Habari za Punde

Ziara ya Mama Asha Balozi Mkoa wa Kaskazini Pemba na Ujumbe wake

MWANAKIKUNDI wa Vikundi vya Ushirika vya Wanawake Wilaya ya Chakechake, akisoma Qu-ran kabla ya kuaza kwa shughuli ya kutoka misaada kwa Vikundi hivyo katika ukumbi wa Makumbusho Chakechake.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akiwahutubia Wanaushirika wa Vikundi vya Wanawake Wilaya ya Chakechake, baada ya kukabidhi misaada iliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, Mama Asha Balozi na Wake wa Wawakilishi na Wabunge kwa ajili ya kuegeze mtaji wa Ushirika wao.
Mwanachama wa Vikundi vya Wanawake vya Chakechake akisomarisala kwa niaba ya vikundi vyote vya Wanawake vya  Wilaya ya Chakechake Pemba katika  ghafla ya kukabidhi misaada kwa vikundi hivyo  katika ukumbi wa makumbusho chakechake
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif. Kulia akimkabidhi Kiongozi wa kimoja  ya Vikundi cha Ushirika shilingi Laki Nne kwa ajili ya kikundi chake, jumla ya Vikundi vya Ushirika vya Wanawake Vitano  katika Wilaya ya Chake chake vimekabidhiwa shilingi laki nne kila kimoja kwa ajili ya maendeleo ya Vikundi vyao.
WANAUSHIRIKA wa Vikundi  vya  Wanawake Wilaya ya Chake Chake Pemba wakimsikiliza Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akiwahutubia katika sherehe za kukabidhi mchango uliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, Mama Asha Balozi na Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Makumbusho Chakechake  
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitembelea  maonesho ya Vikundi vya Ushirika vya Wanawake wa Wilaya ya Chake, baada ya kuwakabidhi misaada kwa ajili ya vikundi vyao.katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Chakechake
WAKE wa Wawakilishi na Wabunge wakitembelea maonesho ya bidhaa za Wanaushirika Wanawake wa Wilaya ya Chake katika ukumbi wa makumbusho, wakati wa kutowa misaada kwa vikundi vya Wanawake Pemba
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitembelea maonesho ya bidhaa za Wanawake wa Mkoa wa Kaskanizi Pemba, wakati wa ziara ya kutembelea Vikundi vya Wanawake akiwa na Ujumbe wa Wake. wa Wawakilishi na Wabunge
WAKE wa Wawakilishi na Wabunge, wakishangilia wakati Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akiwasili katika ukumbi wa skuli ya Micheweni kwa ajili ya kutowa misaada kwa vikundi vya Ushirika vya Mkoa wa Kaskazini Pemba.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akihutuba katika mkutano wa kuwazawadia misaada Wanawake wa Vikundi vya Ushirika vya Mkoa wa Kaskazini Pemba
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Asha Thani, akizungumza katika mkutano huo wakati wa ziara ya Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, katika ukumbi wa skuli ya micheweni
WANAUSHIRIKA wa Vikundi vya Wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimsikiliza Mke wa Makamu wa Pili wa Rais  Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akihutubia katika ukumbi wa skuli ya Micheweni Pemba baada ya kutowa misaada kwa Vikundi hivyo.
WANAUSHIRIKA wa Vikundi vya Wanawake Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimshangilia Mama Asha Balozi Seif, akihutubia katika mkutano wa kutowa misaada kwa Ushirika wa Vikundi hivyo katika ukumbi wa skuli ya Micheweni Pemba. 

WANACHAMA vikundi vya Ushirika vya Wanawake wakishangilia kwa aina yake kutokana na kupata msaada wa kujiendeleza katika miradi yao ya Ushirika kwa kuegezewa mtaji wakiwa na bidhaa wanazozalisha katika vikundi vyao.
WANAUSHIRIKA wa Vikundi vya Wanawake Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimshangilia Mama Asha Balozi Seif, akihutubia katika mkutano wa kutowa misaada kwa Ushirika wa Vikundi hivyo katika ukumbi wa skuli ya Micheweni Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.