Habari za Punde

Vijana 96 Wajitokeza Kupima Afya zao Mwera Wilaya ya Kati Unguja.


 Afisa ya jumuiya hizo akimuorodhesha mmoja wa Kijana aliyejitokeza kupata ushauri nasaha 
 Ofisa wa ZAYEDESA akitowa Elimu ya Ushauri Nasaha kwa Vijana wa Koani jinsi ya kujikinga na maambukizo ya ukimwi na matumizi ya dawa za kulevya.
 
Vijana wengi wanaotumia dawa za kulevya hupata maambukizo ya ukimwi kutokana na matumizi ya vifaa hivyo zaidi ya mtu mmoja, Vijana 96 wamejitokeza kupima afya zao
 Mtoa huduma ya kuchunguza damu kama una maambukizo ya Ukimwi akimtoa mmoja wa Vijana waliofika katika Kituo hicho cha muda waliofungua katika banda la Karafuu Koani kwa ajili ya kutowa ushauri nasaha kwa Vijana wa Maeneo ya Koani na Mwera, vijana 96 wamejitokeza kupima afya zao.  
Mtoa Ushauri Nasaha wa Jumjuiya ya ZAYEDESA, akitowa ushauri nasaha kwa kijana aliefika katika kituo cha muda cha kuhusu maambukizo ya Ukimwi na Matumizi ya Dawa za Kulevya ambazo zimeathiri vijana wengi, Maofisa wa jumuiya hiyo walikuwa katika kutowa huduma hiyo katika wilaya na zaidi ya Vijana 96 Walijitokeza kupima afya zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.