Wananchi wa Mtoni wakiangalia gari ya mizigo iliopata ajali katika barabara hiyo ya bububu. Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo iliotokea katika eneo la mtoni daraja la kwanza dereva wa gari lenye namba za usajili Z494 CS, ikitokea bububu kuelekea mjini amewakwepa wapanda Vespa na Baskeli na kusababisha gari kukosa muelekeo na kutembea kwa maringi mawili na kusababisha kuanguka ubavu.
Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyefariki.
Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyefariki.
Bwana Othman
ReplyDeleteA.alaikum
Unakumbuka ile ajali ilio pita pale mtoni ? Nilisema mimi kwamba eneo letu la mtoni linaongoza kwa ajali kwa njia ya bububu,unajua njia ya bububu kwanza imekuwa ni ndogo kwa mahitaji yetu, gari ni nyingi sana, pia uwendeshaji hauna viwango,yaani madereva hawaheshimu sheria za barabara, pia hata uwendeshaji wao ni mbovu, kwenye kona mtu ana over take, madereva hawana uvumilivu,wao mbio mbio tu na haraka haraka.
Ipo haja ya kuangaliwa hii barabara na kutanuliwa tena upya ikidhi mahitaji ya wananchi.