Baadhi ya watumiaji wa barabara katika manispa ya Zanzibar hupuuza alama za kuongozea na kutowa maelezo katika maeneo ya barabara, kama inavyoonesha alama hii ikisomeka usisimamishe gari hapa na mwenye gari hii kupuuza alama hiyo iliowekwa katika maeneo ya jirani na soko la mwanakwerekwe na kuegesha sehemu hiyo, bila ya kujali madhara yake.
Alama hiyoimewekwa kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo huwa na msongamano mkubwa kwa wananchi wanaofika katika Soko hilo kufuata mahitaji ya Vyakula na mahitaji mengine.
Alama za marabarani zimewekwa kama pambo tu la kupendezesha mji ndio maana madereva wazembe huegesha wanapotaka na kuvunja sharia nyingi tu za marabarani, yote hii inatokana na kutowajibika kwa hao waloweka hizo sheria. Zanzibar tunapenda kubebana ndio maana hatuthamini hata usalama wetu.
ReplyDeleteTotally agree with you mkuu
DeleteMji wa Zanzibar ni vyema ukapangwa kwa kufikiria wapita kwa miguu na waendesha baiskeli na hizo gari. Mji huu mdogo nilitegemea utakuwa na maeneo ya kuegeshea rasmi baiskeli kama miji ya wenzetu. Mji wa zanzibar unatakiwa mwendesha baiskeli atoke fuoni, mathalan hadi Darajani akipita nijia ambayo ni kwa ajili ya baiskeli tu. wajapani walijenga mfano wa njia kama hii Bububu. Ilikuwa jukumu la mji wetu kuhakikisha njia hii haitumiwi na wauza samaki au kwa jambo jengine lolote zaidi ya baiskeli. Pale mwendesha baiskeli akikutwa anatumia njia nyengine ya gari basi akamatwe. Mji wetu upangwe kwa kujali baikeli. Haya ndio maendeleo na sio gari ambazo nchi nyingi sasa ziinafanyiwa utaratibu kupunguzwa. Zanzibar ni mji wa baskeli na tuki fanya hi vyo watu wetu watakuwa na afya na pi a tutapunguza kupeleka hewa chafu hewani Co2.
ReplyDeleteViongozi WA znz daily wanakuja ulaya wanaiyona mifano hai huku hakuna masihara kabisa kuhusu vibango walivyoviweka no parking huwezi gari hata siku moja ukiweka Tu dakika mbili Tu askari keshafika wanakupiga faini
ReplyDelete