Habari za Punde

Mabingwa wa Ligi Daraya la Pili Wilaya ya Mjini Danger

Mjumbe wa ZFA Taifa Abdalla Juma kulia akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi DFaraja la Pili Wilaya ya Mjini Nahodha wa timu ya Danger Khalid Hamad, kwa kushika nafasi ya kwanza katika ligi hiyoimenyakuwa Kombe na Fedha taslim shilingi Laki Nane.
Mjumbe wa ZFA Wilaya ya Mjini Ameir Makungu akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Jangombe Boys Abrahaman Othman, kwa kuwa mshindi wa Pili wa Ligi hiyo.

Wachezaji wa timu ya Danger na wapenzi wa timu hiyowakishangilia Kombe lao la Ubingwa wa Ligi ya Wilaya ya Mjini baada ya kukabidhiwa katika mchezo wa mwisho na timu ya Kilimani Star, uliofanyika uwanja wa Mao.
Mgeni wa mchezo huo Mjumbe wa ZFA Taifa Abdalla Juma na Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Hassan Chura wa kisalimia wachezaji wa timu ya Danger.
Wachezaji wa timu ya Kilimani Star wakisalimiana na timu ya Danger kabla ya mchezo kuaza.
Kikosi cha Timu ya Danger  Mabingwa wa Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini kilicholitowa Kombe hilo kwa kuongoza ligi hiyo kwa  point.kililinyakuwa kombe hilo na kiktita cha zawadi ya Fedha Taslim Shilingi Laki Nne na Kombe.
Kikosi cha timu ya Kiliman Star, kilichoilazimisha Mabingwa wa ligi hiyo kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Tisa Bora Wilaya ya Mijini 
Mchezaji wa timu ya Danger Ramadhani Haji akimpita beki wa timu ya Kilimani Star ,Ahmed Sadalla, katika mchezo wa Ligi ya Wilaya ya Mjini 9 bora, uliofanyika katika uwanja wa Mao, timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.
Mchezaji wa timu ya Danger Hassan Mkwabi akijaribu kumpita beki wa timu ya Kilimani Star Yahya Mussa, katika mchezo wa Ligi ya Wilaya ya Mjini, Tisa Bora uliofanyika katika uwanja wa Mao.
Benchi la timu ya Kilimani wakifuatilia mchezo wao na timu ya Danger.

 

Beki wa timu ya Kilimani Rajab Makame kushoto na mchezaji wa timu ya Danger Hassan Mkwabi wakiwania mpira katika mchezo wa kuhitimisha Ligi ya Wilaya ya Mjini Daraja la Pili uliofanyika uwanja wa Mao, timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.
Kocha wa timu ya Kilimani Star akitowa mawaidha kwa wachezaji wake kuweza kushinda mchezo huo.wakati wa mapumziko.
Kocha wa timu ya Danger akitowa maelekezo kwa wachezaji wake kuweza kushinda mchezo huo, ambao ni muhimu kwao inatakiwa kushinda au kutowa sare ili kutangazwa mabingwa wa ligi hiyo ya Wilaya ya Mjini.  








Wapenzi wa timu ya Danger wakishangilia timu yao kwa ngoma ya mbwa kachoka (beni) wakiwa katika jukwaa la urusi katika uwanja wa mao timu yao imetoka sare ya bila kufungana na timu ya Kilimani Star.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.