Habari za Punde

Ujumbe wa Mawaziri Husika wakagua Unga wa Ngano Mbovu Bandarini. Zanzibar.

Raya Hamad OMKR
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Fatma Abdulhabib Ferej pamoja na watendaji wakuu wa ofisi hio, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe Juma Duni Haji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais inayoshughulikia Mazingira Tanzania Bara Mhe Teresiya Havisa na Ujumbe wa NEMC leo walifika Bandarini Zanzibar kukaguwa Makontena yaliyohifadhiwa unga wa ngano ulioharibika .

Hatuwa hio inafuatia ombi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuomba mashirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ili kupata ufumbuzi na kutafuta njia muafaka ya kuweza kuuondosha na kuuharibu unga huo kwa njia za kiusalama bila ya kuleta athari .

Viongozi hao wamekubaliana kutekeleza na kulishughulikia suala hilo kwa pamoja na kuunda Kamati maalum itakayofatilia na kushughulikia namna ya kuuondosha Bandarini na hatimae kuuangamiza unga huo bila ya kuathiri afya za wananchi na kulinda mazingira yaliopo .

Makontena thalathini yenye wastani wa zaidi ya tani 700 za unga wa ngano ulioharibika unategemewa kuangamizwa baada kuonekana haufai kutumika kwa matumizi ya binaadamu .

1 comment:

  1. Ndio tujuwe wazi kuwa hatujiwezi kontina 30 zimekaa mwaka mzima bila ya kupatiwa ufumbuzi mpakaja waziri kutoka. Tanganyika ndio upatikane ufumbuzi, ndio tuna dai tuwache tupumue
    ?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.