WAKE wa Wawakilishi na Wabunge wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein ( hayupo pichani), akizungumza baada ya kukabidhi Vyakula kwa Wazee wa Nyumba za Welezo na Seblen, Nyumba za Sober House na za Watoto Yatima Mazizini na SOS, makabidhiano hayo yamefanyika Ikulu Migombani.
Viongozi wa Serekali na Nyumba za Wazee ,Watoto na wa Sober House wakimsikiliza Mama Mwanamwema Shein, akitowa maelezokatika hafla hiyo ya kukabidhi Vyakula kwa Taasisi hizo za Watu Maalum.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akizungumza katika hafla ya kukabidhi Vyakula kwa Nyumba za Wazee za Seblemni na Welezo na Nyumba za Sober House na Watoto Yatima, makabidhiano hayo yamefanyika Ikulu ya Migombani Zanzibar
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akizungumza katika hafla hiyo na kutowa maelezo ya mshikamano wa Umoja wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM, katika kusaidia Wanawake katika maendeleo na kutowa shukrani kwa misaada wanaopata na kutowa kwa walengwa.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Vyakula kwa ajili ya Sober House Mwanzilishi wa nyumba hizo Fatma Sukwa, Vyakula vilivyotolewa Mcheleb Unga wa Ngano, Sukari na Mafuta yackula. makabidhiano hayo yamefanyika Ikulu ya migombani Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake Vijana na Watoto Msham Abdalla , akitowa shukrani kwa Mke wa Rais wa Zanzibar , Mama Shein kwa msaada wake kwa Wazee wa Welezo, Sebleni na Watoto wa Mazizini na SOS na Sober House
Muazilishi wa Nyumba za Sober Haouse Zanzibar Bi. Fatma Sukwa, akitowa shukrani kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein , kwa msaada wake kwa Sober Haouse, mchango huo utatumika vizuri na umefika wakati muafaka kwa Vijana hao.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif,wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Nyumba zilizokabidhiwa msaada wa Vyakula na Wakev wa Viongozi, baada ya makabidhiano hayo yaliofanyika Ikulu Migombani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment