imetembelea vikundi vya Udhamini
katika Wilaya ya Morogoro, Iringa na Arusha.
35.
Mheshimiwa Spika, katika
juhudi za kuboresha mazingira ya kazi Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini unaendelea na
ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Ofisi za Wakala lililopo katika Mtaa wa
Makunganya mjini Dar es Salaam ambao unatarajiwa kukamilika katika mwaka wa
fedha wa 2013/2014.
Uimarishaji wa Vyuo vya
Mafunzo ya Sheria
36.
Mheshimiwa Spika, katika kuiimarisha Taasisi
ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania),
Wizara yangu kupitia Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria (Legal
Sector Reform Programme) imekamilisha ujenzi wa majengo ya kudumu ya
Taasisi hii katika kiwanja Na. 2005/2/1 Sam Nujoma/Mpakani, Sinza, Dar Es
Salaam. Jumla ya Shilingi bilioni 16.1 zilitumika katika ujenzi huo. Kwa sasa Taasisi hii inaendesha mafunzo
katika majengo hayo baada ya kuhamia hapo Agosti 2012. Kukamilika kwa majengo hayo kutaiwezesha
Taasisi hii kuongeza udahili wa wanafunzi kufikia 1,500 kwa mwaka.
37.
Mheshimiwa
Spika, katika kipindi
cha Julai 2012 – Februari 2013 Taasisi hii ilidahili wanafunzi wapya 736. Aidha, Taasisi hii imetoa mafunzo
ya Uanasheria Kwa Vitendo kwa wanafunzi 585
waliosajiliwa katika Mwaka wa Fedha wa 2011/12 ambao walikuwa wanaendelea na
mafunzo. Katika kipindi hicho jumla ya
wanafunzi 1,136 walifanya mitihani
ya mwisho na wanafunzi 409 walifaulu
mitihani hiyo na kupata sifa ya kusajiliwa kuwa Mawakili wa Kujitegemea.
Wanafunzi 861 walitakiwa kurudia
mitihani mbalimbali (supplementary examinations) ya kukamilisha mafunzo yao wakati
wanafunzi 43 walishindwa mitihani.
38.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutoa fedha
kupitia Wizara yangu kwa ajili ya kuwapa ruzuku wanafunzi wahitaji wa Taasisi
hii kwa ajili ya kugharamia mafunzo. Tangu Julai 2012 hadi sasa, jumla ya Shilingi 2,232,558,500.00 zimetolewa na
Serikali kwa ajili ya ruzuku kwa wanafunzi hao. Aidha mchakato wa kurejea
Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Mwaka 2004 umeanza ambapo suala la
Mikopo kwa Wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo yamezingatiwa.
39.
Mheshimiwa
Spika, katika kipindi cha Julai, 2012 hadi
Februari 2013, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (Institute of Judicial Administration) kilidahili wanafunzi 551 wa Mwaka wa Kwanza wa Stashahada ya
Sheria na wanafunzi 634 wa Cheti cha
Sheria. Kulikuwa na wanafunzi 273 wa
Mwaka wa Pili wa Stashahada ya Sheria waliokuwa wanaendelea na mafunzo. Jumla
ya wanafunzi 706 walihitimu mafunzo
ambapo 223 walitunukiwa Stashahada
ya Sheria na 483 walitunukiwa Cheti
cha Sheria. Aidha, Chuo kiliendesha mafunzo ya awali (Induction Course) kwa ajili ya Mahakimu Wakazi wapya 290 waliokuwa wameajiriwa kufanya kazi katika
Mahakama za Mwanzo sehemu mbalimbali hapa nchini. Mafunzo hayo ni sehemu ya Mpango
Mkakati wa Chuo ya kuanzisha na kuendesha mafunzo mahsusi na endelevu kwa
Majaji, Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania. Vile vile, Chuo
kimefikia asilimia 50 ya ujenzi wa
bweni la wanafunzi wa kiume 300
linalotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni, 2013.
Habari,
Elimu na Mawasiliano kwa Jamii
40.
Mheshimiwa
Spika,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inahakikisha uboreshaji wa mfumo wa
teknolojia ya habari, elimu na mawasiliano unapewa umuhimu wa kutosha. Katika
kutekeleza azma hiyo, hatua ya kuunganisha kwenye Mfumo mmoja wa mawasiliano
(WAN) Makao makuu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Divisheni ya
Mashtaka na Kanda ya Dar es Salaam imeanza. Katika kutekeleza hili usimikaji wa
LAN (Local Area Network) ambayo ni
ya kisasa yenye uwezo wa kusafirisha na kupokea sauti, picha na takwimu imeanza
kufungwa Makao Makuu. Lengo ni
kurahisisha, kuboresha mawasiliano na kuongeza ufanisi wa kazi. Aidha, Tovuti
ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (www.agctz.go.tz
) imeendelea kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa mbalimbali kwa
jamii. Pia, “Software” ya kutunza
kumbukumbu za vitabu vya maktaba imekamilika na imeanza kutumika.
Vilevile,
Ofisi imeendelea kutoa elimu kwa umma kwa njia mbalimbali ikiwemo kushiriki
katika vipindi vya redio na luninga juu ya masuala ya Katiba na Haki za
Binadamu, mikataba, uandishi wa sheria, uendeshaji wa mashauri ya madai na
usuluhishi, masuala ya haki jinai pamoja na majukumu ya Ofisi kwa ujumla.
41.
Mheshimiwa
Spika,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendelea kuandaa mtandao wa kompyuta
ujulikanao kama “Case Docket Management
System” utakaowezesha utunzaji wa nyaraka mbalimbali za mashauri nchini.
Mfumo huu utakapokamilika utaimarisha upatikanaji wa takwimu za kesi na masuala
mengine ya uendeshaji mashauri. Ofisi pia ipo katika hatua za usimikaji wa
mfumo wa eletroniki kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu za uendeshaji mashauri
katika ofisi zote za mikoa baada ya kazi ya kufunga mfumo kukamilika katika makao
makuu na mkoa wa Dar es Salaam.
42.
Mheshimiwa
Spika, Wizara pia imekamilisha usimikaji wa
mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu (Data Center)
ambao lengo lake ni kuunganisha mifumo ya utunzaji kumbukumbu za Taasisi zilizo
chini ya Wizara. Sambamba na uimarishaji wa mifumo ya teknolojia, Wizara
iliendelea na jukumu la kutoa elimu kwa umma kwa njia ya vipindi vya redio na luninga
kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utoaji na usimamizi wa haki. Vilevile,
Wizara imeingia Mkataba wa makubaliano na Kampuni Tanzu ya Serikali ya China ya
ZTE Corporation ili kufanya upembuzi
yakinifu wa kusimika mfumo wa “e-justice”
katika Mahakama na Magereza ili kurahisisha usikilizaji wa Kesi. Upembuzi huo yakinifu
umekwishaanza na unaendelea kufanyika. Mpango huu wa kusikiliza kesi kwa kutumia
mfumo maalum wa “e-justice” ilikuwa
ni ahadi yangu wakati nikiwasilisha bajeti ya mwaka 2012/2013 bungeni.
Utaratibu wa kutekeleza Mradi huu unaendelea kwa kuratibiwa na Wizara yangu.
Utekelezaji wa Miradi ya
Maendeleo
43.
Mheshimiwa
Spika, katika kipindi cha Mwaka 2012/2013
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Ufadhili wa Shirika la Umoja wa
Mataifa (UNDP) iliwajengea uwezo wa
kitaalamu Mawakili kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wanasheria na
wataalam wengine walio katika Wizara mbalimbalina Idara za Serikali. Mafunzo
haya yalihusu nyanja za kujadili, kuandika na kuhakiki mikataba kwa lengo la
kuimarisha usimamizi wa hatua zote za majadiliano ya mikataba ili kuweza
kubaini matatizo kabla ya mikataba kusainiwa na hatimaye kuwa na mikataba yenye
maslahi kwa Taifa. Vilevile, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatekeleza
Mradi wa Kujenga Uwezo katika mapambano dhidi ya rushwa (STACA). Kazi zilizofanyika kwa Mwaka 2012/2013 kutokana na mradi
huu ni kufanya mapitio ya Sheria mbalimbali zinazokinzana, kufanya mapitio ya
mafaili ya kesi za rushwa kwa kuzitolea ushauri, maandalizi ya Hadidu za Rejea
kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi wa kutengeneza mwongozo wa maadili kwa
waendesha mashtaka na kuandaa majarida (journals)
mbalimbali ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
44.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na jukumu la kuratibu na
kutekeleza Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria kwa Taasisi zilizo chini ya
Sekta ya Sheria ambazo ni Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Jeshi la Polisi, Jeshi la
Magereza, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo, Tume ya Haki za
binadamu na Utawala Bora na Sekretarieti inayoratibu huduma ya msaada wa
Kisheria (Legal Aid Secretariet).
45.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai hadi Februari 2013
Programu imetekeleza kazi zifuatazo; Kukamilisha ujenzi wa majengo ya kudumu ya
Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania); Kuendesha mafunzo ya Jinsia kwa Watumishi
toka Taasisi zinazotekeleza Programu kwa lengo la kupata wakufunzi
watakaoendelea kutoa mafunzo haya ndani ya Taasisi husika; na kutayarisha
andiko la mchakato wa kuandaa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria. Aidha, wahisani wamekubali
kuongeza kipindi cha utekelezaji wa Programu hii kwa mwaka mmoja zaidi hadi
Juni, 2014 ili kukamilisha malengo yaliyochelewa kufikiwa. Programu ya
Maboresho ya Sekta ya Sheria ilipaswa kuisha Juni, 2013.
Uboreshaji
wa Mazingira ya Kazi na Ujenzi wa Majengo
46.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Mahakama ya Tanzania imekarabati na
kujenga Mahakama kama ifuatavyo;-
i.
Ukarabati wa jengo la Mahakama Kuu Dar es salaam na
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu unaendelea;
ii.
Ujenzi wa mabweni ya chuo cha Mahakama Lushoto unaendelea;
iii.
Ujenzi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi uko katika hatua
ya mwisho ambapo inategemewa kukamilika mwezi juni, 2013;
iv.
Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kisarawe umekamilika;
v.
Ujenzi wa Mahakama Kuu Bukoba umekamilika na awamu ya pili ya ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu
Shinyanga unaendelea;
vi.
Magari 33
yamenunuliwa yakiwemo magari 32 ya
Waheshimiwa Majaji na basi moja (1)kwa
ajili ya watumishi wa Wizara.
Maendeleo
na Ustawi Wa Watumishi
47.
Mheshimiwa Spika, katika kuleta
ufanisi na tija kazini jumla ya watumishi 579
wa Wizara na Taasisi zake wamepatiwa mafunzo ya muda mrefu na mfupi katika fani
mbalimbali, nje na ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na mafunzo kazini (on
job training). Watumishi 13 wamepandishwa vyeo na watumishi 15 walihudhuria mikutano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa
kuiwakilisha Wizara katika masuala mbalimbali. Aidha, Tume ya Utumishi wa Mahakama hadi
kufikia mwezi Februari, 2013 imefanya vikao viwili (2) vya kawaida na vikao viwili (2) vya dharura ambapo watumishi 17 waliajiriwa katika masharti ya kudumu na malipo ya
pensheni; Mahakimu 98 walithibitishwa
katika cheo pamoja na kuthibitisha kazini Hakimu mmoja (1). Tume kupitia vikao hivyo ilishughulikia masuala saba (7) ya kinidhamu ambapo sita
walirejeshwa kazini na mmoja (1)
alifukuzwa kazi.
48.
Mheshimiwa
Spika,
Tume ya Utumishi wa Mahakama ilikamilisha mchakato wa kumpata Mtendaji Mkuu wa
Mahakama, Msajili Mkuu wa Mahakama, Msajili wa Mahakama ya Rufani na Msajili wa
Mahakama Kuu. Tume pia ilifanya ziara Katika Mikoa ya Mwanza, Mara, na Kagera
kwa lengo la kutoa elimu kwa watumishi wa Mahakama na Kamati za Maadili za
Mikoa na za Wilaya kuhusu utendaji wake. Aidha, Tume imekagua Kamati za Maadili
za Mikoa na Wilaya katika Mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Manyara, Dodoma,
Morogoro na Pwani. Lengo la ukaguzi huu ni kufuatilia uzingatiaji wa Sheria,
Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
C.
CHANGAMOTO
49.
Mheshimiwa
Spika,
Wizara yangu imeendelea kutekeleza Majukumu yake ya msingi na kupata mafanikio
mbalimbali. Hata hivyo Wizara pia imeendelea kukabiliwa na changamoto. Baadhi
ya Changamoto hizi ni kama ifuatavyo:-
(i)
Baadhi ya Taasisi kukosa Ofisi zake za kudumu na hivyo kutumia gharama kubwa kwa
ajili ya kulipia pango;
(ii)
Bajeti inayotengwa kwenye Wizara na Taasisi
zake imeendelea kuwa pungufu ikilinganishwa na mahitaji halisi ya kutekeleza majukumu ya Wizara ambayo yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka;
(iii)
Wizara inakabiliwa na upungufu wa rasilimali
watu katika Taasisi zake, hali ambayo inaathiri ufanisi
wa utoaji haki kwa wananchi;
(iv)
Baadhi ya wananchi kukosa imani na vyombo
vya utoaji haki kutokana na baadhi ya watumishi wasio waadilifu kuendelea
kulalamikiwa kwa kujihusisha na Vitendo vya Rushwa;
(v)
Suala la Mikopo kwa wanafunzi wa Taasisi ya
Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo limekuwa tatizo kubwa kwa Wizara na kwa
wanafunzi husika ambao ni wahitimu wa
Shahada ya Kwanza. Hali hii inatokana na Sheria ya Bodi ya Mikopo inayowaruhusu wanafunzi wa Shahada
ya Kwanza “undergraduate” peke yake kupata mikopo hiyo;
(vi)
Uwezo na uelewa mdogo wa wananchi walio
wengi kutumia vyombo vya kutoa haki na huduma za Kisheria kuhusu mfumo uliopo
wa Sheria; na
(vii)
Mazingira ya kazi yasiyoridhisha kwa
watumishi walio wengi yanayotokana na maslahi duni na uhaba wa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na vyombo vya
usafiri.
D.
MIKAKATI
YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
50.
Mheshimiwa
Spika,
katika juhudi za kuzipatia ufumbuzi changamoto nilizozielezea, Wizara pamoja na
Taasisi inaendelea kuchukua hatua zifuatazo:-
(i)
Kuendelea kuomba na kufuatilia vibali ili kujaza
nafasi zilizo wazi katika Muundo na kurejea Miundo ili itosheleze mahitaji ya Taasisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa
Umma;
(ii)
Kuboresha mazingira
ya kazi kwa kujenga na kukarabati Majengo ya Mahakama na ofisi za Wizara na Taasisi;
(iii)
Kuendelea kuainisha vipaumbele
vya Wizara na Taasisi zake na kujenga hoja ya kuongezewa Bajeti kulingana na
uwezo wa Serikali;
(iv)
Kuwajengea watumishi
uwezo na ujuzi wa taaluma zao;
(v)
Kuimarisha uwajibikaji na uadilifu kwa
kusimamia vyema Sheria, Kanuni
, Taratibu na Miongozo
ya utekelezaji wa majukumu;
(vi)
Kufanya mawasiliano na Uongozi wa Bodi ya
Mikopo ya Elimu ya Juu na kupendekeza Marekebisho
ya Sheria iliyoanzisha Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo ya Mwaka 2007 kufanyika ili kulipatia ufumbuzi tatizo la Mikopo kwa Wanafunzi wenye Shahada ya Kwanza ya Sheria;
(vii)
Kuendelea kutoa elimu ya Sheria na kusogeza
huduma za Kisheria kwa wananchi; na
(viii)
Kuongeza idadi ya Mawakili wa Serikali,
Majaji, Mahakimu na watumishi wa kada nyingine ili kuongeza kasi ya uendeshaji
wa mashauri mbalimbali nchini. Lengo ni
kulipatia ufumbuzi suala la mlundikano
wa mashauri mahakamani
na msongamano wa Mahabusu na Wafungwa
Magerezani.
E.
MPANGO
NA MALENGO YA MWAKA 2013/2014
51.
Mheshimiwa
Spika,
baada ya kuelezea utekelezaji wa majukumu ya Wizara yangu kwa Mwaka wa Fedha wa
2012/2013, sasa napenda kulielezea Bunge
lako Tukufu Mpango na Malengo ya Wizara yangu kwa Mwaka 2013/2014 kama
ifuatavyo:
i. Kutoa elimu na habari kuhusu
utoaji wa haki kwa jamii;
ii. Kuimarisha utoaji wa huduma za Kisheria;
iii. Kuhakiki na kushiriki
majadiliano ya mikataba mbalimbali;
iv. Kuboresha
miundombinu ya utoaji haki;
v. Kusikiliza na kuendesha
Mashauri nchini;
vi. Kufanya
tafiti na tafasiri za Sheria;
vii. Uandishi wa Sheria na Hati
za Serikali;
viii. Kuimarisha
Taasisi za Mafunzo ya Sheria;
ix. Kuimarisha
shughuli za Usajili, Ufilisi na Udhamini;
x. Kuimarisha Haki za
Binadamu na Utawala Bora;
xi. Kuratibu mchakato wa
Mabadiliko ya Katiba;
xii. Uratibu na
utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria na miradi ya maendeleo;
na
xiii. Kuimarisha
Usimamizi na Uwajibikaji katika rasilimali.
52.
Mheshimiwa
Spika,
katika Mwaka 2013/2014 Wizara itatekeleza
Mpango na Malengo yake ambayo yamezingatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali
katika Mwongozo wake wa Utayarishaji Mpango na Bajeti kwa kuzingatia
Vipaumbele vya Taifa na Kisekta
vilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa
Miaka Mitano na Mpango wa Pili wa Mwaka Mmoja mmoja, MKUKUTA II na Ilani
ya Uchaguzi ya CCM (2010 – 2015). Wizara
ya Katiba na Sheria ikiwa moja ya Wizara zilizo chini ya Nguzo ya Tatu ya
MKUKUTA II ya Utawala Bora na Uwajibikaji, mkazo na msukumo utawekwa katika
kuhakikisha kunakuwa na rasilimali za kutosha na mikakati ya utekelezaji wa mpango
vinawekwa ili kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria na uwajibikaji katika
kusimamia matumizi ya rasilimali na upatikanaji wa haki kwa wakati ikiwa ni
pamoja na kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa ufanisi.
Aidha,
Mpango na Malengo ya Wizara yangu yamelenga kutoa kipaumbele cha kusogeza huduma za utoaji haki karibu na
wananchi kwa kuendelea kuimarisha na kujenga miundombinu muhimu ya utoaji haki,
kujenga uwezo wa watumishi na kuongeza vitendea kazi katika Sekta ya Sheria.
Malengo yafuatayo yatatekelezwa:-
Kutoa elimu, habari na
mawasiliano ya utoaji haki kwa jamii
53.
Mheshimiwa
Spika,
Wizara yangu itaendelea Kuboresha Mfumo wa matumizi ya TEHAMA katika
usikilizaji wa mashauri na utunzaji kumbukumbu pamoja na Takwimu mbalimbali. Hivyo,
kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 Wizara itatekeleza yafuatayo:-
i.
Kuendelea kupanua mtandao wa kielektroniki
kwa ajili ya kusikiliza/kuendesha Mashauri na
shughuli mbalimbali za kiofisi;
ii.
Kuandaa Sera na Mkakati wa TEHAMA kwa Wizara
na Mahakama;
iii.
Kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu kwa
kutumia mtandao wa kompyuta;
iv.
Kuongeza matumizi ya kompyuta katika
shughuli mbalimbali za kiofisi;
v.
Kuimarisha mafunzo ya
ujuzi wa TEHAMA; na
vi.
Kutayarisha programu mbalimbali
zitakazojadiliwa kwenye vyombo vya habari kwa ajili ya kuelimisha umma kuhusu masuala
ya Sheria, haki za binadamu na utawala bora na majukumu ya Wizara pamoja na
Taasisi zake kwa ujumla.
Kuimarisha utoaji wa
huduma za Kisheria
54.
Mheshimiwa
Spika, Wizara itaendelea na mchakato wa
kutunga Sheria itakayoratibu Utoaji wa Huduma za Kisheria kwa Umma na kutambua watoa huduma za msaada wa Kisheria
kwa umma ikiwa ni pamoja na wasaidizi wa kisheria (Paralegals). Aidha, Wizara itendelea kupokea na kushughulikia malalamiko
mbalimbali toka kwa wananchi yanayohusu upatikanaji wa haki zao.
Kuhakiki na kushiriki majadiliano
ya mikataba mbalimbali
55.
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali itahakikisha kuwa maslahi ya taifa yanapewa kipaumble katika
mashirikiano ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Aidha, mashirikiano haya
yanakuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya wananchi kwa ujumla. Katika
kutekeleza lengo hili, ofisi imepanga kutekeleza shughuli zifuatazo:-
(i)
Kushiriki
katika masuala ya Mtangamano wa Kikanda kwa maslahi ya taifa;
(ii)
Kutoa
ushauri wa kisheria na kufanya majadiliano ya mikataba ya kibiashara na
mikataba ya mahusiano ya kikanda na kimataifa (Contracts & Treaties);
(iii)
Kuimarisha
uwezo wa kutayarisha taarifa mbalimbali zinazojadiliwa katika mikutano ya
kikanda na kimataifa;
(iv)
Kushiriki
katika mikutano ya Kamati mbalimbali za uanachama wa vyombo mbalimbali
vinavyohusika na uendeshaji wa mashauri ya jinai, madai, kikatiba na haki za
binadamu.
Kuboresha
Miundombinu ya Utoaji Haki
56.
Mheshimiwa
Spika, kwa Mwaka 2013/2014 Wizara yangu
kupitia Mahakama imepanga kuendelea na ujenzi wa Mahakama Kuu ya Shinyanga na kuanza
ujenzi wa Mahakama kuu katika mikoa ya Kigoma, Mara, Lindi na Morogoro. Aidha, Kanda
maalum ya Mahakama Kuu Ilala na baadaye Temeke na Kinondoni zitaanzishwa ili
kuweza kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
57.
Mheshimiwa
Spika,
katika kuboresha mazingira ya kazi Mahakama itaanza ujenzi wa nyumba za Majaji
katika Mkoa wa Dar es Salaam na pia kuboresha masjala za Mahakama Kuu, Mahakama
za Hakimu Mkazi, Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo kwa kuanzia na zile
zilizoko mijini.
Aidha,
Mahakama pia itafanya upanuzi wa jengo la Mahakama Kuu Dodoma na kuanza ujenzi
wa Mahakama za Mwanzo za Bunda, Ludewa, Bariadi, Kawe, Mkomazi, Mailimoja,
Lukuledi, Gairo, Mangaka na Nyamikoma.
58.
Mheshimiwa
Spika,
Mahakama pia ipo katika hatua za awali za kuanzisha Programu maalum ya ujenzi
wa Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri
Mkuu- TAMISEMI, Mikoa, Wilaya na Halmashauri husika. Ni matumaini yangu makubwa
kuwa Programu hiyo itasaidia katika kufanikisha lengo kuu la Wizara la kusogeza
huduma karibu na wananchi.
59.
Mheshimiwa
Spika,
Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaendelea kuimarisha Ofisi
mpya zilizoanzishwa katika Mikoa na Wilaya kwa kuzijengea uwezo wa kuendesha mashauri
mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utoaji haki kwa ujumla. Aidha, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali itafungua Ofisi mpya katika Mikoa ya Geita,
Simiyu, Katavi na Ofisi moja (1) katika
Wilaya ya Tarime. Vilevile, Wizara itafanya ukarabati wa jengo la Ofisi za
Wizara (Makao Makuu) na kukamilisha ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya RITA. Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora itaendelea kuimarisha Ofisi zake za kanda na
itaanzisha Ofisi nyingine za kanda za Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma.
Kusikiliza na kuendesha
Mashauri nchini
60.
Mheshimiwa
Spika,
Wizara yangu itaendelea kusikiliza na kuyatolea maamuzi mashauri katika ngazi
mbalimbali za Mahakama, kupitia Programu maalum ya kumaliza mlundikano wa
mashauri ya nyuma 1,918 yaliyoko
Mahakama ya Rufani, 12,093 Mahakama
Kuu, 329 yaliyoko Mahakama Kuu –
Divisheni ya Biashara, 1,780
yaliyoko Mahakama Kuu- Divisheni ya Kazi, 5,393
yaliyoko Mahakama Kuu – Divisheni ya Ardhi, 25,370 yaliyoko Mahakama za Hakimu Mkazi, 21,538 yaliyoko Mahakama za Wilaya na 197,715 yaliyoko Mahakama za Mwanzo.
Aidha,
Mahakama pia itaongeza kasi ya usikilizaji wa mashauri katika ngazi za Mahakama
za Mikoa (RMs na Wilaya) kwa kutenganisha shughuli za Kimahakama na za
Kiutawala. Vilevile, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaendesha mashauri
ya Madai, Katiba na Jinai na kushughulikia mashauri ya zamani na mengine mapya
yatakayopokelewa.
Kufanya
Utafiti na Tafasiri ya Sheria
61.
Mheshimiwa
Spika, kwa Mwaka 2013/2014 Wizara yangu
itaendelea kufanya mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazosimamia huduma za jamii kwa
wazee, Sheria zinazomlinda Mlaji na Sheria za makosa ya jinai. Kutafsiri Sheria
kutoka lugha ya kingereza kwenda Kiswahili, kufanya uchambuzi wa hukumu za kesi
za Mahakama ya Rufani ili kuainisha misingi ya kisheria na kuziweka kwenye
tovuti ya Tume ya Kurekebisha Sheria.
Aidha,
Wizara yangu itafanya mapitio ya Sheria mbalimbali ili kuhakikisha kuwa
hazikinzani na Katiba ya Nchi na Misingi ya Haki za Binadamu.
Uandishi wa Sheria na Hati
za Serikali
62.
Mheshimiwa
Spika,
kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Mfumo wa Sheria nchini unaokidhi mahitaji ya
jamii katika kujiletea maendeleo kiuchumi, kijamii na kiteknolojia, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali itatekeleza yafuatayo:-
(i)
kusimamia uandishi, tafsiri
na urekebu wa Sheria mbalimbali za Nchi;
(ii) kutayarisha
maazimio mbalimbali ya kimataifa ambayo Nchi
imeweka saini ili yaridhiwe na Bunge; na
(iii) kuwezesha
upatikanaji wa Sheria mbalimbali
zilizotungwa na Bunge.
Kuimarisha
Taasisi za Mafunzo ya Sheria
63.
Mheshimiwa
Spika,
Wizara yangu itaendelea kuimarisha Taasisi za Mafunzo ya Sheria kwa kuanzisha
ushirikiano maalum wa maendeleo ya watumishi kati ya Mahakama, Chuo cha Uongozi
wa Mahakama na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania.
Kuimarisha
shughuli za Usajili, Ufilisi na Udhamini
64.
Mheshimiwa
Spika,
Wizara yangu imeendelea kuimarisha shughuli za wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini (RITA) ili kuhakikisha kwamba lengo la Taasisi hii la kuwa Wakala linafikiwa
kwa ufanisi. Katika Mwaka wa Fedha 2013/2014 Wakala unatarajia kuupeleka Mfumo
wa Usajili wa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano (Under 5 Births Registration Initiative - U5BRI) hadi ngazi ya
Serikali za Mitaa, ili kupunguza mlundikano wa vizazi ambavyo havijasajiliwa na
kumwezesha mtoto kupata cheti cha kuzaliwa ambacho ni haki yake ya msingi. Mpango
huu unatarajiwa kuanza rasmi katika Mkoa wa Mbeya na kuendelea kuutekeleza
katika Mikoa ya Simiyu, Geita, Shinyanga na Mwanza. Katika Mfumo huu, utoaji wa
vyeti vya kuzaliwa kwa mara ya kwanza hutolewa bila tozo kwa watoto wote walio
na umri wa chini ya miaka mitano. Aidha, Wakala pia utatekeleza Mkakati wa kusajili watoto
wa umri kati ya miaka 6 hadi 18 (6-18
Birth Registration Initiative) waliopo mashuleni kwa kutumia Bajeti ya
Serikali.
Vilevile Wakala unatarajia kuanzisha mazungumzo kati yake
na NIDA - pamoja na Uhamiaji ili kuona namna ya kupunguza gharama za usajili
kwa kutumia Mifumo ambayo tayari ipo kwa ajili ya uandikishaji na uchapishaji
wa vyeti.
Kuimarisha Haki
za Binadamu na Utawala Bora
65.
Mheshimiwa
Spika,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa Sheria na
taratibu zilizowekwa na mamlaka mbalimbali kuhusu haki za binadamu zinafuatwa
wakati wote wa utekelezaji wa majukumu mbalimbali. Kwa kuzingatia hilo, Ofisi
imedhamiria kufanya yafuatayo:-
(i) kutoa
ushauri wa kisheria ulio bora katika masuala ya Katiba na Haki za Binadamu;
(ii) kuandaa
taarifa za utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu nchini kwenye mikataba ya
kikanda na kimataifa ya Haki za Binadamu ambayo Nchi
imeridhia na kuziwasilisha kwenye vyombo husika kwa ajili ya majadiliano; na
(iii) kufanya
ukaguzi katika maeneo yanayohifadhi mahabusu na wafungwa ili kutoa ushauri wa
namna ya kuboresha.
66.
Mheshimiwa
Spika, Wizara yangu kupitia Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora itaendelea kulinda, kukuza na kuhifadhi haki za binadamu
na utawala bora. Katika Mwaka 2013/2014 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora itaendelea kukamilisha uchunguzi wa mashauri ya uvunjwaji wa haki za binadamu
ambao haukukamilika, kufanya tafiti kuhusu haki za binadamu na utawala bora;
kupitia miswada na Sheria ili kuangalia kama zinakidhi vigezo vya kimataifa na
vya kikanda ili kulinda haki za binadamu na utawala bora; na kukagua Magereza
na Vituo vya Polisi na Sehemu nyinginezo wanamozuiliwa watu.
Aidha,
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora itaendelea kushughulikia malalamiko
yaliyosalia na yatakayopokelewa yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu.
67.
Mheshimiwa Spika, katika kusimamia maadili ya Mahakimu, Wizara yangu
kupitia Tume ya Utumishi wa Mahakama itaendelea kuzijengea uwezo Kamati za
maadili za Mikoa na Wilaya kwa Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara Tanga,
Dodoma na Singida kwa kuzipatia mafunzo ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa
ufanisi. Aidha, Tume itaendelea na kazi ya kukagua Kamati za Maadili za Mkoa na
Wilaya kwa Mikoa ya Mtwara, Lindi, Mbeya, Rukwa na Katavi. Lengo likiwa ni
kuona kama zinatekeleza majukumu yake kwa misingi ya sheria na taratibu. Tume
itaitisha vikao vinne vya kawaida kwa ajili ya kujadili na kuamua masuala
mbalimbali ya watumishi.
Kuratibu mchakato wa
Mabadiliko ya Katiba
68.
Mheshimiwa
Spika,
Wizara yangu itaendelea kuratibu jambo kubwa na la kihistoria nchini mwetu
ambalo ni mchakato wa mabadiliko ya Katiba. Awamu ya kwanza ya ukusanyaji wa
maoni ya wananchi na makundi mbalimbali imekamilika. Hivi sasa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba inaendelea na uchambuzi wa maoni hayo ili kuandaa Rasimu
ya Katiba itakayowasilishwa kwenye Mabaraza ya Katiba. Aidha, katika Mwaka wa fedha
2013/2014, Wizara yangu kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba inategemea kufanya
mambo yafuatayo ili kukamilisha Mchakato huu wa mabadiliko ya Katiba:-
(i)
Kusimamia Mikutano ya Mabaraza ya Katiba;
(ii)
Kuchambua maoni yatakayo tolewa na wajumbe wa Mabaraza
ya Katiba;
(iii)
Kuchapisha
Ripoti na Rasimu ya Katiba;
(iv)
Kuwasilisha
Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalum la Katiba; na
(v)
Kutoa
elimu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika Kura ya Maoni.
69.
Mheshimiwa
Spika,
kutokana na umuhimu wa mchakato huu wa mabadiliko ya Katiba, kupitia kwenu Waheshimiwa
Wabunge, ninaomba muwahamasishe wananchi wa majimbo yenu ili waweze kujitokeza kwa
wingi katika kutoa mawazo kuhusu Rasimu ya Katiba kupitia kwa wajumbe wanaounda
Mabaraza ya Katiba. Nawahamasisha na kuziomba Taasisi, Asasi za kiraia, jumuia za
kidini, vyama vya siasa na makundi mengine yote kuunda Mabaraza ya Katiba. Aidha,
ninawaomba wajumbe wa mabaraza kutoa mawazo yao kwa uwazi, uhuru na bila ya hofu
yoyote. Pia nipende kuwahakikishia wananchi kuwa Tume inafanya kazi zake kwa uhuru
na uwazi, na kwamba maoni yote yaliyotolewa na yatakayotolewa na wananchi,
Taasisi, Asasi za Kiraia na makundi mengine yanaheshimiwa na kufanyiwa kazi ipasavyo.
Uratibu na
utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria na Miradi ya maendeleo
70. Mheshimiwa
Spika, Wizara yangu itaendelea kutekeleza Mpango Mkakati
wa Muda wa Kati
(Medium
Term Strategy) wa Programu hii, kwa kuendelea kuziwezesha Taasisi
zinazotekeleza Programu hii kuboresha Mfumo wa Sheria na kuimarisha mazingira
ya kisheria yanayoongeza fursa ya wananchi ya kupata haki kwa wakati ili
kuwezesha jamii kutumia muda wao mwingi katika
kujihusisha na kazi za maendeleo ya kiuchumi na kijamii, badala ya kupoteza
muda huo, wakitafuta haki. Aidha, napenda kulitaarifu Bunge lako tukufu kuwa, Wizara
imekwisha anza kujiandaa kukamilisha
na hatimaye kufunga programu kwa kuanza kutekeleza kazi ya kufanya tathimini ya
hali ya sasa ya Sekta hii (Legal Sector Assessment) ili kujua kiwango cha maendeleo kilichofikiwa,
kubaini changamoto zinazoikabili Sekta hii
na kutambua fursa zilizopo na ambazo zinaweza kutumika kikamilifu katika
mipango hiyo ya kuboresha sekta hii muhimu.
71. Mheshimiwa
Spika, Wizara yangu imeendelea kubuni mbinu na kuanzisha miradi
mbalimbali ya maendeleo ya kuboresha huduma zitolewazo na Taasisi mbalimbali za
Sheria, ili kuweza kufikia dira yetu ya ‘haki sawa kwa wote
na kwa wakati’. Kama ambavyo nililiarifu Bunge lako Tukufu mwaka uliopita kwamba, Wizara yangu
imebuni na itaanzisha Mradi wa “e-justice”,
ninafurahi kulialifu Bunge lako Tukufu kwamba, tayari hatua za awali za Mradi huu zimekwishaanza
na Serikali ya China imeridhia kufadhili mradi huu. Tayari kazi ya upembuzi
yakinifu wa Mradi huo inafanywa na Kampuni ya ZTE Corporation,
iliyokasimiwa kazi hiyo na Serikali ya China. Kutegemea na taarifa ya upembuzi
yakinifu wa Mradi huu itakayo andaliwa, Wizara
yangu itatekeleza Mradi huu kwa awamu tatu.
Awamu
ya kwanza ikiwa ni majaribio (Pilot
Study) kwa Mkoa wa Dar es Salaam, kisha kuhusisha Mikoa yote yenye Kanda za
Mahakama Kuu kwa awamu ya pili na awamu ya tatu
kukamilisha Mradi kwa kufikia Mikoa yote
Tanzania Bara.
72.
Mheshimiwa Spika, katika
kuzingatia umuhimu wa kuwepo na
Mikataba mizuri yenye maslahi kwa taifa,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, itaendelea kuwajengea uwezo wa kitaalam
Mawakili wa Serikali katika nyanja za kujadili, kuandika
na kuhakiki mikataba kupitia Mradi wa UNDP- unaofadhiliwa na
Shirika la Umoja wa Mataifa – UNDP.
Katika uendeshaji wa mashauri ya
rushwa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaendelea kutekeleza
Mradi wa Uimarishaji wa Mapambano Dhidi ya Rushwa Tanzania (STACA) kwa kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali katika uendeshaji
wa mashauri ya rushwa, ununuzi wa
vitendea kazi, uimarishaji wa mfumo wa
utunzaji na usimamizi wa kumbukumbu za mashauri kielektroniki
(Case Docket Management
System).
Kuimarisha
Usimamizi na Uwajibikaji katika rasilimali
73.
Mheshimiwa
Spika, Wizara
yangu imezingatia lengo hili katika mipango yake ili kuhakikisha kwamba
kunakuwa na usimamizi madhubuti wa rasilimali mbalimbali za Serikali. Katika
kufanikisha lengo hili mambo yafuatayo yatafanyika:-
(i)
Kufanya
ukaguzi wa matumizi ya fedha katika Ofisi za Makao Makuu na Mikoa kwa Taasisi
zote za Wizara;
(ii)
Kufanya
ukaguzi wa vifaa mbalimbali vilivyopo na vinavyonunuliwa katika Ofisi zote;
(iii)
Kutayarisha
ratiba ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa malengo yaliyopangwa na Wizara na
Taasisi zake ili kuwezesha utekelezaji na utoaji wa taarifa;
(iv)
Kuimarisha
uratibu, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango ya Wizara;
(v)
Kuimarisha
uwajibikaji na uadilifu katika utendaji wa kazi katika ngazi mbalimbali;
(vi)
Kuwaongezea
watumishi maarifa na ujuzi katika maeneo yao ya kitaalam ili wawe na tija
wakati wa kutekeleza majukumu yao hasa katika maeneo ambayo yameonekana kuwa na
changamoto nyingi katika kuleta ufanisi wa utendaji; na
(vii)
Kuandaa
Mpango thabiti wa rasilimali watu kwa Wizara na Taasisi na kuchambua mahitaji
ya ujuzi kwa kila eneo la utekelezaji.
F.
SHUKRANI
74.
Mheshimiwa
Spika,
naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru sana wadau wetu wa maendeleo kwa
kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha Sekta yetu ya Sheria. Kwa
namna ya pekee napenda kushukuru nchi za CANADA na Denmark ambazo kupitia
Mashirika yao ya Kimataifa ya Maendeleo ya CIDA
na DANIDA wameisaidia sana Wizara
yangu katika kushawishi Mashirika na nchi nyingine wahisani kuelekeza misaada
yao katika kuboresha Sekta ya Sheria. Nayashukuru pia Mashirika na Taasisisi za
Kimataifa zifuatazo: - Benki ya Dunia (WB),
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Watoto (UNICEF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) na Taasisi ya Maendeleo ya
Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (DFID).
75.
Mheshimiwa
Spika,
napenda kutoa shukrani za pekee kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Sheria kwa
ushirikiano na ushauri uliowezesha kutekelezwa kwa majukumu ya Wizara kwa mwaka
2012/2013 kama yalivyobainishwa katika Hotuba hii. Ninapenda kumshukuru Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Angela
Kairuki (Mbunge), Jaji Mkuu Mheshimiwa Othmani
Chande, Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Mheshimiwa Frederick Mwita Werema, Jaji Kiongozi Mheshimiwa Fakih A.R Jundu, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Katiba na Sheria ndugu Fanuel
E.Mbonde, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ndugu Hussein Kattanga, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndugu George Masaju, Msajili Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania, ndugu Ignas Paul Kitusi,
Mkurugenzi wa Mashtaka Dr. Eliezer M.
Feleshi, Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Winifrida Korroso,
Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi.Mary Massey, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo Mheshimiwa Dr. Gerald Ndika,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa RITA, ndugu
Philip Saliboko, Wakurugenzi wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Wizara na
Watumishi wote kwa ushirikiano na kazi kubwa waliyoifanya katika kuandaa Mpango
na Bajeti hii kwa wakati. Ni matarajio yangu kwamba Wizara itaendelea kupata
ushirikiano wao katika mwaka 2013/2014 kama walivyofanya nitekeleze majukumu
yangu na wajibu wangu kwa ufanisi hadi sasa. Mwisho nitoe shukrani kwa Mpiga
Chapa Mkuu wa Serikali kwa kufanikisha uchapishaji wa Hotuba hii.
G.
MAJUMUISHO
76.
Mheshimiwa
Spika,
tukitambua kwamba Sekta ya Sheria ndio jiwe la msingi katika utawala wa
Serikali na kwa kuzingatia umuhimu wa Sekta ya Sheria katika kuchochea
maendeleo ya Nchi kiuchumi, kisiasa, kijamii, kisayansi na kiteknolojia, Wizara
ya Katiba na Sheria inao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba inakuza,
inaimarisha na inalinda amani na utulivu na kudumisha haki za binadamu na
utawala wa Sheria nchini.
Napenda
kutoa wito kwa wananchi wote na Waheshimiwa Wabunge kuhakikisha kuwa azma ya
Serikali ya kulinda Amani, Utulivu na Haki za Binadamu inazingatiwa,
inaendelezwa na kupewa kipaumbele kwa manufaa ya Taifa letu na kizazi kijacho.
H.
MAOMBI
YA FEDHA KWA MWAKA 2013/2014
77.
Mheshimiwa
Spika, katika Mwaka wa fedha 2012/2013
Wizara ya Katiba na Sheria ilitetengewa jumla ya Sh. 186,323,718,000. Hadi kufikia tarehe 28 Februari, 2013 jumla ya
Sh.86,005,210,966.19. Ili kutekeleza
majukumu yaliyopangwa kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014, Wizara yangu inaomba kuidhinishiwa
kiasi cha Sh.230,687,333,000 kwa ajili ya Taasisi, Idara na Vitengo vya
Wizara. Matumizi ya Kawaida yanayoombewa jumla ya Sh.195,427,547,000. Kati
ya fedha hizo, Sh.152,890,448,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na Sh.42,537,099,000
ni kwa ajili ya Mishahara. Miradi ya Maendeleo inaombewa jumla ya Sh.35,259,786,000.
Kati ya fedha hizi Sh.24,000,000,000 ni za ndani na Sh.11,259,786,000
ni fedha za nje. Mchanganuo wa matumizi ya bajeti kwa mafungu ya Wizara ni kama
ifuatavyo:
MATUMIZI:
Fungu 8: Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Matumizi Mengineyo
Sh.33,944,588,000/=
Jumla Sh.
33,944,588,000/=
Fungu
12: Tume ya Utumishi wa Mahakama
Matumizi ya Mishahara Sh. 161,882,000/=
Matumizi Mengineyo
Sh.2,871,716,000/=
Jumla Sh. 3,033,598,000/=
Fungu
16: Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Matumizi ya Mishahara Sh.
2,174,186,000/=
Matumizi Mengineyo Sh.8,332,865,000/=
Matumizi ya Maendeleo
(nje) Sh.826,000,000/=
Jumla Sh.11,333,051,000/=
Fungu 35: Mkurugenzi wa Mashtaka
Matumizi ya Mishahara Sh. 4,383,211,000/=
Matumizi Mengineyo Sh. 6,460,826,000/=
Matumizi ya
Maendeleo(nje)Sh.2,167,759,000/=
Jumla Sh.13,011,796,000/=
Fungu
40: Mahakama
Matumizi ya Mishahara Sh. 30,980,157,000/=
Matumizi Mengineyo Sh.
86,600,000,000/=
Matumizi ya Maendeleo(ndani)
Sh.
20,000,000,000/=
Matumizi ya
Maendeleo(nje)Sh.2,716,668,000 /=
Jumla Sh.140,296,825,000/=
Fungu
41: Wizara ya Katiba na Sheria
Matumizi ya
Mishahara Sh. 2,447,110,000 /=
Matumizi Mengineyo Sh.
8,028,651,000 /=
Matumizi ya Maendeleo (ndani)
Sh.4,000,000,000/=
Matumizi ya Maendeleo.(nje)
Sh.
3,898,840,000/=
Jumla Sh.18,374,601,000/=
Fungu
55: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Matumizi ya Mishahara Sh.1,814,993,000/=
Matumizi
Mengineyo Sh.3,795,802,000/=
Matumizi ya Maendeleo (nje) Sh.1,034,169,000/=
Jumla Sh.
6,644,964,000 /=
Matumizi ya Mishahara Sh.
575,560,000/=
Matumizi Mengineyo Sh. 2,856,000,000/=
Matumizi ya Maendeleo(nje) Sh. 616,350,000 /=
Jumla Sh. 4,047,910,000/=
I.
MAKUSANYO
YA MADUHULI
78.
Mheshimiwa
Spika, Wizara yangu kwa Mwaka 2013/2014 inatarajia kukusanya jumla
ya kiasi cha Sh.5,250,454,700/= kama
maduhuli ya Serikali. Mchanganuo wa makusanyo kwa mafungu husika ni kama
ifuatavyo:
Fungu 16: Sh.
3,002,000/=
Fungu 40: Sh. 2,261,303,900/=
Fungu 41: Sh. 2,983,648,800/=
Fungu 55: Sh. 2,500,000/=
Jumla Sh. 5,250,454,700/=
79.
Mheshimiwa
Spika,
mchanganuo wa maombi ya fedha kwa kila Fungu umeainishwa kwenye Randama
zilizoandaliwa kwa kila Fungu na kuwasilishwa hapa Bungeni rasmi.
80.
Mheshimiwa
Spika,
naomba kutoa hoja.
Kiambatisho ‘A’
MGAWANYO
WA FEDHA ZA MATUMIZI YA KAWAIDA NA MAENDELEO KITAASISI KWA MWAKA WA FEDHA
2013/2014
|
||||||
FUNGU
|
MAELEZO
|
MISHAHARA
|
MATUMIZI
MENGINEYO
|
MAENDELEO
NDANI
|
MAENDELEO
NJE
|
JUMLA
|
8
|
Tume ya Mabadiliko ya Katiba
|
-
|
33,944,588,000
|
-
|
-
|
33,944,588,000
|
12
|
Tume ya Utumishi wa Mahakama
|
161,882,000
|
2,871,716,000
|
-
|
-
|
3,033,598,000
|
16
|
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
|
2,174,186,000
|
8,332,865,000
|
-
|
826,000,000
|
11,333,051,000
|
35
|
Mkurugenzi wa Mashtaka
|
4,383,211,000
|
6,460,826,000
|
-
|
2,167,759,000
|
13,011,796,000
|
40
|
Mahakama
|
30,980,157,000
|
86,600,000,000
|
20,000,000,000
|
2,716,668,000
|
140,296,825,000
|
41
|
Wizara ya Katiba na Sheria
|
2,447,110,000
|
8,028,651,000
|
4,000,000,000
|
3,898,840,000
|
18,374,601,000
|
55
|
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
|
1,814,993,080
|
3,795,802,000
|
-
|
1,034,169,000
|
6,644,964,000
|
59
|
Tume ya Kurekebisha Sheria
|
575,560,000
|
2,856,000,000
|
-
|
616,350,000
|
4,047,910,000
|
JUMLA
|
|
42,537,099,080
|
152,890,448,000
|
24,000,000,000
|
11,259,786,000
|
230,687,333,000
|
MAHAKAMA YA TANZANIA
IDADI YA MASHAURI YALIYOFUNGULIWA,
YALIYOAMULIWA NA YALIYOBAKIA KATIKA MAHAKAMA MBALIMBALI ZA TANZANIA
JEDWALI
Na.1 : Mwenendo wa Mashauri – Mahakama ya Rufani
Mwaka
|
Masha-uri yaliyo-kuwepo
|
Masha-
uri yaliyofu-nguliwa
|
Jumla
ya Masha-uri
|
Masha-
uri yaliyosi-kilizwa
|
Mashauri yaliyo-baki
|
2008/09
|
1,798
|
824
|
2,622
|
552
|
2,070
|
2009/10
|
2,070
|
753
|
2,823
|
651
|
2,172
|
2010/11
|
2,172
|
615
|
2,787
|
637
|
2,059
|
2011/2012
|
2,059
|
727
|
2,786
|
1,043
|
1,743
|
2013/2014
|
1,743
|
450
|
2,193
|
275
|
1,918
|
JEDWALI
Na.2 : Mwenendo wa Mashauri – Mahakama ya Kuu
Mwaka
|
Mashauri yaliyoku-wepo
|
Mashauri yaliyofu-nguliwa
|
Jumla ya Mash-auri
|
Mashauri yaliyosi-kilizwa
|
Masha-uri yaliyo-baki
|
2008/09
|
11,531
|
7,594
|
19,125
|
7,419
|
11,706
|
2009/10
|
11,706
|
7,743
|
19,449
|
8,517
|
10,932
|
2010/11
|
10,932
|
9,453
|
20,385
|
9,669
|
10,718
|
2011/2012
|
10,718
|
4,217
|
14,935
|
5,198
|
9,737
|
2012/2013
|
9,737
|
7,547
|
17,284
|
5,191
|
12,093
|
Jedwali Na.3: Mwenendo wa Mashauri Mahakama Kuu
Divisheni Biashara
Mwaka
|
Mashauri yaliyo-kuwepo
|
Masha-uri yaliyofu-nguliwa
|
Jumla ya Masha-uri
|
Mashauri yaliyosi-kilizwa
|
Mashauri yaliyo-baki
|
2008/9/
|
105
|
12
|
117
|
109
|
8
|
2009/10
|
8
|
310
|
318
|
144
|
174
|
2010/11
|
174
|
268
|
442
|
174
|
268
|
2011/2012
|
268
|
189
|
457
|
172
|
285
|
2012/2013
|
285
|
118
|
403
|
74
|
329
|
Jedwali Na.4: Mwenendo wa Mashauri Mahakama Kuu
Divisheni ya Kazi
Mwaka
|
Mashauri yaliyo-kuwepo
|
Masha-uri yaliyofu-nguliwa
|
Jumla ya Masha-uri
|
Masha-uri yaliyosi-kilizwa
|
Masha-uri yaliyo-baki
|
2008/9/
|
572
|
903
|
1,475
|
412
|
1,063
|
2009/10
|
1,063
|
939
|
2,002
|
585
|
1,417
|
2010/11
|
1,417
|
1,403
|
2,400
|
893
|
1,507
|
2011/2012
|
1,507
|
986
|
2,493
|
896
|
1,597
|
2012/2013
|
1,597
|
674
|
2,271
|
491
|
1,780
|
Jedwali Na.5: Mwenendo wa Mashauri
Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi
Mwaka
|
Masha-uri yaliyo-kuwepo
|
Masha-uri yaliyo-fungu-liwa
|
Jumla ya Masha-uri
|
Masha-uri yaliyosi-kilizwa
|
Masha-uri yaliyo-baki
|
2008/9/
|
4,859
|
|
|
1,548
|
3,311
|
2009/10
|
3,311
|
1,939
|
5,250
|
1,109
|
4,141
|
2010/11
|
4,141
|
2,313
|
6,454
|
1,371
|
5,083
|
2011/2012
|
5,083
|
1,417
|
6,500
|
1,107
|
5,393
|
2012/2013
|
5,393
|
427
|
5,820
|
427
|
3,393
|
Jedwali NA.6 : Mwenendo wa Mashauri –
Mahakama za Hakimu Mkazi
Mwaka
|
Mashauri
yaliyokuwepo
|
Mashauri
yaliyofunguliwa
|
Jumla
ya Mashauri
|
Mashauri
yaliyosikilizwa
|
Mashauri
yaliyobaki
|
2008/09
|
16,698
|
19,001
|
35,699
|
14,361
|
21,338
|
2009/10
|
21,338
|
17,582
|
38,920
|
18,664
|
20,256
|
2010/11
|
20,256
|
28,096
|
48,352
|
19,760
|
28,592
|
2011/12
|
28,592
|
14,191
|
42,783
|
17,781
|
25,002
|
2012/13
|
25,002
|
980
|
25,982
|
612
|
25,370
|
Jedwali Na.7: Mwenendo wa Mashauri – Mahakama za
Wilaya
Mwaka
|
Mashauri
yaliyokuwepo
|
Mashauri
yaliyofunguliwa
|
Jumla
ya Mashauri
|
Mashauri
yaliyosikilizwa
|
Mashauri
yaliyobaki
|
2008/09
|
19,793
|
30,181
|
49,974
|
26,232
|
23,742
|
2009/10
|
23,742
|
31,370
|
55,112
|
28,050
|
27,062
|
2010/11
|
27,062
|
57,227
|
84,289
|
47,677
|
36,612
|
2011/12
|
36,612
|
77,495
|
114,107
|
83,082
|
31,025
|
2012/13
|
31,025
|
94,872
|
125,897
|
104,359
|
21,538
|
Jedwali Na.8 : Mwenendo wa Mashauri – Mahakama za
Mwanzo
Mwaka
|
Mashauri
yaliyokuwepo
|
Mashauri
yaliyofunguliwa
|
Jumla
ya Mashauri
|
Mashauri
yaliyosikilizwa
|
Mashauri
yaliyobaki
|
2008/09
|
50,764
|
128,183
|
178,947
|
132,956
|
45,991
|
2009/10
|
45,991
|
140,095
|
186,086
|
145,770
|
40,316
|
2010/11
|
40,316
|
303,032
|
343,340
|
219,693
|
123,647
|
2011/12
|
123,647
|
512,308
|
635,955
|
510,996
|
124,959
|
2012/13
|
124,959
|
650,181
|
775,140
|
577,425
|
197,715
|
Jedwali Na.9: Malalamiko-Tume Ya Haki
Za Binadamu na Utawala Bora
Mwaka
|
Idadi
ya Malalamiko
|
||||
Ya
Zamani
|
Mapya
|
Jumla
|
Yaliyohitimishwa
|
Yaliyobaki
|
|
2008/09
|
2,285
|
2,073
|
4,358
|
789
|
3,569
|
2009/10
|
941
|
481
|
1,422
|
941
|
481
|
2010/11
|
7,542
|
1,333
|
8,875
|
1,042
|
7,833
|
2011/12
|
7,833
|
886
|
8,719
|
1,554
|
7,165
|
2012/13
|
7,165
|
1,185
|
8,350
|
688
|
7,662
|
Jedwali Na.10: Usajili wa
Matukio-RITA
Mwaka/ Shughuli
|
Vizazi
|
Vifo
|
Ndoa
|
Talaka
|
Udhamini
|
Wosia
|
Mirathi
|
Kuasili
|
2008/09
|
938,775
|
105,482
|
15,345
|
73
|
247
|
-
|
-
|
39
|
2009/10
|
469,274
|
47,118
|
17,106
|
85
|
277
|
83
|
13
|
46
|
2010/11
|
625,670
|
73,810
|
23,108
|
69
|
203
|
36
|
14
|
33
|
2011/12
|
519,511
|
66,463
|
13,631
|
51
|
204
|
33
|
2
|
18
|
2012/13
|
331,272
|
59,099
|
6,094
|
42
|
151
|
37
|
1
|
23
|
Jedwali
Na. 11: Mwenendo wa Mashauri ya Madai kuanzia
Mahakama ya Rufani hadi Mahakama za Wilaya
Mahakama
|
Mashauri yaliyokuwepo Juni 2012
|
Mashauri yaliyofunguliwa
Julai hadi Machi, 2013
|
Jumla
|
Mashauri
yaliyohitimishwa
|
Mashauri yaliyobaki
|
Mahakama
ya Rufani
|
39
|
7
|
46
|
2
|
44
|
Mahakama
Kuu
|
550
|
132
|
682
|
40
|
642
|
Maombi ya
Madai
|
196
|
89
|
285
|
63
|
222
|
Jumla
|
785
|
228
|
1013
|
105
|
908
|
Jedwali Na.12: Mwenendo wa Mashauri
ya Jinai kuanzia Mahakama ya Rufani hadi Mahakama za Wilaya
Mahakama
|
Mashauri yaliyokuwepo Juni 2012
|
Mashauri yaliyofunguliwa Julai hadi
Machi, 2013
|
Jumla
|
Mashauri yaliyohitimishwa
|
Mashauri yaliyobaki
|
Mahakama
ya Rufani
|
26
|
161
|
187
|
122
|
65
|
Mahakama
Kuu
|
359
|
445
|
804
|
316
|
488
|
Mahakama
za chini
|
14,068
|
12,881
|
26,949
|
4,819
|
22,130
|
JUMLA
|
14,453
|
13,487
|
27,940
|
5,257
|
22,683
|
Jedwali Na. 13 MISWADA
Mwaka
|
Idadi ya Miswada
|
||
Iliyoandaliwa
|
Iliyopitishwa na Bunge na Kusainiwa
na Mhe. Rais
|
Inayofanyiwa Kazi
|
|
2008/2009
|
29
|
22
|
7
|
2009/2010
|
37
|
18
|
19
|
2010/2011
|
12
|
4
|
8
|
2011/2012
|
18
|
6
|
12
|
2012/2013
|
6
|
4
|
2
|
Jedwali Na. 14: Mwenendo
wa Mashauri ya Katiba na Haki za Binadamu
Mahakama
|
Mashauri yaliyokuwepo Juni 2012
|
Mashauri yaliyofunguliwa
Julai hadi Machi, 2013
|
Jumla
|
Mashauri
yaliyohitimishwa
|
Mashauri yaliyobaki
|
Mahakama
ya Rufani
|
5
|
4
|
9
|
0
|
9
|
Mahakama
Kuu
|
32
|
29
|
61
|
17
|
44
|
Mahakama
ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu
|
1
|
2
|
3
|
0
|
3
|
Jumla
|
38
|
35
|
73
|
17
|
56
|
Kiambatisho “B”
Orodha
Ya Sheria Zilizotafsiriwa Katika Lugha Ya Kiswahili
Tafsiri ya Sheria za Tawala za Mikoa:
Sura ya 97;
(i)
Tafsiri
ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 287; na
(ii)
Tafsiri
ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288;
(iii)
Tafsiri
rasmi ya Sheria ya Tozo za Mamlaka za Miji, Sura ya 289;
(iv)
Tafsiri
ya Sheria ya Fedha za Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Sura ya 290;
(v)
Tafsiri ya Sheria ya Serikali za Mitaa
(Upambaji wa Majengo) sura ya 293;
(vi)
Sheria
ya Mipango Miji, Sura ya 335
Kiambatisho “C”
Orodha Ya Sheria Zilizofanyiwa
Marekebisho
VAT Act,
cap148
(i)
The
Export Tax Act,
(ii)
The
Protection of New Plant Varieties (Plant Breeders Rights)
(iii)
Tanzania
Investment Act, Cap 38
(iv)
Gaming
Act, cap 41
(v)
Motor
Vehicle (Tax on Registration and Transfer) Act, Cap 124
(vi)
The
Excise (Management and Tariff) Act, cap 147
(vii)
The
Law Reform Commission Act, cap 171
(viii)
The
East African Development Bank Act cap 231
(ix)
Local
Government Finance Act, cap 290
(x)
The
Local Government (Elections) Act cap 292
(xi)
The
Public Service Act, cap. 298
(xii)
Income
Tax Act , cap 332
(xiii)
The
Airport Service Charge Act cap 365.
No comments:
Post a Comment