Habari za Punde

PBZ Yadhamini Michuano ya Kombe la Vyuo Vikuu Zanzibar.

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Vyuo Vikuu Zanzibar Nahodha wa timu ya Chuo cha Afya Mbweni Hashim Othman.baada timu yake kunyakua Ubingwa huo kwa  kuifunga timu ya Chuo Kikuu cha Mbweni kwa mabao 4--3.
Viongozi wakifuatilia mchezo wa Fainal kati ya Chuo Kikuu cha Tunguu na Chuo cha Afya Mbweni.
 Wachezaji wa timu ya Chuo cha Afya Mbweni wakishangilia Ushindi wao dhidi ya Chuo Kikuu cha Tunguu.
 Hivi ndivyo ilivyokuwa katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Vyuo Vikuu Zanzibar katika uwanja wa Amaan. Wanavyuo wakishangilia kwa upinzani mkubwa uwanjani hapo.
Wanavyuo Vikuu Zanzibar wakishangilia timu ya Chuo cha Afya Mbweni kwa kuwa Bingwa na Michuano hiyo iliodhaminiwa na Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ,fainali za mchezo huo zimefanyika katika uwanja wa Amaan, iliozikutanisha timu za Chuo cha Afya Mbweni na Chuo Kikuu cha Tunguu, mchezo huo umeamuliwa kwa matuta baada timu hizo kutoka sare.
                                                       Timu ya Afya imeshinda kwa 4-3.

1 comment:

  1. Haya ndio mambo tunayotaka kuyaona kutoka ktk makampuni yetu, PBZ wameonesha mfano naomba na ZANTEL waige mfano wao.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.