Mfugaji akiwa na shehena ya majani kwa ajili ya malisho ya mifugo yake, akikata mitaa katika maeneo ya Mwera.
Usafiri wa aina hii hutumika katika Vijiji na kurahisisha uchukuzi wa mizigo kutokana na kufika katika maeneo mengi katika mabonde ambapo gari za kawaida ni vigumu kufika.
Usafiri huu ulitumika enzi za mababu zetu na Vijana wanaendeleza usafiri huu wa asili katika visiwa vya Unguja na Pemba hutumika usafiri huu kusafirisha mazao kutoka mashambani hadi barabara kuu kwa usafiri wa kupelekwa marikiti kwa mauzo.
No comments:
Post a Comment