Habari za Punde

Matokeo ya mitihani ya kidato cha Nne 2012 yafutwa, Mitihani kusahihishwa upya


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (kushoto), akiwa bungeni mjini Dodoma. Kulia ni Mbunge wa Sengerema,William Ngeleja.

HABARI zilizotoka bungeni mjini Dodoma  ni kwamba matokeo yote ya kidato cha nne 2012 yamefutwa na mitihani itasahihishwa upya haraka iwezekanavyo.

Taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato cha nne kwa mwaka jana imesomwa leo bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Waziri Lukuvi amesema sababu zilizosababisha wanafunzi hao kufeli ni pamoja na upungufu wa waalimu, mazingira magumu ya kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa na utaratibu mbovu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) uliotumika bila kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu.

Kutokana na sababu hizo, matokeo yote ya kidato cha nne 2012 yamefutwa na mitihani itasahihishwa upya.

2 comments:

  1. nyoooo , angalieni mmebambwa mara hiii eeenh na ujanja ujanja wenu huo wakupasishana mnaowataka na kuwafelisha wengine ..... bado joto ya jiwe inakuja

    ReplyDelete
  2. Mziki wa CHADEMA huo..unafkiri ni CUF walioshinikiza?..mtawataka mwaka huu!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.