Ndugu Wanachama,
Tunapenda kuwajuilisha wanachama wote wa ZIRPP kwamba Tume ya Madiliko ya Katiba imekubali ombi la ZIRPP la kutaka kuunda Baraza lake la Katiba kwa madhumuni ya kuipitia Rasimu ya Katiba mpya na kutoa maoni yake kama Taasisi.
Kwa hivyo, ZIRPP imeandaa mkutano wa wanachama wake kwa madhumuni hayo siku ya Jumapili tarehe 30 Juni 2013, kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 9 jioni. Mkutano huu ni kwa ajili ya wanachama tu.
Kwa wale wanachama ambao bado hawajapata Rasimu ya Katiba wanaombwa wafike ofisini ZIRPP siku za kazi, kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 9:30 jioni, kwa kupatiwa nakala ya Rasimu ili waweze kujiandaa vyema kwa kutoa michango yao mizuri itayosaidia katika jitihada zetu za pamoja za kupata katiba bora. Pia, tutashukuru sana iwapo wanachama wanaokusudia kuhudhuria katika mkutano huu wakathibitisha ushiriki wao kwa maandishi.
Chakula cha mchana, chai, kahawa na vinywaji baridi vitatolewa kwa washiriki wote.
Shime wanachama wote tuhudhurie kwa wingi katika mkutano huu muhimu katika historia ya taifa letu.
Jumbe Said Ibrahim
K.n.y. MKURUGENZI MTENDAJI
ZIRPP
Wwaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa
Awasiuli Osaka Japan
-
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiwa katika picha ya
pamoja na viongozi walioambatana nae katika safari ya Japan ambako
atamwakili...
41 minutes ago
nyinyi zirpp hamna lolote la kusema zaidi ya kukubaliana na mambo ya kuendeleza muungano , msipoteze bure muda ikiwa hii ndio agenda, waznz hawawakilishwi na nyinyi watu wachache wenye uchu wa madaraka na maslahi binafsi na kusahau haki za waznz walio wengi
ReplyDelete@Anonymous wa kwanza.
ReplyDeleteInaonekana hulijui ulisemalo, kwa taaerifa yako ZIRPP ni kama ilivyo UWAMSHO (tawi la propaganda) la CUF.
lengo lao ni kuhakikisha MUUNGANO unakufa na kumrudisha SULTANI kwa kisingizio cha kua 'watu wake wamemtaka arudi.
Kwa maelezo zaidi soma MZALENDO.NET
Wee waache tu, wauvunje watakuja kutueleza vizuri...si wanamuona MORSI kule Egypt?
ReplyDeleteHawa watu wa ajabu kabisa eti juzi A.G. anasema W'bari wasitishwe kua ukivunjika muungano watafukuzwa Bara...mbona hiyo iko wazi!
Bila muungano means kuna TANGANYIKA na Z'BAR sasa utaipangiaje nchi huru kukubali raia wa nchi nyengine..hiyo hutegemea tu nia njema.
Ningemuona Mh. Othman Masoud kuwa ni mtu mwenye kuona mbali kama angewashauri wanasiasa kuanza kuwaelimisha W'bari wanaoishi bara yale yanayoweza kujitokeza pindipo muungano ukivunjika.
Na kwa kufanya hivyo ingewasaidia wahusika kufanya maamuzi sahihi kuhusu hatima yao na sio kuwapotosha.
Suala la ardhi ni nyeti mno, kiasi kwamba hakuna nchi inayoweza kuruhusu mgeni kumiliki na Mh. akumbuke ardhi ni pamoja na nyumba ambazo W'bari wanamiliki.
Tena anajikaza eti mbona WAGANDA, WAKENYA, WASOMALI na wengine wanaishi Bara kwani wameungana?..hivi yeye anajua vikwazo vya kisheria vinavyowakabili hao watu ?
Niambie W'bari wanaoishi kwa kuvua, kuchuuza samaki, kulima (morogoro) kuendesha biashara za daladala na nyingi za kawaida wakiwa wageni..wataruhusiwa..na watakua na uwezo wa kulipia 'work permits?'
Hii ni jamii iliyozowea kuishi kwa majuto...lkn. Mungu atuweke.. letu jicho!
Nakubliana na changiaji3 hawa ni watu waajabu na wanaajenda yao ya siri ukiachia hu muungano, na huyo wanayetaka kumlata wasahau, wengi hao wanojiita,Zirpp, ni Cuf, sasa wameona wameshinda hawana cha kuwaeleza. Wazanzibar wanapita mlango wanyuma, huyu anojidai zirpp kama umuamsho, tunashukuru kasema kweli muamsho walikuwa hawaitakii mema, ndio mungu kawazibu haphapa duniani na dua zao zime wazuru wenye
ReplyDelete