Habari za Punde

Huduma ya Afya kwa Watoto na Mama Mwera.

Huduma ya Afya ikiwa imeenea katika sehemu mbalimbali katika visiwa vya Unguja na kutowa huduma hiyo kwa wakazi wa Vijiji. Moja vituo hivyo ni hiki cha Mwera ambacho hutowa huduma za Mama na Mtoto na huduma nyegine hutolewa kwa wakazi wa maeneo hiyo, nikiwa katika mizunguko ya hapa na pale nilibahatika kufika katika Kituo hichi na kukuta Wakina mama wakipata huduma ya Cliniki kwa watoto wao waliofika katika kituo hicho cha mwera.
 
Mdau jengo hili linakupa kumbukumbu yoyote miaka ya nyuma?

2 comments:

  1. Bwana Othman kwa mara nyingine tena shukrani sana kwa kuweka hili jengo kwani limenikumbusha ule mchezo wa Dr Ayoub uliochezwa Zanzibar miaka ya 70 -80 na kama sikosei jumba hilo lilikuwa ni miongoni mwa sehemu ulimo tengenezwa na kwa hisa niyako kama upo uwezekano tuwekee japo kipande kidogo cha ile sinema ikiwezekana kwani wengi hawaelewi kuwa Zanzibar ilitowa michezo mingi katika miaka ya 70 kabla ya wezetu .asante

    ReplyDelete
  2. Jenlo hili linatunkumbusha ule mchezo uliojulikana kama "ukombozi wa Muafrika" ambao sehemu fulani ya mchezo huo ulifanyika hapo, jikumbushe kwa kutizama hii clip https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=SxIi7VpfNFU

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.