Habari za Punde

Mkutano wa hadhara wa CUF Kondoa

Pichani ni Viongozi wa chama cha wananchi(CUF)wakiwasili kwenye Mkutano wahadhara na kufunga ligi ndogo walioianzisha kwenye kijiji cha Lembo Kata ya Salanka wilayani Kondoa Aliye mbele ni Mkurugenzi wa kurugenzi ya vijana ya masuala ya habari Ashura Mustapha akiwa na mbunge wa viti maalumu kupitia chama hicho Moza Abdallah Said.(picha na mahmoud ahmad kondoa)
Mbunge wa viti maalumu kupitia mkoa wa Dodoma wilaya ya kondoa Moza Abdallah akiwa na mkurugenzi wa idara ya habari vijana wa chama cha wananchi (CUF)ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu la chama hicho Ashura Mustaph wakijadili jambo na mbunge kweny mkutano wa ndani wa chama hicho kabla ya mchezo wa soka wa fainali kati ya timu za Salanka kusini dhidi ya Lembo fc zote za kata ya salanka wilayani kondoa.(picha na mahmoud ahmad kondoa)
Pichani ni maandamano ya viongozi wa CUF wakielekea kwenye uwanjani kuhutubia na kushiriki fainali za mashindano ya CUF CUP yaliondaliwa na mbunge wa viti maalumu wilaya ya kondoa Moza Abdallah ambapo aliwataka wakazi wakata hiyo kukataa kuonewa na kuweka maslahi yao mbele kudai haki ya kuwa mji kwa wilaya hiyo ambayo ilianzishwa mnamo mwaka 1920(picha na mahmoud ahmad kondoa)
 
Mbele kwenye meza ni mgeni Rasmi Mjumbe wa baraza kuu taifa wa CUF Ashura Mustaph akiwa na mwenyeji wake mbunge wa viti maalumu Moza Abdallah na mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kondoa Isack Ibuva wakifuatilia mkutano wa hadhara ukiendelea huko kijiji cha Lembo kata ya Salanka wilayani kondoa(picha zote na mahmoud ahmad kondoa)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.