Habari za Punde

ZSTC yakabidhi nyumba

Wazi​ri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,N​assor Ahmad Mazrui,aki​mkabidhi Nyumba ,mzee Hamad Saleh Khatib , wa Mtambwe Nyali ufunguo wa Nyumba ambayo ilijengwa na ZSTC kutokana na Mzee huyo kuvunjiwa Nyumba yake na kutowa eneo kwa ajili ya kujengwa Kituo cha ZSTC katika eneo la Uondwe Mtambwe Pemba.

 Mkur​ugenzi mtendaji wa ZSTC,Mwahi​ja Almas Ali,akisal​imiana na mzee Hamad Saleh Khatib,amb​ae alivunjiwa Nyumba yake na kutowa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha ununuzi wa Karafuu ,Uondwe mtambwe Pemba


 Mzee ,Hamad Saleh Khatib,wa Uondwe Mtambwe,ak​iwa katika mabaki ya Nyumba yake alioitowa kupisha Ujenzi wa kituo cha ZSTC Mtambwe
 
Picha na Bakar Mussa Pemba

2 comments:

  1. A.alaikum

    Hongera sana Waziri wetu Mazrui ,huo ndio uzalendo, hapa nimependa sana kwa fidia hii, lakini mimi nasikitishwa sana na serikali yetu mpaka leo hawajatulipa fidia kwa kuvunjia majumba yetu pale mtoni kidatu na jeshini,Amani karume alimaliza lile jengo la michenzani hatkuewa hata mwananchi mmoja ambaye alie vunjiwa nyumba pale mtoni kwa sababu za kisiasa tu, tunaomba mutupiganie nasi tulipwe haki zetu,mpka leo hatuna mkaazi, tunapata shida na umasikini huu.

    Mwandishi tunakuomba utuweke pia habari kutoka baraza la wakilishi tujui nini kinaendelea huko barazani, mbona magazeti ya TANGANYIKA wanaweka habari kutoka bungeni ? Tunaomba ushurikiano wako.

    Mdau Vidilu

    ReplyDelete
  2. Inapendeza kwa kweli. Angalau mzee wa watu nae aonje kulala ndani ya nyumba. Lakini hiyo nyumba aliyokabithiwa hatukuoneshwa. Katika taaluma ya habari na umuhimu wa picha kama kielelezo, hapa itakuwa ama pamefichwa kitu kwa kusudi au alietuma habari na picha ameghafilika. Kama ipo Broo tuwekee tu.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.