Habari za Punde

Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo chekundu yakabiliwa na matatizo mengi

Na Husna Mohammed
HOSPITALI ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu ,inakabiliwa na upungufu mkubwa wa huduma mbalimbali jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyakazi na wagonjwa .

Akizungumza na gazeti hili,Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo, Omar Hussein, alisema dawa zimekuwa zikikosekana mara kwa mara na hivyo baadhi ya wagonjwa hushindwa kupata tiba kwa wakati muwafaka.

Alisema matatizo ya ugonjwa wa akili yanahitaji kutumia dawa kwa wakati lakini kukosekana kwa dawa hizo kwa wakati kunawawezesha wagonjwa kutopata tiba.

Alisema ya vitanda ukilinganisha na wagonjwa waliopo kwa sasa havitoshelezi na hivyo kuwafanya baadhi ya wagonjwa kulala chini hasa wodi ya wanaume.

“Wodi nambari mbili ya wanaume vitanda na magodoro havifai kabisa ni vibovu na wodi ya wanawake ni kidogo lakini wodi ya wanaume imezidi hivyo ni ipo haja ya kuangaliwa upya kwa sababu wagonjwa wa akili ni wagonjwa kama wagonjwa wengine,” alisema.

Aidha alisema madaktari, wauguzi, wataalamu wa saikolojia, wataalamu wa kazi za mikono kwa wagonjwa, wahudumu, wapishi, walinzi ni mambo ambayo yanaonesha upungufu mkubwa katika hospitali hiyo.

Hata hivyo, alisema ingawa huduma ya chakula kwa wagonjwa kwa sasa imerudi lakini bado haitoshelezi kama siku za nyuma ilivyokuwa.

Alisema hadi jana hospitali hiyo ilikuwa imelaza wagonjwa 40 wanaume na wanawake 26.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.