Habari za Punde

Kuwasili kwaBoti ya Kilimanjaro 4 Zanzibar.

 Boti Mpya ya Kampuni ya Azam Marine ya Kilimanjaro ikiwa katika Meli ya Kampuni ya RichardsonDevine Marineya Tasmania Australia, ikiwa na boti hiyo ikisubiri kuishuka katika bahari ya Zanzibar baada ya kusafiri kwa masafa marefu hadi hapa ndani ya Zenj.
Boti ya Kilimanjaro 4 ikishushwa katika Meli maalum ilioichukuwa boti hiyo kutoka Australia.ilipowasili katika bandari ya Zanzibar.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Usafiri ya Azam Marine,Husseim Mohammed Said, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya S.SB, Said Bakresa wakati wakisubiri kupokea kwa Boti ya Kilimanjaro 4. akiwa na Maofisa wa Kampuni hiyo katika bandari ya Zanzibar mchana huu.  
 Boti Mpya ya Kilimanjaro 4 ikiwa katika bandari ya forodhani baada ya kushusha katika meli ilioileta Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya SSB Said Salim Bakresa, akiwa na Maofisa wa Kampuni hiyo wakiwa katika bandari ya Zanzibar wakiangalia ushushwaji wa Boti hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya SSB Said Bakresa, akimfahamisha Mdogo wake jinsi ya uungwaji wa Boti hiyo wakati ilipowasili katika bandari ya Zanzibar.
Sehemu ya Daraja la Kwanza katika Boti mpya ya Kilimanjaro 4.ikionekana katika picha baada ya kufunga gati katika bandari ya malindi leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya SSB yanayomiliki Kampuni ya Usafiri wa Baharini Azam Marine Said Bakresa (katikati) akimsikiliza Mtegenezaji wa Boti hiyo kutoka kampuni ya Richardson Devine Marine Ron Devine, akitowa maelezo ya boti hiyo akiwa katika sehemu ya Deki ya VIP, wakati wa boti hiyo ikiwa katika majaribio kutoka bandari ya Malindi hadi katika mnara wa pungume.ikiwa katika majaribio hayo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Usafiri ya Azam Marine Hussein Mohammed Said , akifafanua jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SSB inayomiliki Boti hiyo Said Bakresa. wakiwa katika boti hiyo ikiwa katika safari yake ya majaribio baada ya kuwasili Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya SSB Said Bakresa, akiwa katika chumba cha Nahodha akishuhudia uongozaji wa boti hiyo wakati ikiwa katika majaribio yake baada ya kuwasili Zanzibar.



Waandishi wa habari wakiwa katika Boti ya Kilimanjaro 4, ikiwa katika majaribio yake.

Meneja Mkuu wa Azam Marine Hussein Mohammed Said, akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika boti hiyo wakati wa majaribio yaliofanyika leo baada ya kuwasili, boti hiyo ina uwezo wa kuchukua abiria 700 kwa wakati mmoja na mwendo wa dakika 70 hadi Dar.


 Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zaanzibar wakishuka katika boti ya Kilimanjaro 4 baada kurudi katika majaribio ya boti hiyo yaliofanyika baada ya kushushwa leoZenj....
 Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Azam Marine Said Bakresa, akiwa na Ofisa wa Kampuni yake Abrazak wakati wa majaribio ya Boti hiyo ilipowasili katika bandari ya Zanzibar. 
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine Hussein Mohammed Said, akizungumza na mwandishi wa habari Abdalla Majura, kuhusiana na ujio wa boti ya Kilimanjaro 4,    
Wananchi wa Visiwani Zanzibar wakiangali ushushwaji wa Boti Mpya ya Kampuni ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.