Joseph Ngilisho,Arusha
WANAFUNZI katika skuli za msingi Nanganga na Nambala wilayani Arumeru Mashariki, wameishukuru serikali na shirika la World Reader kwa kuwapatia maktaba wa mkononi ya vitabu kwa njia ya elekroniki ijulikanayo kama E’Reader.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusiana na msaada huo,wanafunzi hao walisema wanashukuru mradi huo kuwafikia, kwani awali walikuwa wakibeba madaftari mengi pamoja na vitabu.
Akizungumzia mradi huo, mmoja wa mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Neema Mollel alisema,hivi sasa wamerahisishiwa kazi kutokana na kusoma vitabu kwa kutumia kifaa maalumu kama laptop ambacho kinahifadhi vitabu zaidi ya 100 vya masomo mbalimbali.
Alisema hatua ya chuo kikuu cha Nelson Mandela kwa kushirikiana na wadau wa World Reader ni kitendo muhimu na kinapswa kuigwa na wadau wengine kwani shule nyingi zinakabiliwa na changamoto kama hizo na zinahitaji msaada.
Mwenyekiti wa Baraza la chuo Kikuu cha Nelson Mandela, Professa David Mwakyusa alisema chuo hicho kitaendelea kuwatumia wataalamu wa teknolojia ya elimu ili kuboresha matatizo ya elimu na kupata wasomi wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment