Habari za Punde

MRITHI WA BRIGITT ALFRED, PRISCA ELEMENT AAHIDI KUMRITHI HADI REDD'S MISS TANZANIA 2013



 Miss Sinza 2012-2013, Brigitte Alfred (kushoto) akimvisha Taji Redd's Miss Sinza 2013, Prisca Element, baada ya kutangazwa mshindi wa taji hilo katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Meeda Club, Sinza jijini Dar es Salaam. 

 Redd's Miss Sinza 2013, Prisca Element (katikati) akiwa na Mshindi wa pili Happynes Maira (kulia) na Mshindi wa tatu, Sarahy Paul, wakiwa na furaha mara baada ya kutangazwa washindi katika shindano lao lililokuwa likishikiliwa na Redd's Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigitte Alfred. 

 Warembo wa Redd's Miss Sinza, wakicheza shoo ya ufunguzi wa shindano lao.


Prisca Element usiku wa kuamkia leo alitwaa taji la mrembo wa Redds Miss Sinza 2013 katika kinyang'anyiro kilichowashirikishwa jumla ya warembo 12, kwenye ukumbi wa Meeda Club na kurithi taji la kwanza la Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred.

Haikuwa kazi rahisi kwa Prisca kutwaa taji hilo kutokana na ushindani mkubwa kutoka kwa warembo bora 11 walioshiriki mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, Fredito Entertainment, Chilly Willy Energy Drink, Sufiani Mafoto blog, Salut5 na CXC Africa.

Hata hivyo, Prisca aliweza kuwazidi kete wanzake na kutwaa taji hilo sambamba na zawadi ya Kitita cha Sh. 400,000 zilizotolewa na waandaaji wa mashindano hayo  Calapy Entertainment chini ya ukurugenzi wa Majuto Omary. 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sinza A, Juma Mgendwa alikabidhi zawadi hiyo kwa Prisca ambaye alisema kuwa amefurahi kushinda taji hilo na kazi yake kubwa ni kutwaa taji la Miss Kinondoni.

"Kwangu ni historia kutokana na ukweli kuwa nimerithi taji la Redds Miss Tanzania Brigitte Alfred, na ninaahidi kufanya kweli katika mashindano yanayofuata na kutwaa mataji ya Miss Kinondoni na vile vile taji la Redds Miss Tanzania, nitashirikiana na waandaji wangu ili kufanya maandalizi ya kina ili kufikia malengo hayo," alisema Prisca.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Happiness Maira ambaye alizawadiwa sh. 300,000 alizokabidhiwa na Mratibu wa Masoko na Biashara wa kinywaji cha Dodoma Wine, Frank Matonda na zawadi ya mshindi wa tatu ilikwenda kwa Sarahy Paul na kukabidhiwa zawadi ya shs 200,000 na Swabir Abdulrehman ambaye ni Mkurugenzi wa Usambazi wa Kampuni ya TSN Distribution kupitia kinywaji cha Chilly Willy.

Nafasi ya nne ilichukuliwa na Nicole Michael na tano ilichukuliwa na Nasra Hassan ambao wote walizawadiwa shs 150,000 kila mmoja na  Mkurugenzi wa Mashindano hayo, Majuto. Warembo hao watano wataiwakilisha Sinza katika mashindano ya Miss Kinondoni 2013.

Mashindano hayo yalishuhudiwa na umati mkubwa wa mashabiki wa urembo na kupambwa na burudani safi ya bendi bora nchini, African Stars maarufu kwa jina la Twanga Pepeta ambayo ilitambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya za albamu ya Nyumbani ni Nyumbani.Twanga Pepeta ilifanya mambo makubwa jukwaani huku ikiwa ikitumbuiza kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha mwaka mmoja na zaidi.


 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) akiwa na Albert Makoye (kushoto) na Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfred, wakishuhudia shindano hilo.

Shoo ya utangulizi ikiendelea...

Warembo wakisebeneka na shoo ya ufunguzi.


 Shoo ya ufunguzi, warembo wakiendelea kuwabamba mashabiki wao....



 Mshiriki, Catrina Laurence, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.



  Mshiriki, Nasra Hasan, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.



  Mshiriki, Maua Abdul, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.



  Mshiriki, Doris Mwaipopo, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.



  Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza 2013, Prisca Element, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.



  Mshiriki, Jaqueline Robert, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.



  Mshiriki, ambaye ni mshindi wa pili, Happynes Maira, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.


  Mshiriki, ambaye ni mshindi wa tatu, Sarahy Paul, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.


  Mshiriki, Martha Joseph, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.



  Mshiriki, Nicole Michael, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.


 Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza 2013, Prisca Element na Doris Mwaipopo wakipita jukwaani na vazi la Ufukweni.


 Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza namba 2 Happynes Maira (kulia) na wenzake wakipita jukwaani na vazi la ubunifu.


 Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza 2013, Prisca Element, (kulia) na Jaqueline Robert wakipita jukwaani na vazi la usiku.



 Washiriki, wakipita jukwaani na vazi la usiku.


 Warembo wote waliochuana wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutanzwa warembo watano bora.


 Warembo watano Bora, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi, kutoka (kushoto) ni Sarahy Paul, Nasra Hassan, Nicole Michael, Prisca Element na Happynes Maira.


 Mratibu wa shindano hilo Majuto Omary wa pili (kulia) akiwa meza kuu na Mkurugenzi wa Kamatio ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga na wengineo.


 Kalala Junior, akiwaongoza wanenguaji wa Twanga, kushambulia jukwaa wakati wa shindano hilo.


 Warembo watatu wa Miss Ubungo, wakipita jukwaani wakati wakitambulishwa ukumbini hapo, warembo hawa ndiyo wataungana na warembo wa Miss Sinza kuwania Taji la Miss Kinondoni.


 Mkurugenzi wa Usambazi wa Kampuni ya TSN Distribution, Swabir Abdulrehman (katikati) akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu, Sarahy Paul. Kulia ni Meshack Nzowa Ofisa uhusiano wa kinywaji cha Chilly Willy.


 Mratibu wa Masoko na Biashara wa kinywaji cha Dodoma Wine, Frank Matonda, akimkabidhi zawadi mshindi wa pili, Happynes Maira.


Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Sinza A, Juma Mgendwa, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza, Redd's Miss sinza 2013, Prisca Element.

5 comments:

  1. ASLKM, HII NDIO MARA YANGU YA MWANZO KUTOA COMMET,
    NASIKITIKA SANA KWA MTANDAO MKUBWA KAMA HUU KUOA HABARI KAMA HII TENA KWA WINGI WA MAPICHA YA HABARI MOJA TU HII KWASABABU HAIHUSU ZANIZBAR HALAMU MAMBO KIPUUZI, HAMNA HABARI AU? HE TUMACH TENA.

    ReplyDelete
  2. Wow,wow wow!
    Kaka tunashkuru kwa picha za warembo lakini tunaskitika zimekua nyingi sana.

    Ukweli ni kwamba huu ni mtandao wa kijamii na haya mambo yapo ktk jamii yetu kazma tuyajue.

    Hata hao wanaochukia na kukemea kama wasingeyaona wangepataje kukemea?

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa haya mambo ya Tanganyika ya kutangaza pombe ungemuachia Michuzi. au ndio unabangaiza na kuganga njaa kwa kutafuta udhamini? Kwa kweli hili litakuharabia kwa kukuondolea principles za blog yako. Mambo ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe.Usijidhalilishe kwa kutafuta udhamini au umaarufu.

    ReplyDelete
  4. Mimi nasema hawa akina "Banchicha" sijui tuwaeleweje?

    Wanajidai kua watu wa dini lakini, huku wanachukia watu wengine, sielewi Dini ya namna hii wanajifunzia wapi?

    Namna walivyo wavivu wa ufikiri, kila kitu kibaya wanakihusisha na Tanganyika lkn. wanasahau kua Bwana wao Sayyid Jamshid alikua mlevi wa kutupwa! na Z'bar ilikua hata haijaungana na Tanganyika!

    ReplyDelete
  5. shehe mche mungu hao kinabanchicha wameongea points wewe unaleta ushabiki mche mungu.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.