Habari za Punde

Wafanyabiashara sokoni Chakechake walalamikia kodi kubwa wanayotozwa

Na Amina Mmanga na Mariam Pilipili, Pemba.
WAFANYABIASHARA wa soko la Chake Chake, wanailalamikia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kushindwa kupunguza kodi wanazotozwa wafanya biasha Bandarini, jambo ambalo linalopelekea kupanda kwa bei za bidhaa kiholela.
Wafanyabiashara hao walisema kuwa, Serikali kushindwa kupunguza kwa bei ya kodi za ushuru, wanazotozwa wakati wa kushusha biashara zao bandarini, kumepelekea bidhaa kupanda bei, hali inayowafanya kukosa wateja wakati wa kuuza bidhaa zao sokoni.
Walisema kuwa, imekuwa ni muda mrefu sasa tokea kupanda bei kwa bidhaa, katika Soko la Chake Chake, hali inayopelekea kuzorota kwa biashara na kupata hasara kubwa, jambo ambalo hurudisha nyumba maendeleo na kupelekea umasikini.
Wakizungumza na waandishi wa habari, kwa nyakati tofauti wafanya biashara wa soko la Chake Chake Kisiwani Pemba, waliiyomba Serikali kuwapunguzia kodi ya Bandarini, ili waweze kusonga mbele kimaisha.

Hemed Salim Hemed, ambae ni miongoni mwa wafanya biashara wa soko chake chake, alisema kuwa, Tungule na vitunguu maji, vimekuwa mstari wa mbele katika kupanda bei siku hadi siku,  ambapo tenga moja la Tungule limepanda kutoka Tsh 40,000 hadi Tsh 90,000,wakati gunia moja la Vitunguu maji limetoka Tsh 150,000 hadi kufikia Tsh195,000  .
“Kwa kweli bidhaa mbali mbali zimekuwa ni ghali sana, zinapanda bei siku hadi siku zinavyozidi kusongo mbele, tungule imekuwa ghali zaidi, kisado kimoja cha tungule imefikia sh 5000, wakati hapo awali ilikuwa sh 2,500, jambo ambalo imekuwa ni kero kwa wateja wetu “alisema  Hemed
Nae Juma Khamis Ali (Mshindo) alisema kuwa, Kerot na Pili pili boga imeonekana kwa sasa kupanda bei, ambapo awali ilikuwa ikiuzwa kilo moja Tsh 4500 wakati hivi sasa kilo inauzwa Tsh 6000.
Alisema kuwa kiroba kimoja cha Karoti hapo awali kilikuwa kikuuzwa Tsh 800,000, ambapo sasa kinauzwa Tsh 100000, kwa upande wa Nazi na Tangawizi, amesema kuwa bei zake ni na fuu kidogo ambapo gunia moja ya nazi ni Tsh 60,000 mwanzo ilikuwa ni Tsh 45,000 na kilo moja ya Tangawizi ni sh 2000 ambapo likuwa ni sh 1,500.
Kwa upande wa viazi mbatata, alisema kuwa rahisi katika soko hilo, kufuatia kushuka bei kutoka  Tsh 100,000 hadi kufikia 80,000 kwa gunia moja, jambo ambolo lilionekana kufurahiwa na wafanya biashara.
“ziko baadhi ya bidhaa ziko katika bei ya wastani, tofauti na bidhaa nyengine nyingi, ipo haja kwa Serikali kuzipunguzia ushuru bidhaa zote ili wananchi waweze kunufaika na kuondokana na umasikini”alisema.
Aidha aliwataka wafanya biashara wenzake, wawe na umoja na mshikamano, wakati wanapo panga mikakati ya biashara zao, kwa kujali maisha ya wananchi na kulingana na vipato vyao vilivyo.
“Kwa kweli kwa sisi wafanya biashara wa soko hili, tunaonekana hatuna umoja kwani, kuna wafanya biashara wengine wanakiuka kanuni na mipango ya biashara zetu, wakati tunapo panga bei “alisema Mshindo.
Saidi Mussa Omari, ambae ni miongoni mwa wafanya biashara wa soko hilo, anaetoa biasha kutoka Tanga hadi Pemba, alisema kuwa kupanda kwa bei hizo, kumepelekea kukosekana kwa usafiri wa uhakika kutoka Tanga, hadi kisiwani Pemba kwani, wakati mwengine wanasitisha safari zao kulingana na hali ya hewa inapokuwa mbaya .
“tunapo sitisha safari zetu kutokana na hali ya hewa, biashara hupanda kupitia kiasi, kwani zinakuwa zimepungua ila ni kutokana na kukosekana kwa usafiri wa uhakika”alisema.
 “mbali ya bidhaa kuwa ghali lakini tuna changamoto kubwa inayo tukabili katika Soko hili ikiwemo na ubovu wa Soko  hili la chake chake kuvuja na kutufanya kukosa raha wakati wa mvua zinapo nyesha.”alisema Saidi.
Na Mtumwa Salim Hamad ni mmoja wateja wa Soko hilo, alisema kuwa kwa kweli hali ya biashara ni ngumu sana, lakini hawanabudi kununua hivyo hivyo, na kuiyomba Serikali iwapunguze ushuru Bandarini, ili wafanya biashara waweze kupunguza bei kwani wanaumia.
Kwa upande wake mkuu wa Soko hilo, Khamis Abdalla Ali amesema kuwa, kuoanda bei kwa bidha hizo, halisabashiwa na soko hilo, bali ni ughali wa bidhaa kutoka kwao mkoani Tanga, pamoja na Serikali kutoza ushuru mkubwa wa Bandari.
“Ni kweli hali ya Soko yairizishi lakini ni meshawaita baraza la Mji na kuwaonesha na wamesema watafanyia utengenezi, hivyo nawaomba wafanya biashara na wateje kwa jumla wawe na ustahamilivu wa hali ya juu “alisema mkuu huyo .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.