Habari za Punde

Auawa, kichwa chatenganishwa na kiwiliwili

Na Bakar Mussa,Pemba
KIJANA mmoja mwenye umri wa miaka 20 alietambuliwa kwa jina la Amour Omar Ali, mkazi wa Finya Mkoa wa Kaskzini Pemba, ameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingoni kisha kichwa kutenganishwa na kiwiliwili.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mohammed Shehani Mohammed alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12:30 na saa moja asubuhi katika eneo la Kivuli, Finya.

Alisema kijana huyo alivamiwa na kundi la watu wakati akifanya kazi zake za kufukua mkaa na kumpiga mapanga kisha kumtenganisha kichwa na kiwili wili.

Alisema sababu za mauaji hayo bado hazijajulikana na polisi wanaendelea kufanya msako wa kuwatafuta.
Polisi imewaomba wananchi kutoa taarifa iwapo wana taarifa za watu waliohusika na mauaji hayo.



1 comment:

  1. Hii, inathibitisha kua ubaya hauna kwao..unawaona hao "BANCHICHA" a.k.a "UWAMSHO" wanavyouwana kinyama..halafu wasingizie ni matatizo ya muungano!

    Ukatili gani huu?...halafu wanajifanya wanajua dini saaana...wenzao wote makafiri!

    Yaani mwenzao anatafuta riski kwa kujipigia mkaa wameenda kumdhulumu, sijui tena, WAZUSHI watakuja na sababu gani katika hili...itakayohalalisha ukatili wa namna hii!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.