Amesema Mtume Swalla
Allaahu ‘Alayhi wasallam
: " من
لم يدع قول الزور والعمل به والجهل فليس لله حاجة في أن يدع طعامه وشرابه " رواه
البخاري ومسلم
‘Yule asieacha kuzungumza maneno maovu na huku akiyatenda kwa
kughafilika au kutojua, Allaah (Subhaanahu
Wata’ala) hana haja na yeye kuacha chakula chake na kinywaji chake.’
Imepokewa
na Bukhaari na Muslim
Kusema
uongo, kuzua, kufitini, kutukana yote ni miongoni mwa mambo maovu yaliyokatazwa
kwa aliyefunga.
Allaah
Subhanahu Wata’ala ametuasa kuchunga ndimi zetu na kututaka mawazo yetu yaelekee kwenye
kuikamilisha funga kwani funga si kuacha kula na kunywa peke yake pamoja na
kustarehe bali pia ni kujizuia na maovu na maasi mengine.
Ewe
Mola tujaalie siku tunayofunga iwe tofauti kabisa na siku tusiyofunga ili
tuweze kuikamilisha funga yako tukitaraji malipo yako uliyotuahidi.
Aamiyn
Aamiyn
No comments:
Post a Comment