Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Mke wa Makamo wa Rais wa China Mama Lu Yuanchao,wakiangalia samaki wa kufuga katika bwawa maalum nje ya ukumbi wa Nyumba maalum palikofanyika mazungumzo katika ya ujumbe wa Rais wa Zanzibar na
Makamo wa Rais wa China,ikiwa ni katika ziara ya kiserikali
jana, katika Mji wa Beijing.[Picha na Ramadhan Othman China.]
Makamo wa Rais wa China,ikiwa ni katika ziara ya kiserikali
jana, katika Mji wa Beijing.[Picha na Ramadhan Othman China.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kusainiwa kwa mkataba wa ushirikiano katika masuala ya bahari na uvuvi kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Watu wa China sio tu ni hatua muhimu ya kuimarisha sekta hiyo Zanzibar bali pia ni kielelezo cha urafiki wa kweli wa Serikali na wananchi wa nchi mbili hizo.
Dk. Shein amesema hayo jana mjini Beijing China wakati alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Taasisi ya Taifa inayoshughulikia Uvuvi ya China Bwana Liu Cigui katika siku ya pili ya ziara yake ya siku saba nchini humu.
Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika muda mfupi kabla ya kushuhudia kutiwa saini mkataba huo Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Saba inatilia mkazo uendelezaji wa sekta ya uvuvi kwa kuwa ni sekta muhimu katika kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo Zanzibar 2020.
Alibainisha kuwa ingawa Zanzibar ni kisiwa lakini hadi sasa haijaweza kuitumia vyema rasilimali hiyo ya bahari kuendeleza uchumi na ustawi wa wananchi wake hivyo hatua hizo za Serikali zimelenga kufanya mabadiliko makubwa katika sekta hiyo ili iweze kuchukua nafasi katika uchumi wa Zanzibar.
“Uvuvi ni sekta muhimu katika kutimiza malengo ya Dira yetu ya Maendeleo 2020 na ni sekta ambayo ikiendelezwa ipasavyo ina uwezo wa kutuwezesha kutimiza malengo yetu ya kuinua uchumi na kuondoa umasikini”alisema Dk. Shein.
Aliongeza kuwa kuanzishwa Wizara maalum inayoshughulikia Uvuvi, kupitisha Sera ya Uvuvi na Mapango Mkakati wa Sekta hiyo ni miongoni mwa hatua za kuthibitisha dhamira ya kweli ya serikali kuimarisha sekta ya uvuvi Zanzibar.
Hatua hizo alisisitiza kuwa zinachukuliwa kuhakikisha kuwa sekta ya uvuvi inaleta mabadiliko katika ustawi wa Zanzibar na wananchi wake kwa kuchangia ipasavyo katika kukuza uchumi, kupunguza umasikini na kuinua kiwango cha maisha cha wananchi wake.
Hata hivyo alieleza kuwa dhamira hiyo inahitaji kuungwa mkono na washirika wake wa maendeleo ikiwemo China na kusema kuwa “Ndio maana katika ziara yangu hii uvuvi ni moja ya maeneo ambayo nimeyapa kipaumbele katika maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Zanzibar na China”alisisitiza Dk. Shein na kubainisha utafiti, mafunzo, ufugaji samaki na uhaulishaji tekinolojia kuwa miongoni mwa maeneo muhimu katika ushirikiano huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi hiyo Bwana Liu Cigui alisema Serikali ya China iko tayari kuisaidia Zanzibar kuendeleza sekta ya Uvuvi lakini alishauri kuwepo mpango endelevu ili kuleta ufanisi wa ushirikiano huo kwa kuanzisha timu ya pamoja ya watalaamu itakayosimamia masuala hayo pamoja na kuanzisha kituo cha pamoja cha utafiti wa masuala ya bahari.
“Tukianzisha timu ya pamoja ya wataalamu na kituo cha utafiti wa mambo ya bahari sisi (China)tunaweza kutoa msaada unaotakiwa na hatimae kuchangia katika kuinua hali za maisha za watu wenu, kuongeza ajira na kutoa matokeo mazuri katika uchumi kwa jumla”alieleza bwana Liu.
Aliongeza kuwa Serikali ya China kuanzia mwaka jana imeanza kutoa fursa za mafunzo ya elimu ya juu katika masuala ya bahari hivyo vijana wa Zanzibar wanakaribishwa kuchukua mafunzo hayo.
“Serikali yetu imeanza kutoa nafasi za elimu ya juu katika masuala ya bahari hivyo vijana wa Zanzibar nao wanakaribishwa kuja kuchukua mafunzo hayo hapa kwetu”alisema Bwana Liu na kutoa mwaliko wa warsha ya masuala ya uvuvi itakayofanyika hivi karibuni kwa Waziri wa Uvuvi na wataalamu kutoka Serikali ya Zanzibar kushiriki.
Mkuu wa Taasisi hiyo alieleza kuwa miongoni mwa majukumu ya taasisi yake ni kufanya tafiti za kisayansi za bahari na rasilimali zake na kusimamia Sheria ya mazingira ya bahari na uvuvi.
Dk. Shein na ujumbe wake ameondoka mjini Beijing leo mchana kwenda Nanjing kuedenelea na ziara yake. Katika ziara hiyo amefuatana na mke wake mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yusuf Mzee, Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdillah Jihad Hassan.
Hapa rais wetu mpendwa kachemsha,serekali ya awmu ya7 inamiaka3 ndio kwanza anakumbuka sekta ya uvuvi baada kwenda huko china?.Mda wote wa miaka3 hajazungumza na wavuvi na wafugaji, imekuwa porojo nyingi kuliko vitendo,kama kweli rais wetu anataka kushirikiana na wachina, angeuliza muekezaji alopewa, shirika la uvuvi kapotelea wapi maboti tuliyopewa na nduguzetu .Wajerumani yamezama bila sababu yamsingi,muwekezaji tunasikia ,wizara ya fedha ishampa mamilioni ya shilngi na shirika kauwa
ReplyDeleteHii ni nchi ya kusadikika A.K.A nchi ya Uwamsho!
ReplyDelete