Mtume
Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:
الصِّيَامُ جُنَّةٌ، فَإِذَا كَانَ أَحَدُكُمْ صَائِمً
ا فَلَا يَرْفُثْ
وَ
لَا يَجْهَلْ، فَإِنِ امْرُؤٌ قَاتَلَهُ أَوْ شَاتَمَهُ
فَلْيَقُلْ إِنِّي صَائِمٌ إِنِّي صَائِمٌ”
Funga ni kinga.
Endapo mmoja wenu amefunga asitamke maneno machafu ( matusi na mfano wake) wala
asiseme kwa sauti kubwa ( wakati wa kukasirika). Na endapo mtu atataka ugomvi
nae au kamtukana basi amwambie, ‘Hakika mimi nimefunga, Hakika mimi nimefunga
Imepokewa
na AnNasaaiy
Tunapofunga
hatujizuii na kula, kunywa na matamanio ( kustarehe na aila zetu) pekee bali
pia hujizuia na mambo mengine kama ugomvi, matusi , kufitinisha na mawazo
yoyote ambayo yatatuweka mbali na Allaah Subhaanahu Wata’ala.Ndiyo maana
tumepewa suluhisho endapo tutajikuta katika hali hii ni kumjuulisha tu mwenzako
kama wewe upo katika funga hivyo haiyumkini kutenda au kunena yaliyo kinyume na
maadili ya funga.
Ewe
Mola, tuepushe ndimi zetu na matusi na maneno yenye kuudhi, tuepushe nyoyo zetu
na kuchukia na kufitinisha. Tuepushe viungo vyetu vyengine kujiepusha na yenye
kukuasi wewe Yaa Rabbal ‘Aalamiyn
Aamiyn
No comments:
Post a Comment