Habari za Punde

Ajali ya kuanguka kwa ukuta wa tangi la maji iliyouwa watu watatu leo Machomane , Pemba

 ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama kisiwani Pemba, wakiwa katika zoezi la kuokoa miili ya Marehemu waliopoteza maisha katika ajali ya kuangukiwa na Ukuta wa tangi la Maji Machomanne Chake Chake Pemba leo
 Askari wa JWTZ, kwa kushirikiana na Askari wa vikosi vya SMZ, wakiingiza miili ya marehemu iliyoangukiwa na ukuta wa tangi la Maji Machomanne, katika gari ya kubebea wagonja Ambalesi kwa kuipeleka katika hospitali ya Chake Chake
 ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama kisiwani Pemba, wakiutoa mwili wa Marehemu juu ya Mnara wa tangi la Maji Machomanne, ulioangukiwa na ukuta wa tangi hoo


 WANANCHI mbali mbali wakiuangalia mnara wa Tangi la Maji Machomanne, ulioanguka na kupoteza maisha ya wananchi watatu leo asubuhi. (picha na Abdi Suleiman

 ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama kisiwani Pemba, wakiushusha chini mwili wa marehemu aliyepoteza maisha baada ya kuangukiwa na ukuta wa mnara wa Tangi la Maja Machomanne Pemba


 ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama kisiwani Pemba, wakiupeleka mwili wa marehemu katika gari ya kubebea wagonja, ulioelemewa na ukuta wa mnara wa Tangi la Maji Machomanne Pemba
 WANANCHI mbali mbali wakiwa katika hospitali ya chake chake , wakitizama miili ya ndugu zao waliopoteza maisha baada ya kuangukiwa na mnara wa tangi la maji Machomanne Pemba
 Mkuu wa mkao wa kusini Pemba, Juma Kassim Tindwa, akimfahamisha jambo waziri wa Nnchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, walipofika katika Hospitali ya Chake Chake, kuaangalia majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo.
DAKTARI bingwa kutoka Quba anayefanya kazi zake kisiwani Pemba, (jina halikufahamika) akimtibu mmoja kati ya majeruhi waliolazwa katika hospitali ya chake chake, kufuatia kuwangukiwa na ukuta wa mnara wa tangi la Maji Mchomanne Pemba.

(Picha zote  na Abdi Suleiman, Pemba).

1 comment:

  1. hivi maalim mapara ndio tunavyotaka ukiweka picha utupe na maelezo japo kwa ufupi ili na sisi tulioko mbali tuweze angalau kupata idea kuhusu kile ambacho kimetokea na sio kutuwekea picha tupu nakupongeza kwa hili asante sana. Na pia ukiona tunakosoa sio kama hatuthamini mchango wako ila huwa tunapenda kuona na kuelewa nini lengo la blog yako kwani tunaamini lengo lako ni kuhabarisha wale walioko mbali na hapo nyumbani.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.