Mkurugenzi wa Benchmak Productions na Jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi juu ya uzinduzi wa msimu mpya wa EBSS. Kushoto kwake ni Afsa Biashara mkuu wa Zantel, Sajid Khan
Meneja wa Kampeni wa Push Mobile, Rodney Rugambo akielezea namna usaili kwa njia ya simu utakavyofanyika
Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan akizungumza wakati wa kuzindua msimu mpya wa Epiq BSS. Kulia kwake ni Ritha Paulsen, Mkurugenzi wa Benchmark Productionsna jaji mkuu, na kushoto ni mshindi wa Epiq BSS mwaka jana, Walter Chillambo
Msimu huu mpya,ambao utakuwa msimu wa saba toka shindano hilo lianzishwe
mwaka 2006, unatarajiwa kujumuisha wadau wakubwa wa muziki, hivyo kusaidia
kuwajenga washiriki kwa kuwapa ujuzi zaidi pamoja na kuwajengea ushirikiano
utakaowasidia kuendeleza kazi zao za muziki baada ya mashindano.
Shindano la mwaka huu litakuwa na kauli mbiu ya ‘KAMUA’ ikimaanisha
kutumia uwezo wako wote katika kufanya kile unachopenda, litaenda kufanya
usaili kwenye mikoa sita ya Mbeya, Arusha, Zanzibar, Mwanza, Dodoma na Dar es
Salaam.
Kwa mwaka jana shindano la Epiq BSS lilipata mafanikio makubwa hasa kwa
idadi kubwa ya vijana kujitokeza kufanya usaili, na kubwa zaidi ikiwa ni vijana
wote walioingia kumi na mbili bora kufanikiwa kutoa nyimbo zao ambazo zimefanya
vizuri.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shindano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benchmark Production, Rita Paulsen amesema mwaka huu wana mpango wa kuwafikia
vijana wengi zaidi lakini pia kutengeneza wasanii nyota wengi zaidi ukiacha
mshindi.
“Sote ni mashahidi wa namna shindano hili lilivyopata
mafanikio toka ilipozinduliwa miaka saba iliyopita, na hakika kila mwaka
tumekuwa tukisogea mbele zaidi, na mwaka huu mpango wetu ni kuzalisha
wanamuziki watakaofanikiwa wengi zaidi’
Shindano la mwaka huu pia
litakuwa na vitu vingi vipya, ikiwemo ongezeko la jaji mmoja katika usaili wa
mikoani, ambapo jaji huyo atakuwa ni mdau wa mziki kutoka mkoa husika.
‘Kwenye kila mkoa tutakakoenda kufanya usaili tutakuwa
na jaji mwenyeji ambaye tunaamini atasaidia kuongeza ladha ya machaguo ya
vipaji na hivyo kuhakikisha tunapata vipaji aina tofaouti’ alisema Paulsen.
Naye Afsa biashara Mkuu wa
Zantel, Sajid Khan amesema uzinduzi huu wa leo ni furaha kubwa kwa kampuni ya
Zantel kwani unaashiria ufunguzi wa milango ya kuwasaidia vijana wengi wa
kitanzania kutimiza ndoto zao.
‘Kwa mwaka jana pekee Epiq
BSS ilifanikiwa kusaili vijana zaidi ya elfu hamsini, jambo ambalo linaonyesha
kitu kimoja, kuna uhitaji wa kuwekeza zaidi katika kuwaendeleza vijana’ alisema
Khan.
Ikitekeleza
ahadi yake ya kuwasaidia vijana baada ya shindano, kampuni ya Zantel
iliwarekodia wimbo mmoja mmoja washiriki wote waliongia kumi na mbili bora,
ikiwa ni pamoja na kuwapa ziara ya kujitangaza kwenye mikoa mitatu.
‘Tumefanikiwa
kuwajengea vijana hawa msingi wa kazi yao ya muziki, na tuna furaha kusema
wengi wao hadi sasa wanafanya vizuri, na huu ndio aina ya udhamini kampuni ya
Zantel inapenda kujihusisha nao’ alisisitiza Khan.
Mshindi wa mwaka huu pia
atajinyakulia milioni hamsini pamoja na mkataba wa kurekodi.
Katika kuwapa fursa vijana
ambao hawatafikiwa na majaji, Zantel pia itafungua laini za kurekodi kwa simu
toka siku ya kwanza ya kuanza usaili mikoani, ambapo washiriki watapiga namba
0901551000 ili kujirekodi kwa njia ya simu, au kutuma neno KAMUA kwenda 15530
kupata maelezo zaidi.
Usaili utaanzia Dodoma
tarehe 29 and 30 ya mwezi huu katika ukumbi wa Maisha Club, ikifuatiwa na
Zanzibar tarehe 5 na 6 mwezi wa saba katika hoteli ya Bwawani. Mbeya usaili
utakuwa tarehe 10 hadi 11 mwezi wa saba pale club Vybes, Mwanza
tarehe 14 hadi15 mwezi wa saba Club Fussion, na Arusha itakuwa
tarehe 20 hadi 21 mwezi wa saba Club Tripple A ikimalizikia na Dar
es Salaam tarehe 26 hadi 28 pale
Uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment