Na Rajab Mkasaba, Ikulu
MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar inaendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM katika kuimarisha
sekta za maendeleo ikiwemo huduma ya maji safi na salama katika maeneo mbali
mbali Unguja na Pemba.
Dk. Shein aliyasema hayo leo kwa
nyakati tofauti katika ziara yake ya Kichama katika Wilaya ya Kusini Unguja.
Dk. Shein alisema kuwa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar imefanya juhudi kubwa za kutafuta fedha kwa njia ya mkopo
zzaid ya bilioni 64.4 kutoka Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika
(ADB) kwa ajili ya kuimarisha sekta ya maji pamoja na kiasi cha Tsh. Bilioni 36
kwa ajili ya miundombinu ya maji.
Jitihada zinafanywa katika
kuhakikisha tatizo la maji linamalizika katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar
likiwemo Jimbo la Makunduchi.
Katika ziara hiyo, Dk. Shein
aliweka jiwe la msingi mradi wa Chama wa maduka na kupata maelezo pamoja na
kukagua ujenzi wa ukumbi mpya wa mikutano uliopo katika eneo la afisi ya CCM
Wilaya ya Kusini Unguja.
Dk. Shein pia, aliweka jiwe la
msingi katika jengo la ushirka wa UWT, Daima Tupendane. Aidha, alifika Tawi la
CCM Mzuri kuangalia ukarabati wa afisi ya Tawi la CCM na kusalimiana na
wanachama wa CCM wa Wadi ya Mzuri na kutoa kadi za CCM kwa wanachama wapya 203.
Mara baada ya kuweka jiwe la
msingi katika jingo la ushirika wa UWT, Daima Tupendane, Dk Shein alipongeza
juhudi za ushirika huo na kuahidi kuwasaidia walipofikia katika ujenzi huo pamoja
na kuwapa mtaji wa kuanzisha bekari ya mikate. Dk. Shein alieleza juu ya suala
zima la ajira kwa vijana na jinsi serikali ilivyojipanga juu ya hilo.
Baada ya hapo Dk. Shein alikagua
ukarabati wa Tawi la CCM Bwejuuambapo alipokelewa kwa shangwe kubwa na kuwapa
kai wanachama wapya 186 wakiwemo vijana na baadae aliwasilimia.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Vuai Ali alisema kuwa ziara zake zimewaonesha njia wanaCCM katika
msimamo wa kuimarisha Muungano na vipi unatakiwa ulindwe na udumishwe sanjari
na Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964.
Akiwa katika majumuisho ya Mkoa
huo baada ya kumaliza ziara yake, Dk. Shein alisema kuwa uhai wa chama umo
katika vikao, na kusifu juhudi zilizofanywa na viongozi wa chama pamoja na
juhudi za utekelezaji wa Ilani na Sera za CCM na kuupongeza Mkoa huo kwa
kingiza wanachama wapya.
Pamoja na hayo, Dk. Shein
aliupongeza Mkoa huo wa Kusini kwa kuendelea kuenzi na kuitunza historia ya ASP
hadi kufikia CCM nakueleza kuwa ziara hiyo imefana sana.
Aidha, alieleza kuwa Mapinduzi
ya Januari 1964, ndio mkombozi wa nchi na lazima wafundishwe vijana jinsi
Zanzibar ilivyokombolewa na kwa nini Mapinduzi yametokea. Aidha, alieleza
umuhimu wa Muungano na mafanikio yake yaliopatikana na kusisitiza utadumishwa
daima.
Viongozi wa CCM ni lazima wajue
kuwa wanajukumu la kuwatumikia wanaCCM il kuweza kuimarisha chama.
Alizma Mkoa wa Kusini
kujitahidi kuimarisha chama na kuhakikisha afisi za Matawi zinakuwa na nyenzo
za kufanyia kazi huku akieleza jinsi alivyofurahishwa na mashirikiano yaliopo
kati ya Wabunge na Wawakilishi na kusisitiza kuzidisha mashirikiano hayo.
Alieleza kuwa anafarajika sana
kuwaona viongozi wa Majimbo wanakuwa kitu kimoja na kueleza matumaini yake
katika ziara hiyo kwani wameanza vizuri na CCM ina kasi kubwa.
Uongozi wa Mkoa huo aliwataka
kujiandaa katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 na kuhakikisha CCM,inashinda
uchaguzi huo.
Jamani hiinch kuitianja kama hivi ndio ilani ya CCM kama ndio hivyo 2015 haipo mbali atafute chukuwambia wazanzibar wenziwe?
ReplyDelete