Na
Mwantanga Ame, Dodoma
SERIKALI
ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetoa shilingi milioni 30 kuwafariji wananchi walioathirika na
shambulizi la bomu lililotokea katika kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi mjini
Arusha.
Akizungumza
na gazeti hili, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif, alisema
serikali imetoa hundi ya kiasi hicho cha
fedha kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ikiwa ni
mchango wa SMZ katika tukio hilo.
Alisema
serikali imeguswa kwa kiasi kikubwa na
tukio hilo na inaendelea kulaani tukio hilo la kinyama.
Alisema
serikali inaamini tukio hilo ni la kigaidi na itahakikisha inashirikian na
serikali ya Jamhuri ya Muungano kuwasaka wahusika wote ili kufikishwa katika
vyombo vya sheria.
Balozi
Seif, mwanzoni mwa wiki hii alifnya ziara ya kuwakagua majeruhi waliolazwa
katika hospitali ya Mount Meru mjini Arusha.
No comments:
Post a Comment