|
YALIYOMO
UTANGULIZI..........................................................
|
1
|
MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA MWAKA
2012/2013...............................................................................
|
4
|
Mpango kazi wa Elimu.......................................................
...
|
7
|
IDARA
YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI......................
|
9
|
Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Mwaka 2012/2013................................................................................
|
9
|
Mradi wa Upanuzi na Uimarishaji wa Huduma za Maktaba.
|
10
|
Mradi wa Uimarishaji wa Chuo Kikuu cha Taifa cha
|
10
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya
Msingi...........................
|
11
|
Mradi wa Ujenzi wa Vyuo vya Kiislam
................................
|
14
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya Mbadala na
Amali.......................................................................................
|
14
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya
Lazima...........................
|
17
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya
Ufundi............................
|
19
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya
Maandalizi.....................
|
20
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya Msingi kwa Wilaya ya
Magharibi................................................................................
|
22
|
Mradi wa
Sayansi na Technolojia...........................................
|
22
|
Mpango wa Maendeleo kwa Mwaka
2013/2014....................
|
23
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya Maandalizi.....................
|
23
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu
Msingi................................
|
24
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya Msingi kwa Wilaya ya
Magharibi................................................................................
|
25
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya
Lazima...........................
|
26
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya
Ufundi............................
|
27
|
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya Mbadala na
Amali.......................................................................................
|
27
|
Mradi wa Uimarishaji wa Chuo Kikuu cha Taifa cha
Zanzibar..................................................................................
|
28
|
Mradi wa Upanuzi na Uimarishaji wa Huduma za
Maktaba..................................................................................
|
28
|
Mradi wa Ujenzi wa Vyuo vya
Kiislam.................................
|
29
|
Utafiti.....................................................................................
|
29
|
Ukusanyaji na Uchambuzi wa Taarifa za
Elimu....................
|
30
|
Maendeleo ya
Kisera..............................................................
|
30
|
Ufuatiliaji na
Tathmini...........................................................
|
31
|
IDARA
YA UENDESHAJI NA UTUMISHI........................
|
31
|
IDARA YA ELIMU YA MAANDALIZI NA MSINGI........
|
34
|
Elimu ya Madrasa na Vyuo vya
Kuran..................................
|
35
|
Elimu ya
Maandalizi..............................................................
|
35
|
Elimu ya Msingi…………………………………………….
|
36
|
IDARA
YA ELIMU YA SEKONDARI.................................
|
39
|
Kazi za
Ujasiriamali...............................................................
|
40
|
Serikali za
Wanafunzi............................................................
|
40
|
Huduma za Dakhalia..............................................................
|
41
|
IDARA YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO KATIKA
ELIMU.....................................
|
41
|
Sera ya ICT katika Elimu na Mpango Mkakati
wake.............
|
42
|
Utekelezaji wa Mradi wa TZ-21 Century Basic
Education.................................................................................
|
42
|
Kuimarisha Njia za Mawasiliano na Usambazaji wa Taarifa
kupitia TEKNOHAMA...........................................................
|
42
|
Kuimarisha Elimu ya Maandalizi kwa Kutumia Vifaa vya
ICT..........................................................................................
|
43
|
IDARA YA ELIMU MBADALA NA WATU
WAZIMA................................................................................
|
44
|
Kisomo
...................................................................................
|
44
|
Vituo vya
Kujiendeleza..........................................................
|
45
|
Vyombo vya Habari................................................................
|
46
|
IDARA YA MAFUNZO YA
UALIMU.................................
|
47
|
Mafunzo ya Ualimu
Kazini.....................................................
|
48
|
OFISI YA MKAGUZI MKUU WA ELIMU..........................
|
51
|
TAASISI YA ELIMU
|
52
|
MAMLAKA YA MAFUNZO YA AMALI...........................
|
54
|
TAASISI YA ELIMU YA
JUU..............................................
|
56
|
CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA
|
56
|
TAASISI YA KARUME YA SAYANSI NA
TEKNOLOJIA........................................................................
|
59
|
CHUO KIKUU CHA
|
61
|
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU CHUKWANI.....
|
61
|
BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU............................
|
62
|
BARAZA LA
MITIHANI LA ZANZIBAR...........................
|
64
|
BODI YA HUDUMA ZA
MAKTABA..................................
|
66
|
KITENGO CHA
UHASIBU...................................................
|
68
|
KITENGO CHA
HABARI, ELIMU NA
MAWASILIANO....................................................................
|
68
|
KITENGO CHA UNUNUZI NA UGAVI..............................
|
70
|
KITENGO CHA UKAGUZI WA HESABU ZA NDANI.....
|
71
|
KITENGO CHA URATIBU WA ELIMU YA JUU..............
|
72
|
KITENGO CHA ELIMU MJUMUISHO NA STADI ZA MAISHA
………………………………................................
|
73
|
Elimu
Mjumuisho...................................................................
|
73
|
Ushauri
Nasaha.......................................................................
|
75
|
Mapambano dhidi ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya.........
|
75
|
Masuala ya
Jinsia...................................................................
|
75
|
KITENGO CHA
URAJISI.....................................................
|
76
|
Baraza la Elimu......................................................................
|
76
|
Leseni za
Walimu...................................................................
|
77
|
Maombi ya Usajili wa Skuli za Serikali na
Binafsi................
|
77
|
Kesi za Ujauzito na Ndoa za
Wanafunzi...............................
|
77
|
KITENGO CHA MICHEZO NA UTAMADUNI..................
|
78
|
MAPATO................................................................................
|
80
|
SHUKRANI............................................................................
|
81
|
JUMLA YA GHARAMA ZA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA
AMALI........................................................
|
81
|
KIAMBATISHO....................................................................
|
83
|
HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI KUHUSU MAKADIRIO YA
MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI KWA MWAKA WA
FEDHA 2013/2014
UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako
Tukufu sasa liingie katika Kamati ili niweze kutoa maelezo ya makadirio ya
mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa mwaka wa fedha
2013/2014.
2.
Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninamshukuru Mwenyezi
Mungu kwa kutuwezesha kukutana kwa mara nyengine tena katika kikao cha Bajeti
cha Baraza lako tukufu tukiwa wenye afya njema na wazima na kuniwezesha
kuwasilisha hotuba hii.
3.
Mheshimiwa Spika, pili, naomba kuchukua fursa hii
kuwapongeza Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Seif Sharrif Hamad, Makamu wa kwanza wa Rais
wa Zanzibar na Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar kwa mafanikio makubwa yaliopatikana katika Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ya awamu ya saba yenye muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Nawashukuru sana
kwa maelekezo, ushauri na ushirikiano mkubwa wanaonipa ambao umeniwezesha
kutekeleza majukumu niliyokabidhiwa katika sekta hii muhimu kwa maendeleo ya
taifa letu.
4.
Mheshimiwa Spika, pia, ninakupongeza kwa umahiri na
uwezo mkubwa unaouonesha katika kuliongoza Baraza lako tukufu kwa misingi ya
uadilifu na uaminifu mkubwa na hatimaye kutufikisha katika kikao hichi cha tatu
cha bajeti. Vile vile napenda kumpongeza Mheshimiwa Ali Abdulla Ali Naibu Spika
wa Baraza na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini kwa kukusaidia katika kuliongoza
Baraza letu. Pia napenda kuwapongeza Waheshimiwa Wenyeviti wa Baraza Mheshimiwa
Mgeni Hassan Juma na Mheshimiwa Mahmoud Mohammed Mussa kwa uongozi wao kwa Baraza.
Aidha, napenda kuwapongeza Waheshimiwa Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa Kamati
za Baraza la Wawakilishi na wajumbe wote walioteuliwa hivi karibuni katika
kamati mbali mbali za Baraza lako tukufu. Vile vile napenda kumpongeza
Mheshimiwa Hussein Ibrahim Makungu kwa kuchaguliwa kwake kuwa muwakilishi wa
jimbo la Bububu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
5.
Mheshimiwa Spika, napenda kuipongeza na kuishukuru
Kamati ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake ya Baraza la Wawakilishi
ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Mgeni Hassan Juma kwa kutuongoza vyema
na kutushauri ipasavyo. Wajumbe wa Kamati hii waliweza kuichambua na kujadili
hotuba ya bajeti kwa undani kabisa na mwishowe kuipitisha. Pia, ameweza kuishauri Wizara ipasavyo kila
walipotembelea shughuli tunazozisimamia.
6.
Mheshimiwa Spika, shukrani zangu pia ziende kwa
Waheshimiwa wajumbe wote wa Baraza lako Tukufu kwa namna walivyokuwa karibu na
wizara yangu katika kushajiisha wananchi wa maeneo yao katika kusukuma mbele shughuli za
kielimu.
7.
Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, napenda kumshukuru
kwa dhati msaidizi wangu, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mheshimiwa
Zahra Ali Hamad kwa juhudi zake, mashirikiano anayonipa katika kutekeleza
majukumu tuliopewa na Taifa. Aidha
napenda kuwapongeza watendaji wakuu na wafanyakazi wote wa Wizara yangu
wakiwemo Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Kamishna, Wakurugenzi, maafisa wa
ngazi mbali mbali za elimu, walimu na wafanyakazi wengineo wote wa Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kufanya kazi kwa nidhamu, bidii na ushirikiano,
hali ambayo imeniwezesha kuwasilisha hotuba hii mbele ya Baraza lako Tukufu.
8.
Mheshimiwa Spika,
Vile vile napenda kuwashukuru kwa
dhati wananchi wa Jimbo la Donge kwa kunipa ushirikiano mkubwa katika kutimiza
majukumu yangu nikiwa Mwakilishi wao.
9.
Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii
kuishukuru kwa dhati kabisa Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo
kwa ushirikiano mkubwa uliotupa mwaka 2012/2013. Kwa ujumla upatikanaji wa
fedha ulikuwa ni wa kuridhisha kwani hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013 jumla ya
T.Sh. 3,016,700,000/- zilipatikana kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za
maendeleo ikiwa ni sawa na asilimia 59.2 ya makadirio. Kwa upande wa kazi za
kawaida, jumla ya T.Sh. 67,691,445,910/- zilipatikana ikiwa ni sawa na asilimia
95.3 ya makadirio. Jadweli namba 10 (a) na (b) zinatoa uchambuzi zaidi. Ni
matumaini yangu kwamba ushirikiano huu utaendelezwa na kudumishwa.
10.
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuelezea utekelezaji wa
shughuli za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kipindi cha mwaka
2012/2013, naomba uniruhusu nieleze kwa ufupi mafanikio yaliyopatikana katika
Wizara hii kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
MAFANIKIO
YALIYOPATIKANA KATIKA MWAKA 2012/2013
11.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imepata mafanikio
makubwa katika sekta ya elimu kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Miongoni mwa mafanikio hayo ni :-
·
Wizara
imesaini hati ya maelewano na Wizara ya Elimu ya Juu ya Falme ya Oman
juu ya ushirikiano katika ngazi ya elimu ya juu. Kupitia maelewano hayo
Serikali ya Falme ya Oman
imeanzisha Mpango wa kuwagharimia masomo ya juu wanafunzi wetu kwa kupitia Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar .
Mpango huo unaoitwa “Sultan Qaboos
Academic Fellowship for SUZA” (SQF) umeanza kufanya kazi kwani nafasi za
masomo ya juu zimetangazwa na vijana mbali mbali wameomba nafasi za udhamini wa
masomo katika ngazi ya shahada ya kwanza, shahada ya uzamili na shahada ya
uzamivu.
·
Idadi
ya wanafunzi waliogharimiwa masomo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Zanzibar iliongezeka
kutoka wanafunzi 1,086 mwaka 2011/2012 hadi wanafunzi 1,897 mwaka 2012/2013.
·
Walimu
wapya 578 waliajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi.
·
Ujenzi
wa skuli mpya za sekondari 13 kati ya 16 umekamilika. Skuli hizo ni Mwanda,
Chaani, Matemwe, Uzini na Dole kwa Unguja na Utaani, Ngwachani, Wawi,
Kiwani-mauani, Tumbe, Konde, Pandani na Madungu kwa Pemba .
Skuli hizi zote zimekamilika na kuanza kutumika
·
Ujenzi
wa skuli mpya za sekondari za ghorofa katika maeneo ya Kiembesamaki,
Kwamtipura, Mpendae (ufadhili wa Benki ya Dunia) Kibuteni na Mkanyageni
(ufadhili wa Badea) unaendelea.
·
Ukarabati
wa skuli za sekondari za Forodhani na Tumekuja kwa Unguja na Utaani na Fidel
Castro kwa Pemba umekamilika na skuli hizo
hivi sasa zinatumika. Ukarabati wa skuli za sekondari za Hamamni kwa Unguja na
Uweleni kwa Pemba unaendelea na uko katika
hatua za mwisho.
·
Awamu
ya pili ya ujenzi wa kampasi ya Chuo cha Ualimu cha Benjamin William Mkapa huko
Mchangamdogo, Pemba imekamilika.
·
Ujenzi
wa skuli mpya ya msingi ya kisasa iliyofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu
wa China
hapo Mwanakwerekwe imekamilika na kukabidhiwa rasmi.
·
Vifaa
mbali mbali vya teknolojia ya habari na mawasiliano zikiwemo kompyuta
vimefungwa na kusambazwa katika skuli 74 za msingi kupitia mradi wa TZ-21. Kazi
ya kufunga na kusambaza inaendelea katika skuli zilizobakia.
·
Matokeo
ya mtihani kidato cha pili yalikuwa mazuri ambapo kati ya wanafunzi 19,679
(wanawake 11,045 na wanaume 8,644) wa skuli za sekondari za Serikali walifanya
mtihani huo mwezi wa Novemba 2012, wanafunzi 11,195 (wanawake 6,768 na wanaume
4,427) wamefaulu na kuchaguliwa kuingia kidato cha tatu mwaka 2013. Idadi hii
ni sawa na asilimia 56.9 ya waliofanya mtihani huo. Kiwango hiki cha ufaulu
kimepanda kwa asilimia 0.8 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2011.
·
Shirika
la “Global Partnership for Education
(GPE)” lenye makao makuu yake mjini Washington
limeidhinisha msaada wa dola za Kimarekani millioni 5.2 kwa ajili ya
utekelezaji wa mpango kazi wa elimu wa Zanzibar
kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2013/2014 hadi 2015/2016. Fedha hizo
zitatumika katika kuinua ubora wa elimu yetu katika ngazi ya maandalizi na
msingi.
·
Vipando
230 vimenunuliwa na SACCOS za Elimu, Unguja na Pemba
kwa ajili ya kuwakopesha walimu.
Mpango
Kazi wa Elimu
12.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa mpango kazi wa
maendeleo ya elimu kwa kipindi cha miaka minne ya mwisho, kuanzia mwaka
2012/2013 hadi 2015/2016. Mpango kazi huo umezingatia Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2020, Awamu ya
Pili ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUZA II), na ilani ya
Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010 hadi 2015. Mpango kazi huo unatoa
mwongozo wa njia ya kufikiwa kwa malengo ya Elimu kwa Wote na Malengo ya
Milenia kwa upande wa elimu ifikapo mwaka 2015. Shabaha za mpango kazi huo
ifikapo mwaka 2016 ni kama hivi ifuatavyo:
·
Uandikishaji
safi (NER) wa
wanafunzi katika ngazi ya elimu ya maandalizi ifikie asilimia 30.
·
Uandikishaji
safi (NER) wa
wanafunzi katika ngazi ya elimu ya msingi ifikie asilimia 95.
·
Idadi
ya wanafunzi kwa darasa ipunguwe hadi wanafunzi 40 kwa darasa.
·
Asilimia
ya wanafunzi wanaofanya mtihani wa Kidato cha Pili na kufaulu na kuchaguliwa
kuendelea na masomo ya Kidato cha tatu ifikie asilimia 70. Pia zaidi ya
asilimia 50 ya wanafunzi wote wanaoandikishwa kufanya mtihani wa kuingilia Kidato
cha tatu waweza kufaulu katika masomo ya Kiingereza, Hisabati, Biolojia, Kemia
na Fizikia.
·
Asilimia
ya wanafunzi wa kidato cha nne wanaofaulu na kupata sifa za kuendelea na masomo
ya kuingia kidato cha tano iongezeke hadi kufikia asilimia 20 ya wanafunzi wote
walioandikishwa kufanya mtihani.
·
Idadi
ya wanafunzi wanaojiunga na taasisi za
elimu ya juu, iongezeke na kufikia asilimia 20 ya wanafunzi wote
waliomaliza kidato cha sita.
·
Asilimia
50 ya waombaji wa mkopo wa elimu ya juu waweze kupatiwa mikopo ya kusoma katika
taasisi za elimu ya juu.
·
Wanafunzi
wote wa msingi wapatiwe vitabu vyote vya kiada;
·
Wanafunzi
wote wenye mahitaji maalum waweze kupatiwa vifaa maalumu kwa ajili ya kusomea
na kujifunzia na kuweza kusoma katika mazingira rafiki;
·
Vituo
vya elimu ya watu wazima vitowe elimu ya watu wazima kwa mujibu wa mahitaji ya
soko la ajira;
·
Walimu
wote wa msingi na sekondari wawe wamefuzu mafunzo ya ualimu.
·
Uongozi
na usimamizi wa elimu uweze kuimarishwa katika ngazi zote;
·
Skuli
zote za msingi na sekondari ziweze kufanyiwa ukaguzi kila mwaka;
·
Miundo
mbinu ya Taasisi za elimu ya juu iweze kuimarishwa; na
·
Kuongeza
fursa za upatikanaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya amali.
13.
Mheshimiwa Spika, mpango kazi unatekelezwa kwa
ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi, mashirika yasio ya kiserikali,
wahisani mbali mbali pamoja na wananchi wote kwa jumla. Baadhi ya shabaha za
mpango kazi huu yanatekelezwa kupitia miradi mbali mbali iliyomo katika mipango
ya maendeleo na bajeti yetu ya kazi za kawaida.
14.
Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, sasa naomba
uniruhusu nieleze kuhusu shughuli mbali mbali zilizotekelezwa katika Idara moja
moja na taasisi zinazojitegemea katika mwaka 2012/2013 na matarajio na malengo
kwa mwaka 2013/2014.
IDARA YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI
15.
Mheshimiwa
Spika, Idara ya Sera, Mipango na Utafiti ina majukumu ya
kuandaa mipango ya maendeleo, kuratibu na kufuatilia raslimali na misaada mbali
mbali ya wahisani, kusimamia, kufanya mapitio ya tathmini ya sera, mipango
programu na miradi mbali mbali inayotekelezwa na Wizara, kuratibu shughuli za
utafiti wa kielimu na kusimamia ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji wa
takwimu mbali mbali za kielimu.
Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Mwaka
2012/2013
16.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2012/2013, Wizara ilipanga kutekeleza
jumla ya miradi kumi ya maendeleo. Miradi hiyo ilitengewa jumla ya T.Sh.
38,969,291,000/-, kati ya fedha hizo T.Sh.5,100,000,000/- ni za mchango wa SMZ,
T.Sh. 3,208,315,000/- ni ruzuku kutoka kwa wahisani mbali mbali wa maendeleo na
T.Sh. 30,660,976,000/- ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB),
Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) na Benki ya Dunia. Hadi
kufikia tarehe 30 Juni 2013, jumla ya T.Sh. 2,614,700,000/= za SMZ zilipatikana
ikiwa ni sawa na asilimia 59.2 ya makadirio. Kwa upande wa washirika wa
maendeleo, fedha zilizopatikana ni T.Sh. 28,559,603,224.68 sawa na asilimia
84.3 ya makadirio.
Utekelezaji halisi wa miradi hiyo ni
kama ifuatavyo:-
Mradi wa Upanuzi na Uimarishaji wa Huduma za Maktaba
17.
Mheshimiwa
Spika, mradi ulipangiwa kutumia jumla ya T.Sh. 200,000,000/=
kwa ajili ya kutangaza zabuni ya ujenzi wa tawi la Maktaba Kuu Pemba, kumchagua
mkandarasi, kujenga msingi wa jengo jipya na kufanya ukarabati wa jengo la
Maktaba liliopo. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013, jumla ya T.Sh. 55,000,000/=
zilipatikana ikiwa ni sawa na asilimia 27.5 ya makadirio. Kazi zilizofanyika ni kumchagua mkandarasi na
kutiliana saini mkataba wa ujenzi.
Mradi wa
Uimarishaji wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.
18.
Mheshimiwa
Spika, mradi huu unatekelezwa na SMZ kwa kushirikiana na
Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) na ulikuwa na malengo
yafuatayo:-
(i)
Kufunga vifaa vya ICT na vipoza hewa katika majengo
mawili.
(ii)
Kuweka miundombinu kwa ajili ya mawasiliano ya simu
na “Internet”.
(iii)
Kununua vifaa vya kufundishia kwa ajili ya Kitivo cha
Uhandisi.
(iv)
Kukamilisha kazi za ujenzi na kusambaza miundo mbinu
ya umeme.
(v)
Kuanza
kutumiwa kwa majengo.
Mradi huu ulipangiwa kutumia jumla ya
T.Sh. 1,725,000,000/- za SMZ na T.Sh.4, 332,959,000/- za BADEA. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013 jumla ya
T.Sh. 1,659,700,000/- za SMZ sawa na asilimia 96.2 ya makadirio zilipatikana.
Aidha, kwa upande wa BADEA, T.Sh. 594,833,392/= zilipatikana ikiwa sawa na
asilimia 13.7 ya makadirio. Utekelezaji halisi ni kama
ifuatavyo:-
i)
Vifaa
vya ICT na vipoza hewa vimenunuliwa na vimefungwa.
ii)
Miundo
mbinu kwa ajili ya mawasiliano ya simu na “Internet” imewekwa. Kampasi ya
Tunguu imeunganishwa na huduma za Intenet.
iii)
Ujenzi
wa majengo ya SUZA huko Tunguu umekamilika pamoja na miundo mbinu ya umeme. Majengo
mapya ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
yaliyopo Tunguu yalihamiwa mwezi wa Oktoba mwaka wa 2012 na kuanza kutumika
rasmi.
iv)
Baadhi
ya vifaa vya maabara vimepatikana.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu ya Msingi
19.
Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa kwa
mashirikiano baina ya wananchi, SMZ, Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ,
Sida, UNICEF, UNESCO na USAID. Mradi
ulitengewa jumla ya T.Sh.800,000,000/- za SMZ na T.Sh. 3,045,061,000/- kutoka
Sida, UNESCO na UNICEF na ulikuwa na malengo yafuatayo:-
(i)
Kukamilisha
ujenzi wa madarasa 150 kwa kushirikiana na wananchi katika Wilaya tisa za
Unguja na Pemba .
(ii)
Kufanya ukarabati katika skuli 15 za msingi.
(iii)
Kuchonga madawati 2,250 na kuyasambaza katika
madarasa mapya yaliyojengwa.
(iv)
Kuwapatia walimu mafunzo mbali mbali yakiwemo ya
matumizi ya lugha ya Kiingereza kwa ajili ya kufundishia, mafunzo juu ya
matumizi ya mtaala mpya wa ngazi ya msingi na mafunzo ya kufundisha katika
mfumo wa elimu mjumuisho.
(v)
Kukamilisha
ujenzi wa nyumba tatu za walimu.
(vi)
Kuendeleza
ujenzi wa skuli moja ya msingi katika eneo la Mwanakwerekwe.
(vii)
Kutoa
mafunzo kwa walimu na kamati za skuli juu ya kuimarisha huduma za maji, afya na
mazingira katika skuli.
(viii)
Kuendelea
na utekelezaji wa mradi wa TZ-21.
Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013,
jumla ya T.Sh. 407,000,000/- za SMZ zilipatikana sawa na asilimia 51 ya
makadirio. Kwa upande wa Sida, UNICEF na UNESCO fedha zilizotolewa ni T.Sh.
4,643,963,511.78/- sawa na asilimia 149 ya makadirio. Hii imetokana na
kupatikana fedha nyingi zaidi kutoka Sida kuliko ilivyotarajiwa. Utekelezaji
halisi ni kama ifuatavyo:-
i)
Jumla
ya madarasa 51 (Unguja 24, Pemba 27) ya skuli
za msingi yamekamilishwa. Ujenzi wa madarasa mengine 118 (Unguja 66, Pemba 52) unaendelea.
ii)
Ukarabati
wa majengo umefanyika katika skuli za msingi za Chuini, Kidimni, Kitogani, Kilimahewa,
Unguja-Ukuu na Micheweni.
iii) Jumla ya madawati 1,782, viti 774 na
meza 774 yamechongwa na kusambazwa katika skuli za msingi na sekondari za
wananchi.
iv) Ujenzi wa skuli ya msingi ya Urafiki
iliyopo Mwanakwerekwe umekamilika kwa hatua zote. Wizara imekabidhiwa skuli hiyo pamoja na
samani za madarasani, ofisini na maktaba tarehe 21 Aprili, 2013.
v)
Majaribio
(pilot testing) ya matumizi ya miongozo ya maji, afya na mazingira katika skuli
yametolewa kwa walimu 36 wa skuli za msingi za Pemba
na wajumbe wa kamati za skuli 15 za Unguja. Ujenzi wa vyoo, minara ya maji na
sehemu za kukoshea mikono katika skuli 13 (Unguja 05 na Pemba
08) unaendelea.
vi) Mradi wa TZ-21 umeendelezwa kwa kutoa
machapisho ya “e-content”, kutathmini miundiombinu ya vyuo vya ualimu, vituo
vya walimu na skuli za msingi ili kuona utayari wao wa kupokea vifaa vya ICT na
kuunganishwa na huduma ya “internet”. Pia vifaa mbali mbali zikiwemo kompyuta
vimefungwa katika skuli 74. Jumla ya nakala 33,884 za vitabu zimechapishwa na
kugawiwa katika skuli za msingi, vituo vya walimu na vyuo vya ualimu. Programu
mpya (EMIS Database) kwa ajili ya uingizaji na uchambuzi wa takwimu imewekwa
Wizarani. Wafanyakazi 12 wa divisheni ya
takwimu wamefundishwa (kwa vitendo) jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kompyuta kwa
kuingiza na kusafisha data na kutoa ripoti za kitakwimu.
Mradi
wa Ujenzi wa Vyuo vya Kiislamu
20.
Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa na SMZ pekee
na ulikuwa na malengo yafuatayo:-
(i)
Kujenga
uzio kuzunguka eneo la Chuo cha Kiislamu Micheweni na Chuo cha Kiislamu
Mazizini.
(ii)
Kuendeleza
ukarabati wa majengo ya Chuo cha Kiislamu Micheweni.
Mradi huu ulitengewa jumla ya T.Sh.
25,000,000/-. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013, mradi uliingiziwa T.Sh.
20,000,000/- sawa na asilimia 80 ya makadirio. Kazi za ujenzi wa uzio
zinaendelea.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu Mbadala na Amali.
21.
Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa na SMZ kwa
mashirikiano na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Mradi ulipangiwa
kutekeleza malengo yafuatayo:-
(i)
Kuendelea
kutoa mikopo kwa vikundi vya wahitimu kutoka vituo vya mafunzo ya amali.
(ii)
Kuendeleza
ujenzi wa Kituo cha Elimu Mbadala cha Wingwi Mtemani Pemba.
(iii)
Kutafuta
washauri elekezi na wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya elimu mbadala
vitatu, vituo vya mafunzo ya amali viwili, upanuzi na ukarabati wa Taasisi ya
Karume ya Sayansi na Teknolojia, upanuzi na ukarabati wa Chuo cha Maendeleo ya
Utalii Zanzibar na ujenzi wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali
Zanzibar.
(iv)
Kuandaa
mitaala kwa ajili ya mafunzo ya wakufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii
Zanzibar na wakufunzi wa mafunzo ya amali.
(v)
Kupitia
na kurekebisha mitaala ya mafunzo kwa wanafunzi wa vituo vya Elimu Mbadala.
(vi)
Kununua
vifaa na magari kwa ajili ya Ofisi ya uratibu wa mradi wa Kamisheni ya Kazi.
Jumla ya T.Sh. 100,000,000/- za SMZ
na T.Sh. 1,994,098,000/- za AfDB zilitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi
huu. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013,
jumla ya T.Sh. 65,000,000/- za SMZ sawa na asilimia 65 ya makadirio
zilipatikana. Aidha T.Sh. 1,230,072,040/- za AfDB sawa na asilimia 61.7 ya
makadirio zilipatikana. Utekelezaji halisi ni kama
ifuatavyo:-
i)
Wizara
imevikopesha vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS) vya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali, Unguja na Pemba jumla ya
T.Sh. 530,500,000/- kwa ajili ya kununua vespa za kuwakopesha walimu. Jumla ya
vespa 100 zimekopeshwa kwa walimu wa skuli za Unguja na vespa 130 zimekopeshwa
kwa walimu wa skuli za Pemba . Aidha, jumla ya
T.Sh. 154,950,000/- zimekusanywa kutoka kwa vikundi vilivyokopeshwa hapo
zamani.
ii)
Jumla
ya T.Sh. 30,000,000/= zimetumika kwa ajili ya kuwalipa fidia ya mazao wananchi
wa Vitongoji ambao mazao yao
yaling’olewa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji.
iii) Uchambuzi wa tathmini ya zabuni za
kuwaajiri washauri elekezi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya viwili vya elimu
mbadala, vituo viwili mafunzo ya amali, upanuzi na ukarabati wa Taasisi ya
Karume ya Sayansi na Teknolojia, upanuzi na ukarabati wa Chuo cha Maendeleo ya
Utalii Zanzibar na ujenzi wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali
unaendelea.
iv) Uchambuzi wa tathmini za zabuni za
kuwaajiri washauri elekezi kwa ajili ya kazi ya kupitia na kurekebisha mitaala
kwa ajili ya mafunzo ya wakufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar,
wakufunzi wa mafunzo ya amali na mafunzo ya wanafunzi wa vituo vya elimu
mbadala umekamilika. Washauri hao wameanza
kazi ya kuandika mitaala husika.
v)
Vifaa
vya ofisi na gari nne za mradi zimenunuliwa.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu ya Lazima.
22.
Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa kwa
mashirikiano baina ya SMZ, Benki ya Dunia na BADEA. Mradi huu ulikuwa na malengo yafuatayo:-
(i)
Kukamilisha
ujenzi wa skuli za sekondari za ghorofa za Kiembesamaki, Kwamtipura na Mpendae.
(ii)
Kukamilisha
ujenzi wa skuli za sekondari za Miwaleni, Donge, Maungani, Makongeni na
Chanjamjawiri zilizoanzishwa na wananchi.
(iii)
Kukamilisha
ujenzi wa skuli za sekondari za Paje Mtule, Tunguu na Dimani.
(iv)
Kukamilisha
ukarabati wa skuli za sekondari za Tumekuja, Fidel Castro, Forodhani, Uweleni,
Hamamni na Utaani.
(v)
Kuchonga
seti 2,000 za meza na viti kwa madarasa ya sekondari yaliyomalizika kujengwa.
(vi)
Kuanza
ujenzi wa skuli mpya za sekondari za Kibuteni Unguja na Mkanyageni Pemba .
(vii)
Kuandika,
kuchapisha na kusambaza vitabu vya kiada na miongozo ya walimu kwa ajili ya
madarasa ya kwanza hadi la nne.
(viii)
Kuandika
na kuchapisha moduli za kutolea mafunzo kazini kwa walimu wa Sayansi na
Hisabati wa msingi.
(ix)
Kutoa
mafunzo kwa walimu wa msingi na sekondari.
(x)
Kutoa
mafunzo kwa walimu wakuu juu ya uendeshaji wa skuli.
Mradi huu ulitengewa jumla ya T.Sh.
900,000,000/- za SMZ, T.Sh. 24,000,000,000/- za Benki ya Dunia na T.Sh.
3,930,054,000/- za BADEA. Hadi kufikia
tarehe 30 Juni 2013, jumla ya TSh. 525,000,000/- za SMZ sawa na asilimia 58.3
zilipatikana. Pia T.Sh. 21,790,084,140.90/- za BADEA na Benki ya Dunia sawa na
asilimia 92.3 ya makadirio zimepatikana.
Utekelezaji halisi ni kama ifuatavyo:-
i)
Ujenzi
wa skuli za sekondari za ghorofa unaendelea katika skuli za sekondari za
Mazizini, Kwamtipura na Mpendae. Skuli hizi zote zinatarajiwa kukamilika na
kutumika mara tu skuli zitakapofunguliwa katika mwezi Agosti 2013.
ii)
Ujenzi
wa skuli mpya za sekondari za Paje Mtule, Tunguu na Dimani umefikia asilimia
94.
iii)
Ukarabati
wa skuli za sekondari za Utaani, Fidel-Castro, Forodhani na Tumekuja umekamilika
na skuli hizo hivi sasa zinatumika. Ukarabati wa skuli za sekondari ya Uweleni
na Hamamni unaendelea.
iv)
Ujenzi
wa skuli mpya za sekondari za Kibuteni, Unguja na Mkanyageni, Pemba
unaendelea vizuri.
v)
Jumla
ya samani 80,806 zimepokelewa kwa ajili ya skuli mpya za sekondari za Mwanda,
Chaani, Matemwe, Uzini, Dole, Paje-Mtule, Dimani na Tunguu kwa Unguja na
Utaani, Ngwachani, Wawi, Madungu, Kiwani-Mauani, Chwaka-Tumbe, Konde, Pandani
na Chuo cha Ualimu Benjamin Mkapa (awamu ya kwanza).
vi)
Wizara
imetiliana saini mikataba na wazabuni watano wa kuandika na kuchapisha vitabu
na miongozo ya walimu kwa ajili ya wanafunzi wa madarasa ya kwanza hadi la nne.
Kazi ya uandishi na uhariri wa miswada ya vitabu hivyo inaendelea.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu ya Ufundi
23.
Mheshimiwa Spika, mradi huu umetekelezwa na SMZ pekee
na ulikuwa na malengo yafuatayo:-
(i)
Kuanza
ujenzi wa dakhalia mpya ya skuli ya sekondari ya ufundi Kengeja.
(ii)
Kuipatia
skuli ya sekondari ya ufundi Kengeja vifaa vya karakana
(iii)
Kuendelea
na ukarabati wa majengo, kununua vifaa vya kufundishia na vitabu kwa ajili ya Taasisi
ya Karume ya Sayansi na Teknolojia.
Jumla ya T.Sh. 400,000,000/- za SMZ
zilitengwa kwa ajili ya kukamilisha malengo yaliyowekwa. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013, jumla ya
T.Sh. 50,000,000/- zimepatikana ikiwa ni sawa na asilimia 25 ya makadirio.
Utekelezaji halisi ni kama ifuatavyo:-
i)
Wizara
imetiliana saini na kampuni itakayopeleka vifaa vya karakana ya umeme katika
skuli ya sekondari ya ufundi ya Kengeja.
ii)
Ukarabati
wa mfumo wa maji safi
katika eneo la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia umekamilika. Pia,
vifaa mbali mbali vya kufundishia vikiwemo “multimedia” tatu na vitabu 150 vya
somo la Hisabati vimenunuliwa.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu ya Maandalizi.
24.
Mheshimiwa Spika, mradi huu ulitengewa jumla ya T.
Sh. 150,000,000/- za SMZ na T.Sh. 491,200,000/- za UNICEF. Malengo ya mradi huu
yalikuwa ni :-
i)
Kuendelea
kutoa mafunzo ya mtaala mpya kwa walimu wa elimu ya maandalizi.
ii)
Kuandika
na kuchapisha moduli kwa ajili ya wakufunzi wa walimu wa maandalizi kwa njia ya
redio.
iii) Kuanza kutoa mafunzo ya walimu wa
maandalizi 1,000 kwa njia ya redio.
iv) Kununua vifaa vya kufundishia.
v)
Kujenga
na kuchonga samani za skuli mbili mpya za maandalizi.
Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013,
jumla ya T.Sh. 50,000,000/- za SMZ sawa na asilimia 33.3 ya makadirio
zilipatikana na kutumika. Kwa upande wa UNICEF, T.Sh. 23,357,300/- sawa na
asilimia 22.9 zimepatikana. Utekelezaji halisi wa mradi ulikuwa kama ifuatavyo:-.
i)
Walimu
210 wa elimu ya maandalizi wa skuli za Unguja na Pemba
wamepatiwa mafunzo juu ya utumiaji wa mtaala mpya wa elimu ya maandalizi
ii)
Ujenzi
wa skuli ya maandalizi Jongowe umeanza na ujenzi wa skuli ya maandalizi Konde
umeendelezwa.
iii) Ukarabati wa madarasa matatu na vyoo
vya skuli ya maandalizi Machomanne umefanyika.
iv) Moduli ya tatu kwa ajili ya kutolea
mafunzo kwa wakufunzi wa walimu wa maandalizi imeandikwa. Mafunzo kwa walimu
yatatolewa baada ya kukamilika kwa uandishi na kuchapishwa kwa moduli ya nne
hadi ya sita.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu ya Msingi kwa Wilaya ya Magharibi
25.
Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa na SMZ pekee
na ulikuwa na malengo yafuatayo :-
i)
Kukamilisha
ujenzi wa madarasa 70 yaliyoanzishwa na wananchi.
ii)
Kuchonga
madawati 1,050.
Mradi huu ulitengewa jumla ya T.Sh.
800,000,000/- kwa ajili ya kukamilisha malengo yaliyowekwa.
Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013,
jumla ya T.Sh. 135,000,000/= zimepatikana ikiwa ni sawa na asilimia 16.9 ya
makadirio. Jumla ya madarasa 18 katika skuli za Chuini, Kianga, Fuoni-Birikani
na Kinuni yamekamilika.
Mradi
wa Sayansi na Teknolojia
26.
Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa na Chuo Kikuu
cha Taifa cha Zanzibar
kwa mashirikiano na Benki ya Dunia na ulikuwa na malengo yafuatayo:-
i)
Kununua
vifaa vya maabara za Sayansi na ICT.
ii)
Kusomesha
wakufunzi katika ngazi ya shahada ya pili na ya tatu.
Mradi ulitengewa jumla ya T.Sh.
830,529,600/- za Benki ya Dunia. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013, jumla ya
T.Sh. 277,292,840/- sawa na asilimia 34.1 ya makadirio zimepatikana na
kutumika. Utekelezaji halisi wa malengo
ni kama ifuatavyo:-
i)
Vifaa
mbali mbali vya kufundishia vikiwemo vitabu, vifaa vya maabara na vya ICT
vimenunuliwa.
ii)
Jumla
ya wafanyakazi 56 (31 shahada ya uzamivu, 21 shahada ya uzamili, 02 shahada ya
kwanza na 02 stashahada wanaendelea na masomo katika vyuo mbali mbali. Ada za masomo na stahiki
nyengine zimelipwa.
Mpango
wa Maendeleo kwa Mwaka 2013/2014
27.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014,
Wizara imepanga kutekeleza miradi tisa yote ikiwa ni miradi inayoendelea. Kati
ya miradi hiyo, minne inatarajiwa kutekelezwa kutokana na bajeti ya SMZ pekee
na miradi mitano itatekelezwa kwa mashirikiano baina ya Serikali na washirika
wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi.
Jumla ya T.Sh. 5,350,000,000/- za SMZ na T.Sh.8,779,632,000/- ambazo ni
ruzuku kutoka kwa washirika mbali mbali wa maendeleo na TSh. 21,417,987,000/-
ni mkopo kutoka Benki ya Dunia, Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika
(Badea) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimetengwa kwa ajili ya
utekelezaji wa malengo ya miradi hiyo. Jadweli namba 46 inatoa uchambuzi zaidi.
Malengo ya miradi mbali mbali
itakayotekelezwa ni kama ifuatavyo:-
Mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya Maandalizi.
28.
Mheshimiwa Spika, mradi huu utatekelezwa kwa
mashirikiano kati ya SMZ, GPE na UNICEF.
Malengo ya mradi huu ni kama hivi ifuatavyo:-
i)
Kuendelea
kutoa mafunzo ya mtaala mpya kwa walimu wa elimu ya maandalizi.
ii)
Kukamilisha
ujenzi wa skuli za maandalizi za Jongowe na Konde.
iii) Kununua samani kwa skuli za
maandalizi za Jongowe, Konde na Tunduni.
iv) Kuwapa mafunzo walimu wa skuli za
maandalizi kwa kupitia vipindi vya redio.
v)
Kuandika
na kuchapisha moduli ya 4 na ya 5 kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa wakufunzi wa
walimu wa maandalizi kwa njia ya redio.
vi) Kununua vifaa vya kufundishia watoto
wa vituo vya Tucheze Tujifunze.
Mradi umetengewa jumla ya T.Sh.
150,000,000/- za SMZ na T.Sh. 1,567,600,000/- za UNICEF na GPE.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu ya msingi
29.
Mheshimiwa Spika, mradi huu utatekelezwa kwa
mashirikiano kati ya wananchi, mashirika ya maendeleo yakiwemo Sida, UNICEF,
UNESCO, GPE na USAID. Mradi huu utakuwa na
malengo yafuatayo:-
i)
Kukamilisha
ujenzi wa madarasa 480 kwa kushirikiana na wananchi katika wilaya tisa za
Unguja na Pemba .
ii)
Kufanya
ukarabati wa majengo katika skuli 12 za msingi.
iii)
Kuchonga
madawati 10,000 na kuyasambaza katika madarasa mapya yaliyojengwa.
iv)
Kuwapatia
walimu mafunzo mbali mbali yakiwemo ya matumizi ya lugha ya Kiingereza kwa
ajili ya kufundishia, mafunzo juu ya mtaala mpya wa ngazi ya msingi na mafunzo
juu ya kufundisha katika mfumo wa elimu mjumuisho.
v)
Kukamilisha
ujenzi wa nyumba tatu za walimu.
vi)
Kuendelea
na utekelezaji wa mradi wa TZ-21.
Mradi umetengewa jumla ya T.Sh.
1,000,000,000/- za SMZ, T.Sh. 7,212,032,000/- kutoka Sida, UNICEF, UNESCO na
GPE.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu ya Msingi Wilaya ya Magharibi.
30.
Mheshimiwa Spika, mradi huu una madhumuni ya
kuimarisha utoaji wa elimu ya msingi kwa skuli za Wilaya ya Magharibi kwa
kuongeza madarasa na samani kwa lengo la kupunguza wingi wa wanafunzi
madarasani. Mradi huu utatekelezwa na SMZ na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China . Mradi utakuwa na malengo yafuatayo:-.
i) Kujenga
skuli mbili mpya za msingi.
ii) Kukamilisha
madarasa 20 ya skuli za msingi yaliyoanzishwa na wananchi.
iii) Kununua
samani za skuli za msingi zitazojengwa
Mradi
umetengewa jumla T.Sh. 850,000,000/- za SMZ.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu ya Lazima
31.
Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa kwa
mashirikiano kati ya SMZ, Benki ya Dunia na BADEA. Mradi huu utakuwa na malengo
yafuatayo:-
i)
Kukamilisha
ujenzi wa skuli za sekondari za Kibuteni na Mkanyageni.
ii)
Kukamilisha
ujenzi wa madarasa katika skuli nne za sekondari yalizoanzishwa na wananchi.
iii) Kuchonga na kusambaza samani katika
skuli za sekondari zilizokamilishwa kujengwa.
iv) Kujenga “grills” katika vyumba vya
maabara vya skuli mpya za sekondari 16.
v)
Kukamilisha
ujenzi wa skuli za sekondari za Paje mtule, Dimani na Tunguu na kujenga ukuta
kuzunguka skuli mbili mpya za sekondari kati ya skuli zilizojengwa kwa ufadhili
wa Benki ya Dunia.
Mradi umetengewa jumla T.Sh.
1,000,000,000/- za SMZ na T.Sh. 17,647,160,000/- kutoka Benki ya Dunia na Badea.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu ya Ufundi.
32.
Mheshimiwa Spika, mradi huu utatekelezwa na SMZ
pekee. Malengo ya mradi huu ni kama ifuatavyo:-
i)
Kuanza ujenzi wa dakhalia mpya ya skuli ya sekondari
ya ufundi, Kengeja.
ii)
Kununua vifaa vya kufundishia kwa ajili ya skuli ya
sekondari ya ufundi, Kengeja na Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia.
Mradi
umetengewa jumla ya T.Sh. 500,000,000/-.
Mradi
wa Uimarishaji wa Elimu Mbadala na Amali
33.
Mheshimiwa Spika, mradi huu utatekelezwa na SMZ kwa
kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Mradi utakuwa na malengo
yafuatayo:-
i)
Kukamilisha
uandaaji wa mitaala kwa ajili ya mafunzo ya wakufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya
Utalii Zanzibar na wakufunzi wa mafunzo ya amali.
ii)
Kukamilisha
mapitio na marekebisho ya mitaala ya mafunzo kwa wanafunzi wa vituo vya Elimu Mbadala
iii)
Kuchagua
mshauri elekezi, kuandaa michoro ya ujenzi wa vituo vitatu vya elimu mbadala na
vituo viwili vya mafunzo ya amali na kutangaza zabuni za ujenzi.
iv)
Kuchagua
mshauri elekezi na kuandaa michoro ya ukarabati na utanuzi wa Taasisi ya Karume
ya Sayansi na Teknolojia, Chuo cha Utalii Maruhubi na ujenzi wa makao makuu ya
Mamlaka ya Mafunzo ya Amali. Pia kutangaza zabuni za ujenzi.
v)
Kulipa
sehemu ya fidia ya vipando kwa wananchi wa eneo la Kituo cha Mafunzo ya Kazi za
Amali, Vitongoji ambao mazao yao
yalig’olewa wakati wa ujenzi wa kituo.
Jumla ya T.Sh. 700,000,000/- za SMZ
na T.Sh. 1,529,906,000/- za AfDB zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.
Mradi
wa Uimarishaji wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar .
34.
Mheshimiwa Spika, mradi huu utatekelezwa na SMZ kwa
kushirikiana na Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Afrika (Badea) na unakusudia
kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) kwa
kukamilisha malipo ya wakandarasi wa ujenzi na wazabuni wa samani, vifaa vya
maabara na vifaa vya ICT. Pia mradi utaanza maandalizi ya awamu ya pili ya
ujenzi wa Chuo.
Mradi huu umetengewa T.Sh.
850,000,000/- za SMZ na T.Sh. 2,240,921,000/- kutoka Badea.
Mradi
wa Upanuzi na Uimarishaji wa Huduma za Maktaba.
35.
Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa na SMZ pekee
na utakuwa na lengo la kuendelea na ujenzi wa maktaba kuu, tawi la Pemba . Mradi umetengewa T.Sh. 400,000,000/- za SMZ.
Mradi
wa Ujenzi wa Vyuo vya Kiislamu:
36.
Mheshimiwa Spika, mradi huu utatekelezwa na SMZ pekee
na utakuwa na malengo yafuatayo:-
(i)
Kuendelea
na ujenzi wa uzio kuzunguka eneo la Chuo cha Kiislamu Micheweni na kuanza
maandalizi ya ujenzi wa uzio katika Chuo cha Kiislamu, Mazizini.
(ii)
Kuendeleza
ukarabati wa majengo ya Chuo cha Kiislamu Micheweni yaliyopo.
Jumla ya T.Sh.100,000,000/- za SMZ
zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha malengo hayo.
Utafiti
37.
Mheshimiwa Spika, Wizara imefanya utafiti wa
majaribio wa SACMEQ IV wenye lengo la kupima uwezo wa mwanafunzi wa msingi
katika kusoma na kufanya Hisabati. Jumla ya wanafunzi 450, walimu 50 na walimu
wakuu 15 wameshiriki utafiti huo. Taarifa za utafiti huu zinafanyiwa uchambuzi
kwa kutumia kompyuta na zimepelekwa katika Kituo cha Uratibu wa Kazi za
“SACMEQ” kilichopo katika Taasisi ya Kimataifa cha Mipango ya Elimu (IIEP) huko
Paris kwa
matayarisho ya utafiti mkuu unaotarajiwa kufanyika katika mwezi Septemba 2013.
Wizara pia imefanya utafiti wa hali ya kisomo (literacy survey) ili kubaini
maendeleo na changamoto zinazokikabili kisomo cha watu wazima. Taarifa za
utafiti huo zimefanyiwa uchambuzi na uandishi wa ripoti unaendelea.
Pia, Wizara imekamilisha uandishi wa
rasimu ya kwanza ya Ripoti ya Tathmini ya miaka 10 ya Elimu kwa Wote (EFA-End
of Decade Assessment). Uandishi wa rasimu ya mwisho unaendelea baada ya kupata
maoni ya Mshauri Elekezi kutoka UNESCO.
38.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara
imekusudia kukamilisha utafiti mkuu wa SACMEQ IV, kukamilisha uandishi wa
ripoti ya hali ya kisomo Zanzibar
pamoja na kukamilisha uandishi ripoti ya tathmini ya miaka 10 ya Elimu kwa
Wote.
Ukusanyaji
na Uchambuzi wa Taarifa za Elimu
39.
Mheshimiwa Spika, Idara inaendelea kuchambua na kutoa
takwimu za elimu zinazoonesha maendeleo ya sekta ya elimu Zanzibar kupitia Divisheni yake ya Elimu. Wizara
kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) inaendelea na zoezi
la matayarisho ya programu maalum ya uchambuzi kwa kutumia kompyuta (data base)
kwa ajili ya kurahihisha uchambuzi na utoaji wa takwimu kwa wakati. Aidha, skuli zote za msingi za serikali,
Afisi za Elimu za Wilaya na Vituo vya walimu (TCs) zitapatiwa programu hii
pamoja na kompyuta kwa ajili ya mfumo huo. Vile vile Wizara inafanya mazungumzo
na mashirika hisani ili kuwezesha mfumo huo kutumika pia katika skuli za
sekondari. Mfumo huo utazisaidia skuli kuweza kuweka kumbukumbu za mwanafunzi
mmoja mmoja pamoja na kutathmini maendeleo yao ya kielimu. Pia utaziunganisha skuli zote
na “database” iliyopo Wizarani.
Maendeleo
ya Kisera
40.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Wizara
iliandaa mpango kazi wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Elimu Zanzibar wa miaka
minne kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 hadi 2015/2016. Mpango-kazi huo
utatekelezwa kwa ushirikiano kati ya SMZ, Mashirika yasio ya kiserikali,
Jumuiya za Kimataifa.
Wizara inakusudia kuitafsiri sera ya
elimu ya mwaka 2006 kwa lugha ya Kiswahili ili kuweka mazingira mazuri ya
utekelezaji wake. Wizara pia imepanga kuwasilisha sera ya elimu ya mwaka 2006
kwa watoaji wa elimu wa skuli binafsi
ili kupata uelewa mzuri na wenye uhakika wa mfumo mpya wa elimu wa Zanzibar.
Ufuatiliaji
na Tathmini
41.
Mheshimiwa Spika, ufuatiliaji na tathmini ya
utekelezaji wa malengo ya Wizara ulifanyika katika kipindi chote cha mwaka
2012/2013. Maafisa 30 wa Wizara
walipatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo.
42.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Wizara
imepanga kuendelea na kazi za ufuatiliaji na tathmini ya mipango ya kazi mbali
mbali ya Wizara pamoja na kuandaa na kutoa ripoti za ufuatiliaji na tathmini
hizo. Wizara pia itaandaa mkutano mkubwa wa kufanya tathmini ya elimu (Joint
Education Sector Review) itayoshirikisha wadau mbali mbali wa elimu.
43.
Mheshimiwa Spika, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti
imepangiwa kutumia jumla ya T.Sh. 2,170,000,000/- kwa Unguja na T.Sh
871,000,000/- kwa Ofisi ya Pemba kwa kazi za
kawaida.
IDARA
YA UENDESHAJI NA UTUMISHI
44.
Mheshimiwa Spika, Idara hii inahusika na masuala yote
ya kiutumishi na uendeshaji, kusimamia kanuni za kazi na maslahi ya
wafanyakazi. Idara pia inahusika na
shughuli za kuratibu safari za wafanyakazi wote ndani na nje ya nchi, utunzaji
wa kumbukumbu za wafanyakazi pamoja na utunzaji wa majengo. Vile vile, Idara inaratibu
mafunzo mbali mbali ya wafanyakazi kulingana na mahitaji.
45.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, jumla ya
walimu 578 (343 Unguja, 235 Pemba ) waliajiriwa baada ya kupata kibali cha uajiri
kutoka Tume ya Utumishi Serikalini. Kati yao, walimu 200 ni wa shahada ya
kwanza, mmoja ni wa shahada ya pili, 59 ni wa stashahada ya sayansi na walimu
184 ni wa stashahada ya sanaa. Pia Wizara imepata kibali cha uajiri wa walimu
wa cheti 150 kwa ajili ya skuli za msingi katika Mikoa 4 ya Unguja na Pemba . Walimu hawa hivi sasa wanakamilisha taratibu za
ajira na wataajiriwa rasmi mara tu skuli zitakapofunguliwa katika mwezi Agosti
2013.
Katika jitihada za kuwaendeleza
watumishi wa Wizara, jumla ya wafanyakazi 821 walipatiwa fursa ya kujiunga na
masomo katika ngazi tofauti kuanzia cheti hadi shahada ya uzamivu katika vyuo
mbali mbali vya ndani na nje ya nchi.
46.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, jumla ya
wafanyakazi 110 walistaafu kazi kwa mujibu wa sheria,wafanyakazi 03 walifukuzwa
kazi kutokana na makosa mbali mbali, 04 waliacha kazi kwa hiari zao 13
walifariki dunia. Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi, Amin. Aidha
wafanyakazi 43 walipewa uhamisho kwenda kuendelea na kazi katika Wizara na
Taasisi mbali mbali za Serikali na wafanyakazi 17 walichukua likizo bila ya
malipo.
Hadi kufikia mwezi Juni, 2013, Wizara
ilikuwa na jumla ya wafanyakazi 13,677, kati yao , 8,381 ni wanawake na 5,296 ni wanaume.
Wafanyakazi 9,991 wapo Unguja (wanawake 6,542 na wanaume ni 3,449). Kwa upande
wa Pemba wapo wafanyakazi 3,686 (wanaume ni
1,847 na wanawake ni 1,839). Kati ya
wafanyakazi wote, 12,128 ni wa kada ya ualimu na 1,448 ni wafanyakazi wasiokuwa
wa kada ya ualimu.
47.
Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza juhudi za
kuwasaidia wafanyakazi wetu katika kujikwamua na matatizo ya kimaisha, Wizara
imeweza kuwadhamini wafanyakazi 457 (378 Unguja na 79 Pemba )
kupata mikopo ya fedha taslimu, vifaa vya ujenzi, vipando na vifaa vya matumizi
ya nyumbani. Wafanyakazi hawa
walifaidika na mikopo yenye thamani ya T.Sh. 706,677,397/-.
48.
Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii,
kuushukuru uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar ,
Benki ya Posta Tanzania ,
CRDB, Benki ya Barclays na Saccos zote kwa kuwapatia watumishi wa Wizara yangu
mikopo hii ya fedha taslimu na vifaa mbali mbali ili waweze kujikwamua
kimaisha. Nawaomba waendelee na utaratibu huu nasi tutatoa ushirikiano mkubwa
kufanikisha azma hii.
49.
Mheshimiwa Spika, ninafuraha kulijulisha Baraza lako
tukufu kuwa Wizara itaanza kulipa viwango vipya vya maposho kwa Wakuu wa Vyuo,
Walimu Wakuu na wasaidizi wao, Maafisa Wa Elimu wa Mikoa na Wilaya na Wakaguzi
wa Elimu kuanzia mwezi Julai 2013, baada ya kupitishwa rasmi na Wizara ya Nchi
Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Viwango hivyo vinatarajiwa
kuongeza ari, juhudi na tija katika utekelezaji wa kazi zao. Pia, katika mwaka
2013/2014, Idara itaendelea kuwapatia walimu na wafanyakazi wasiokuwa walimu
mbali mbali nafasi za masomo ili kuimarisha utendaji wa kazi zao. Pia, itatoa
mafunzo kwa maofisa utumishi wa Idara na Taasisi mbali mbali za Wizara na
walimu wakuu kuhusu sheria na kanuni za utumishi Serikalini, kuboresha
‘database’ la wafanyakazi, kukamilisha utayarishaji wa mpango mkuu wa
rasilimali watu wa Wizara, kuwapatia huduma bora na vitendea kazi wafanyakazi
ili kuimarisha utendaji kazi. Vile vile, itawapatia likizo na huduma
wafanyakazi 3,210 kwa kadiri hali ya fedha itakavyoruhusu.
50.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Idara
imepangiwa jumla ya T.Sh. 38,215,000,000/- kwa Unguja na T.Sh. 15,790,000,000/-
kwa Pemba kwa kazi za kawaida.
IDARA
YA ELIMU YA MAANDALIZI NA MSINGI
51.
Mheshimiwa Spika, Idara ya Elimu ya Maandalizi na
Msingi ina majukumu ya kusimamia utoaji wa elimu bora kwa ngazi ya maandalizi
na msingi pamoja na uratibu wa elimu katika vyuo vya Kur-ani na madrasa hapa
nchini. Aidha husimamia skuli binafsi za maandalizi na msingi ili kuhakikisha
kuwa elimu inayotolewa na skuli hizi inafuata mtaala uliokubalika na Serikali.
Pia, Idara ina jukumu la kusimamia ustawi wa huduma za wanafunzi.
Elimu
ya Madrasa na Vyuo vya Kuran
52.
Mheshimiwa Spika, Idara hii inashughulikia jumla ya
madrasa/vyuo vya Kur-ani 2,251. Aidha
zipo skuli za maandalizi za madrasa 84, Unguja na Pemba
zinazosimamiwa na kuhudumiwa kupitia Kituo cha Zanzibar Madrasa Resource Centre
(ZMRC), ambazo ufundishaji wake unafuata misingi ya dini ya kiislamu.
53.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/204, Wizara kwa
kushirikiana na Shirika la UNICEF inakusudia kutoa mafunzo kwa walimu wa
madrasa/vyuo vya Kur-ani 350, Unguja 200 na Pemba
150. Pia itaendelea kufanya ziara mbali mbali za kikazi katika madrasa na vyuo
vya Kur-ani pamoja na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili pamoja na
kushajiisha kufanya ziara za pamoja za kubadilishana uzoefu.
Elimu
ya Maandalizi
54.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, elimu ya
maandalizi ilikuwa inatolewa katika skuli 278 zilizosajiliwa, kati ya hizo
skuli 34 ni za Serikali na skuli 244 ni za binafsi. Aidha zipo skuli 41 za msingi na 21 za msingi
na kati zenye madarasa ya maandalizi na vituo 176 vya Tucheze Tujifunze (TUTU),
ambavyo vinatoa mafunzo ya maandalizi kwa njia ya redio vyenye jumla ya watoto
4,097 na wasimamizi wa vituo 360. Vituo hivi vipo katika Wilaya ya Kaskazini
‘A” na Magharibi kwa Unguja na Wilaya ya Micheweni kwa Pemba .
Vipindi hivyo vinarushwa kwa kupitia ZBC redio kwa watoto wa maandalizi na
darasa la kwanza na la pili. Kwa mwaka
2012/2013, idadi ya wanafunzi wa skuli za maandalizi imefikia 30,912 wakiwemo
wanaume 15,008 na wanawake 15,904. Jadweli namba 13(a) – (c) zinatoa ufafanuzi
zaidi.
55.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Idara
iliendelea na juhudi za kuielimisha jamii kuwapeleka watoto wenye umri wa miaka
minne kuandikishwa kwenye skuli za maandalizi.
Kazi hiyo ilifanywa kupitia mikutano na masheha, maafisa tawala wa
Mikoa, wenyeviti wa bodi za elimu za mikoa na kamati za skuli za Unguja na Pemba .
56.
Mheshimiwa Spika, Idara ilitoa mafunzo kwa walimu 201,
kati yao 115 Unguja na 95 Pemba
wanaofundisha madarasa ya maandalizi yaliyomo ndani ya skuli za msingi kuhusu
mbinu za kufundishia watoto wadogo. Pia,
walimu 30 wa skuli za maandalizi wamepatiwa mafunzo kwa ajili ya kuwaandaa kuwa
wakufunzi wa elimu ya maandalizi katika vituo vya walimu vilivyoko katika
maeneo yao .
Elimu
ya Msingi
57.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, elimu ya
msingi ilitolewa katika skuli za msingi 342 zikiwemo skuli 263 za serikali na
79 za binafsi. Idadi ya wanafunzi katika
ngazi hii ya elimu imefikia 247,353 sawa na asilimia 124.4 ikilinganishwa na
asilimia 121.5 ya mwaka 2011/2012. Aidha, watoto wote 35,703 walioandikishwa
kuanza darasa la kwanza katika skuli za Serikali wamepatiwa nafasi. Miongoni mwa watoto hao, 17,860 ni wanawake
na 17,843 ni wanaume. Jadweli namba 14 na 15 zinatoa ufafanuzi zaidi.
58.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, walimu wa
skuli za msingi walipatiwa mafunzo juu ya elimu ya mazingira, afya na huduma ya
kwanza ili kuweza kuzifanya skuli ziwe na mazingira rafiki kwa vijana,
yatakayowezesha kupatikana kwa elimu bora.
Pia, Idara imetoa mafunzo kwa walimu wa darasa la kwanza 150 (65 Pemba , 85 Unguja) wanaowapokea watoto wanaotoka
maandalizi juu ya kutumia mbinu bora za kufundisha watoto wadogo. Vile vile,
Idara imezipatia vifaa vya kufundishia na kujifunzia skuli za msingi 120 (72
Unguja na 48 Pemba ) zilizo katika mazingira
magumu zaidi ya kiuchumi.
59.
Mheshimiwa Spika, Idara kwa kushirikiana na Jumuiya
ya Lions Club imetoa mafunzo kwa walimu 30 wa ushauri nasaha skulini kwa ajili
ya kuwajengea uwezo juu ya mbinu bora za kuwashauri na kuwanasihi wanafunzi.
Vile vile, Wizara ikishirikiana na jeshi la Polisi inaendelea kutoa mafunzo juu
ya somo la usalama wetu kwanza katika skuli 10 za Wilaya ya Mjini kwa lengo la
kuwawezesha wanafunzi kuzielewa sheria mbali mbali za nchi, kutambua wajibu wao
kwa jamii, kujilinda dhidi ya vitendo vya uvunjaji wa amani na kujilinda dhidi
ya vitendo vya unyanyasaji na kuleta ustawi na maendeleo katika jamii.
60.
Mheshimiwa Spika, Idara kwa kushirikiana na Shirika
la Save the Children linaendelea na majaribio ya mradi wa adhabu mbadala katika
skuli za msingi 20 (12 Unguja na 8 Pemba ).
Mpango wa uhamasishaji jamii juu ya uimarishaji na ukuzaji wa matumizi ya
adhabu mbadala unaendelezwa katika skuli zetu za Unguja na Pemba .
61.
Mheshimiwa Spika, Idara, kwa kushirikiana na Umoja wa
Serikali za wanafunzi wa Zanzibar (USEWAZA) ilifanya ziara katika skuli mbali
mbali za Unguja kwa lengo la kutoa taaluma juu ya utendaji wa serikali
zao. Pia, USEWAZA imeandaa na kurusha
vipindi mbali mbali katika kituo cha ZBC TV vya kuelimisha jamii juu ya
maendeleo ya elimu, ushauri nasaha, nafasi ya watoto wenye ulemavu katika
jamii, mapambano dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, umuhimu wa jamii kuchangia
gharama za elimu kwa lengo la kuimarisha mazingira ya skuli na kupatikana kwa
elimu iliyobora.
62.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara
itaendelea kuzifanyia kazi changamoto mbali mbali zilizoko katika elimu hasa
uhaba wa madarasa na msongamano wa wanafunzi, ukosefu wa vitabu na uhaba wa
walimu wa baadhi ya masomo ili kuinua kiwango cha elimu katika ngazi za
maandalizi na msingi. Pia, Idara itaendelea kuhamasisha jamii kuwapeleka watoto
wao katika skuli za maandalizi na msingi, kuendelea kuzisaidia skuli zilizoko
katika mazingira magumu ya kiuchumi ili kuzipatia vifaa vya kujifunzia na
kufundishia vikiwemo madaftari, chaki, penseli, vifutio, rangi na vibao vya
kusomea kadri ya hali ya upatikanaji wa fedha itakavyoruhusu.
63.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya, kitengo cha Malaria inatarajia kutoa mafunzo
kwa walimu na wanafunzi kupitia vituo vya walimu kuhusu kuondoa malaria Unguja
na Pemba .
64.
Mheshimiwa Spika, Idara hii imepangiwa kutumia jumla ya
T.Sh. 237,945,000/- kwa Unguja na T.Sh. 81,055,000/- kwa Pemba
kwa kazi za kawaida.
IDARA
YA ELIMU YA SEKONDARI
65.
Mheshimiwa Spika, Idara ya Elimu ya Sekondari inajukumu
la kusimamia utekelezaji kazi za ufundishaji kwa ujumla na ufuatiliaji wa
utendaji kazi maskulini, kupanga walimu katika skuli zote za serikali za
sekondari na kuwapangia skuli wanafunzi waliofaulu katika ngazi mbali mbali za
elimu, shughuli za uzalishaji mali na uwekaji wa kumbukumbu za mapato na
matumizi ya skuli, kufuatilia utendaji wa serikali za wanafunzi na huduma za
dakhalia.
66.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, elimu ya
sekondari ilikuwa inatolewa katika skuli 252 kati ya hizo skuli 205 ni za
serikali na 47 ni za binafsi. Skuli hizo
zilikuwa na wanafunzi 78,956 kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita
kati yao
wanaume ni 36,162 na wanawake ni 42,794.
Katika ngazi ya elimu ya lazima (FI hadi FII) walikuwepo wanafunzi
49,977 ambao ni asilimia 84.5 ya watoto wenye umri wa miaka 14 – 15
wanaotarajiwa kuwepo skuli. Kwa upande
wa sekondari, kidato cha tatu hadi cha sita walikuwepo wanafunzi 27,139 na
michepuo (kidato 1 – 4) walikuwepo wanafunzi 4,070. Jadweli namba 17, 18 na
22 zinatoa uchambuzi zaidi
67.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Idara, imetoa mafunzo kwa walimu kuhusu miiko na
maadili katika kazi ya ualimu, mafunzo ya uongozi kwa walimu wakuu wapya pamoja
na wasaidizi walimu wakuu wapya. Pia, Idara imetoa mafunzo kuhusu utunzaji
vifaa vya maabara na kemikali na ununuzi wa vifaa kwa walimu wa sekondari wa
masomo ya sayansi kwa skuli 70 za Unguja na Pemba .
Mafunzo pia yalitolewa kwa walimu wa paneli za masomo kwa skuli 74 na
uimarishaji wa somo la Kiingereza na Hisabati kwa skuli 50 za Unguja na Pemba .
68.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara,
inakusudia kuendelea kutoa mafunzo kwa walimu wapya watakaoajiriwa pamoja na
kutoa mafunzo ya uongozi kwa walimu wakuu wapya na wasaidizi walimu wakuu
wapya. Pia, Idara inakusudia kuendelea kutoa mafunzo zaidi kwa walimu wa paneli
za masomo ya uimarishaji wa somo la Kiingereza, Hisabati na Sayansi pamoja na
utumiaji na utunzaji wa vifaa vya maabara kwa walimu wa masomo ya Sayansi.
Kazi za Ujasiriamali
69.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, shughuli za
ujasiriamali zimeendelezwa katika skuli zetu.
Skuli zetu nyingi zimeweza kukusanya mapato kutokana na miradi
iliyobuniwa ambapo fedha zinazopatikana husaidia katika kutatua matatizo madogo
madogo yanayozikabili skuli hizo.
70.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2013/2014, Idara
inakusudia kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa walimu husika na itaendelea
kuzisaidia skuli kubuni miradi ambayo itasaidia skuli hizo kuweza kujitegemea.
Serikali
za Wanafunzi
71.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa 2012/2013, Serikali
za wanafunzi katika skuli zimetekeleza majukumu yake kwa kiwango
kinachoridhisha. Serikali hizo
zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwasaidia walimu kusimamia kazi za usafi wa
mazingira ya skuli, kudumisha nidhamu za wanafunzi na kuwaandaa wanafunzi
katika kazi za uongozi baada ya kumaliza skuli.
Katika mwaka 2013/2014, Idara
inakusudia kuandaa mafunzo kwa viongozi wa serikali kwa skuli za Serikali na
binafsi ili kukuza uelewa wao.
Huduma
za Dakhalia
72.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, idadi ya
wanafunzi walioishi dakhalia ilifika 1,774, kati yao wanaume 839 na wanawake 917. Katika
kuimarisha dakhalia zetu, Idara imeupitia upya mwongozo wa kuchukua wanafunzi
watakaoishi dakhalia. Vile vile imeandaa mikakati madhubuti ya kuziendesha
dakhalia kwa ubora na uendelevu ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza wakiwa
katika mazingira mazuri na yaliyo bora. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru
wazazi wa wanafunzi wanaoishi dakhalia kwa kuendelea kuwahudumia watoto wao.
73.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Idara
imepangiwa kutumia jumla ya T.Sh. 1,706,700,000/- kwa Unguja na T.Sh. 113,300,000/-
kwa Pemba kwa kazi za kawaida.
IDARA
YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO KATIKA ELIMU
74.
Mheshimiwa Spika, Idara ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano katika Elimu huratibu na kutoa mafunzo ya TEKNOHAMA kwa watendaji
wa Wizara, kusimamia matumizi sahihi ya TEKNOHAMA katika kusoma na kufundishia
katika ngazi mbali mbali za elimu. Pia inajukumu la kutayarisha na kusimamia
programu mbali mbali za usambazaji wa
taarifa mbali mbali za elimu na kulinda usalama wa taarifa na rasilimali za
wizara kwa kutumia TEKNOHAMA.
Sera
ya ICT katika Elimu na Mpango Mkakati wake
75.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Idara iliandaa
rasimu ya Sera ya ICT katika elimu na kuanza maandalizi ya mpango mkakati wa
sera hiyo. Wadau mbali mbali wa elimu walipata fursa ya kutoa michango yao kupitia warsha na
mikutano iliyofanyika kwa nyakati tofauti.
Rasimu ya Sera hiyo itapitishwa katika vikao vya ngazi mbali mbali vya
Serikali kabla ya kutumika rasmi.
Utekelezaji
wa Mradi wa “TZ-21 Century Basic Education”.
76.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, elimu ya
msingi imeimarishwa kwa matumizi ya TEKNOHAMA chini ya mradi wa “21ST Century Basic Education” kwa kutoa
machapisho mbali mbali kwa mtindo wa “e-content”
pamoja na kuendesha mafunzo kwa walimu wa masomo ya lugha, hisabati na sayansi.
Aidha, walimu wa masomo ya lugha 1,201 wamepatiwa mafunzo juu ya “e-content”,
kati ya hao walimu 911 ni wanawake na 190 wanaume.
Kuimarisha
njia za Mawasiliano na Usambazaji wa Taarifa kupitia TEKNOHAMA.
77.
Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha njia za
mawasiliano na usambazaji wa taarifa kupitia TEKNOHAMA, Idara ilifanya
marekebisho ya tovuti ya Wizara kutokana na ile ya mwanzo kukabiliwa na
matatizo ya kiufundi na kwa muda mwingi kutokuwepo hewani. Pia yalifanyika mabadiliko ya “Hosting na Domain” mpya ya tovuti hiyo
ili kuleta ufanisi zaidi. Anuani yetu ya sasa ni www.moez.go.tz. Kwa kutumia tovuti hiyo, Wizara
imekuwa ikitoa taarifa mbali mbali zinazohusu maendeleo ya kielimu kama vile utoaji wa matokeo ya mitihani ya kidato cha
pili, darasa la saba na kidato cha nne.
Pia tovuti imetumika kutangaza zabuni, mikopo ya elimu na taarifa za
ajira kwa kadri hali inavyoruhusu. Aidha, Ofisi kuu Pemba
imefungiwa mtandao ili kuweza kuhaulisha taarifa kutoka sehemu moja kwenda
sehemu nyengine kwa urahisi zaidi.
Kuimarisha
Elimu ya Maandalizi kwa kutumia vifaa
vya ICT
78.
Mheshimiwa Spika, Idara iliandaa mafunzo ya walimu
wasaidizi wanaosimamia vituo vya utoaji wa elimu ya maandalizi kwa njia ya
redio. Jumla ya washiriki 180 wamepatiwa mafunzo ya uendeshaji wa vituo vya
Tucheze Tujifunze (TUTU), kati ya hao 91 kutoka Pemba
na 80 kutoka Unguja. Pia Idara kwa
kushirikiana na shirika la habari la Zanzibar (ZBC) inaendelea kurusha hewani
vipindi cha Tucheze Tujifunze (TUTU) na hadi kufikia mwezi wa Juni tayari
vipindi 119 vimerushwa hewani.
79.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara inakusudia
kuandaa mpango mkakati wa Sera ya ICT, kutoa mafunzo ya ICT kwa walimu 90 na
watendaji wengine 36 wa Wizara kulingana na kada zao, kuanzisha vituo 40 vya
Tucheze Tujifunze (TUTU) kwa Wilaya ya Kaskazini B, Wilaya ya Magharibi na
Wilaya ya Mkoani, kuimarisha matumizi sahihi ya TEKNOHAMA kwa ajili ya
kujifunza na kufundisha na kuimarisha njia za mawasiliano na usalama wa taarifa
kupitia TEKNOHAMA.
80.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara hii
imepangiwa kutumia T. Sh. 300,000,000/- kwa Unguja na T.Sh. 100,000,000/- kwa Pemba kwa kazi za kawaida.
IDARA YA ELIMU MBADALA NA WATU WAZIMA
81.
Mheshimiwa Spika, Idara hii inawajibu wa kuondoa
tatizo la kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa wananchi wote wa visiwa vya
Zanzibar, kuwapatia Elimu Mbadala vijana walioacha masomo njiani na wale ambao
hawakubahatika kuandikishwa kabisa na kuwaendeleza kielimu wale wote wenye nia
ya kufanya hivyo.
Kisomo
82.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Jumla ya
madarasa mapya 23 ya kisomo yamefunguliwa mjini na vijijini Unguja na Pemba . Madarasa hayo yana wanakisomo 463 wakiwemo
wanawake 411 na wanaume 52. Jumla ya wanakisomo 5,617 wamefanyiwa upimaji
katika hatua zote nne. Katika upimaji huo jumla ya wanakisomo 4,671 wakiwemo
wanawake 3,968 na wanaume 703 wamefaulu na 434 wamekombolewa.
83.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara
itaendelea na jitihada zake za kushajihisha na kuhamasisha wananchi ambao
hawajui kusoma na kuandika kujiunga katika madarasa ya kisomo hasa katika Mkoa
wa Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba ambako kuna idadi kubwa ya wananchi
wasiojua kusoma na kuandika ukilinganisha na mikoa mengine. Pia kufungua na
kuziendeleza maktaba za kisomo kwa kuzipatia nyezo stahiki.
84.
Mheshimiwa Spika, Elimu Mbadala inatolewa kwa vijana
wenye umri kati ya miaka 10 hadi 15 walioko nje ya skuli, wakiwemo walioacha
njiani kutokana na sababu mbali mbali. Idadi ya madarasa ya Elimu Mbadala ni 34
kwa Unguja na Pemba yenye jumla ya wanafunzi 839 (Pemba
376 na Unguja 463) kati ya wanafunzi hawa, wanawake ni 211 na wanaume ni 628.
85.
Mheshimiwa Spika, kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo
kina vijana 309 (wanawake 92 na wanaume 217). Wanafunzi wanaosoma katika kituo
hiki licha ya kusoma masomo ya kawaida pia wanafundishwa fani mbali mbali
zikiwemo ushoni, upishi, umeme, uchongaji na utunzaji nyumba. Kituo kimeshatoa
wahitimu 323 wa fani za umeme na uchongaji tokea kuanzishwa kwake wakiwemo
wanaume 237 na wanawake 86 ambao wametunukiwa vyeti. Wengi wa wahitimu wetu wameweza kuajiriwa
katika taasisi mbali mbali binafsi na wengine wamejiajiri wenyewe.
86.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara
inakusudia kupanua wigo wa kuhamasishaji vijana kujiunga na madarasa ya Elimu
Mbadala katika skuli za msingi na pia kuongeza wanafunzi katika Kituo cha Elimu
Mbadala, Rahaleo.
Vituo
vya Kujiendeleza
87.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka, 2012/2013, jumla ya
wanafunzi 3,522 (wanawake 1,776 na wanaume 1,745) wamesajiliwa katika vituo
mbali mbali vya kujiendeleza Unguja na Pemba .
Katika mwaka huu wanafunzi 11,396 wamefanya mitihani ya faragha wa kidato cha nne
na wanafunzi 1,935 wamefaulu, sawa na asimilia 17.0 ya watahiniwa wote.
Pia, jumla ya wanafunzi 653 wa kidato
cha sita wametahiniwa, kati yao
213 wamefaulu sawa na asilimia 32.6
88.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara itahamasisha
vijana wengi zaidi kujiunga na vituo vya kujiendeleza hasa katika maeneo ambayo
yana idadi kubwa ya vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo baada ya
mitihani yao ya
Kidato cha pili na Kidato cha nne.
89.
Mheshimiwa Spika, Idara ina jumla ya vikundi 64 vya
programu za wanawake ambavyo 44 kati ya hivyo viko Unguja na 20 Pemba . Vikundi
hivyo vina jumla ya kinamama 757 ambao wanajishughulisha na shughuli mbali
mbali za uzalishaji mali
zikiwemo kilimo, ususi na ushoni.
90.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara
inakusudia kuviimarisha zaidi vikundi hivyo kwa kuvipatia mafunzo ya ujasiriamali
na utunzaji wa fedha.
Vyombo
vya Habari
91.
Mheshimiwa Spika, vyombo vya habari ni nyenzo muhimu sana katika kuendeleza
programu za Idara. Katika mwaka
2012/2013, Idara imeweza kurusha hewani vipindi 19 vya redio kwa Unguja na 4
kwa Pemba .
Pia ilirusha hewani vipindi 5 vya Televisheni kwa Unguja na vipindi 4
kwa Pemba . Aidha Idara iliandaa makala tatu
zilizochapishwa katika gazeti la Zanzibar
leo.
92.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara
itaendelea na juhudi za kuwaelimisha wananchi na wanakisomo kwa kutumia vyombo
vya habari, vipeperushi, majarida, makongamano pamoja na kuzitumia maktaba
zilizopo mjini na vijijini ipasavyo.
93.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Idara hii
imepangiwa kutumia jumla ya T.Sh. 252,000,000/- kwa Unguja na T.Sh. 50,000,000/-
kwa Pemba kwa kazi za kawaida.
IDARA
YA MAFUNZO YA UALIMU
94.
Mheshimiwa Spika, Idara ina jukumu la kusimamia
mafunzo ya ualimu vyuoni na kazini. Mafunzo ya ualimu hutolewa katika vyuo vya
ualimu vitatu ambavyo ni Chuo cha Kiislamu Mazizini, Chuo cha Kiislamu
Micheweni na Chuo cha Benjamin William Mkapa Pemba. Vyuo hivi hutoa mafunzo ya
Stashahada ya sanaa sekondari, Stashahada ya sayansi sekondari, Stashahada ya
Ualimu Msingi, Stashahada ya Dini na Kiarabu na cheti cha ualimu wa Elimu
Mjumuisho. Kwa mwaka 2012/2013, vyuo hivyo vilikuwa na jumla ya wanafunzi 745
(wanaume 161 na wanawake 584). Kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 37 (wanawake ni
29 na wanaume 9) walichukua mafunzo ya cheti cha Ualimu wa Elimu Mjumuisho
katika Chuo cha Kiislamu Mazizini. Jadweli namba 30 (a) – (c) zinatoa ufafanuzi
zaidi.
95.
Mheshimiwa Spika, mtaala mpya wa mafunzo ya Stashahada
ya Ualimu Msingi umeanza kutumika mwaka 2012/2013. Mtaala huo umeingiza masomo
mapya yakiwemo teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA), mafunzo ya
amali, uongozi na michezo.
96.
Mheshimiwa Spika, Idara ilishirikiana na Taasisi ya
Elimu kuendesha mafunzo kwa wakufunzi wa vyuo kuhusu uelewa na matumizi ya
mtaala mpya wa Stashahada ya ualimu msingi.
Pia, UNESCO ilidhamini mafunzo kwa wakufunzi 75 Unguja na Pemba juu ya mbinu bora za ufundishaji ikiwemo
ufundishaji wa uweledi na matumizi ya TEKNOHAMA. FAWE Zanzibar iliendesha
mafunzo kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu juu ya mbinu za kufundisha kwa
kuzingatia jinsia (gender responsive
pedagogy). British Council iliendesha mafunzo maalum ya ufundishaji wa
lugha ya Kiingereza katika vyuo na skuli za sekondari kwa walimu na wakufunzi
wa lugha ya Kiingereza.
97.
Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha mafunzo ya ualimu,
wanafunzi wapya watakaojiunga na Vyuo vya ualimu watasomeshwa Kiingereza cha
mawasiliano kwa muda wa wiki nne kabla ya kuanza masomo waliyochagua. Lengo ni
kuwapa msingi wa lugha ya Kiingereza ambayo itatumika kama
lugha ya kusomeshea kuanzia darasa ya tano.
Mafunzo ya Ualimu Kazini
98.
Mheshimiwa Spika, Vituo vimeendelea kutoa mafunzo ya
ualimu kazini kwa mujibu wa mahitaji ya maeneo yao . Pia mafunzo ya ualimu kwa njia ya elimu
masafa yameendelea kutolewa katika vituo tisa ambapo jumla ya walimu 675
(wanaume 119, wanawake 556) wamemaliza mafunzo ya cheti daraja la IIIA mwezi wa
Aprili 2013.
99.
Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuimarisha
ufundishaji wa masomo ya Sayansi, walimu saba walishiriki mafunzo mbali mbali yaliyotolewa
na SMASSE huko Nairobi na walimu watatu
wameshiriki mafunzo huko Lusaka ,
Zambia .
100.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Idara imeendesha
mafunzo ya ualimu kazini. Mafunzo yaliyotolewa
ni kama ifuatavyo:-
i)
Walimu
150 wa sekondari (Unguja 100 na Pemba 50)
wamepatiwa mafunzo ya kuinua uwezo wao wa kufundisha masomo ya Hisabati na
Sayansi.
ii)
Walimu
468 (wanawake 276 na wanaume 192) wanaosomesha Kiingereza madarasa ya 5 na 6
walipata mafunzo ya kuinua lugha ya Kiingereza.
iii) Walimu 387 (wanaume 151 na wanawake
236) wanaofundisha somo la Sayansi darasa la 5 na 6 walipatiwa mafunzo ya kukuza
lugha ya Kiingereza na mawasiliano katika vituo 10 Unguja na Pemba .
iv) Walimu 1,038 wa Hisabati na Sayansi
katika skuli za msingi (Unguja 611 na Pemba
427) wamepatiwa mafunzo ya kuinua uwezo wao wa kufundisha masomo hayo.
v)
Walimu
16 walishiriki mafunzo ya lugha ya Kiingereza na mbinu za kufundisha kwa njia
ya mtandao (online study).
vi) Walimu wakuu 50 wa skuli teule za
msingi na sekondari, maafisa wa elimu wilaya 6, waratibu wa vituo 5 na mkaguzi
wa elimu 1 walipatiwa mafunzo ya siku 2 juu ya usimamizi wa mafunzo kazini.
vii) Walimu wa Kiingereza sekondari,
wakufunzi wa vyuo, wakaguzi na washauri wa lugha 232 (wanaume 152 na wanawake
80) Unguja na Pemba walishiriki mafunzo ya
kufundisha stadi ya kusikiliza kwa kutumia redio za kufundishia “life player”
(MP3).
viii) Mafunzo ya awali ya kompyuta
yalitolewa kwa washiriki 20 ambao ni walimu wakuu na wasaidizi walimu wakuu wa
skuli za Unguja.
ix) Wakufunzi wa TAP 19 (Unguja 12 na Pemba 6) walipatiwa mafunzo maalumu.
101.
Mheshimiwa Spika, Idara imechukua juhudi za
kuwaelimisha wafanyakazi wake. Wakufunzi wanane wa vyuo vya ualimu wamekwenda
masomoni, wakufunzi watano wamejiunga na masomo ya shahada ya uzamili na wawili
wamejiunga na shahada za uzamivu na mmoja shahada ya kwanza ya Elimu Mjumuisho.
Wafanyakazi wawili walipata mafunzo ya uzamili kupitia Chuo Kikuu Huria. Pia
wafanyakazi watatu wamepata mafunzo mafupi ya ufundishaji wa uongozi wa vijana,
wafanyakazi 2 wamejiunga na Chuo cha Utumishi wa Umma kwa mafunzo ya cheti, na
wafanyakazi wawili wameshiriki katika mafunzo mafupi nchini China na India .
102.
Mheshimiwa Spika, Idara inatarajia kukamilisha Sera
ya Mafunzo ya Ualimu Kazini, kutoa mafunzo kwa walimu wa Sayansi na Hisabati
kupitia mradi wa TAP na kuwafuatilia walimu wote waliopata mafunzo mbali mbali
katika mwaka uliyopita.
103.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Idara
imepangiwa kutumia jumla ya T. Sh. 250,000,000/- kwa Unguja na T.Sh.
50,000,000/- kwa Pemba .
OFISI
YA MKAGUZI MKUU WA ELIMU
104.
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu
inajukumu la kuzikagua skuli zote za Serikali na binafsi ili kufuatilia
utekelezaji wa mitaala, pamoja na kutoa mafunzo mafupi na maelekezo kwa walimu
wakuu na walimu juu ya kufanikisha kazi zao.
105.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Ofisi ya
Mkaguzi Mkuu wa Elimu ilipanga kuzikagua skuli 300 zikiwemo za Serikali na
binafsi na iliweza kukagua skuli 321.
106.
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu kwa
kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF imechapisha moduli 600 za
viwango sanifu vya elimu ya msingi na kusambazwa katika skuli za serikali na
binafsi. Vile vile, Ofisi kwa
kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida) imetayarisha moduli
ya mafunzo ya ukaguzi kwa wakaguzi wapya. Moduli hiyo ilitumika kuwapa mafunzo
mafupi wakaguzi wapya walioteuliwa na itatumika pia kwa watakaoteuliwa hapo
baadaye.
107.
Mheshimiwa Spika, Ofisi ilifanya mapitio ya mfumo ya
ukaguzi wa elimu hapa Zanzibar
kwa kukusanya maoni ya wadau mbali mbali, wakiwemo wakaguzi, wajumbe wa bodi za
elimu, kamati za skuli, waratibu wa vituo vya walimu, walimu wakuu, viongozi wa
serikali za wanafunzi. Ripoti hio itasaidia katika kuandaa muundo mpya wa
ukaguzi.
108.
Mheshimiwa Spika, Katika kujenga uwezo wa wakaguzi,
mafunzo mbali mbali yalitolewa yakiwemo mafunzo ya kompyuta na mafunzo ya
ukuzaji mitaala. Wakaguzi wanne walifanya
ziara nchini Rwanda
kujifunza na kuona mifumo mbali mbali ya ukaguzi wa skuli ambayo Rwanda
inaitumia ili kuongeza maarifa yatakayosaidia katika kurekebisha mfumo wetu wa
ukaguzi.
109.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Ofisi ya
Mkaguzi Mkuu inatarajiwa kukagua skuli 342 zikiwemo skuli 267 za serikali na 75
za binafsi. Ili kuwa na usimamizi wa ukaguzi
wa elimu wenye tija, Ofisi imelenga kuwawezesha walimu wakuu na wasaidizi
walimu wakuu kufanya ukaguzi wa skuli (School Based Inspection) uliofanisi
zaidi. Ofisi itaendelea kutoa mafunzo kwa walimu wakuu wapya, wasaidizi walimu
wakuu na baadhi ya wakuu wa seksheni juu ya usimamizi na utekelezaji wa dhamana
zao. Pia Ofisi itatayarisha muundo mpya
wa Ukaguzi pamoja na Sheria ya Ukaguzi.
110.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Ofisi ya Mkaguzi
Mkuu wa Elimu imepangiwa ruzuku ya T.Sh. 106,000,000/- kwa kazi za kawaida.
TAASISI
YA ELIMU ZANZIBAR
111.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Taasisi ya
Elimu Zanzibar, ilitoa mafunzo ya mtaala mpya wa stashahada ya ualimu kwa ngazi
ya msingi kwa wakufunzi 56 wa vyuo vya ualimu. Vile vile, Taasisi iliwasilisha
mtaala mpya wa Stashahada ya ualimu ngazi ya msingi kwa Baraza la Elimu.
112.
Mheshimiwa Spika, Taasisi iliendelea kutoa mafunzo ya
awali ya matumizi ya mihutasari mipya ya msingi kwa walimu 720 wa darasa la nne
kupitia vituo tisa vya walimu Unguja na Pemba .
Mihutasari mipya ya madarasa ya 5 na 6 na mihutasari mipya ya maandalizi
ilisambazwa kwa skuli zote za maandalizi na msingi za Unguja na Pemba . Pia, Taasisi ilifanya warsha ya uandishi wa vitabu
kwa madarasa ya kwanza hadi la sita.
113.
Mheshimiwa Spika, Taasisi ilifanya ufuatiliaji na
tathmini juu ya utekelezaji wa mihutasari ya darasa la kwanza katika skuli 72. Taasisi ilitayarisha muongozo wa kuandaa Sera
ya Ukuzaji Mitaala, Mpango wa Mafunzo kwa watumishi wa Taasisi, rasimu ya
muongozo kwa ajili ya kutathmini vitabu na rasimu ya viwango vya kujifunza kwa
elimu ya msingi kwa madarasa ya 1-4.
114.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Taasisi
itaandika, kuchapisha na kusambaza vitabu vya kiada na miongozo ya walimu wa
madarasa ya 5 na 6 kwa masomo 6 kati ya masomo 12. Pia itaandaa viwango vya
kujifunza kwa elimu ya msingi kwa madarasa ya 5 na 6. Aidha, Taasisi itaandaa
mtaala wa stashahada kwa walimu wa maandalizi na mtaala wa mafunzo kazini ya
wasaidizi wa maabara wa skuli za sekondari.
115.
Mheshimiwa Spika, Taasisi vile vile itabuni vifaa vya
kufundishia masomo ya Sayansi na Hisabati, itavifanyia uhariri vitabu vya
wanafunzi wa skuli za maandalizi pamoja na kuendesha mafunzo ya uandishi na
utunzaji wa vitabu kwa washauri wa masomo. Aidha, Taasisi itafanya utafiti juu
ya sababu ya matokeo mabaya ya mitihani kwa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa
skuli za msingi na sekondari.
116.
Mheshimiwa Spika, Taasisi inakusudia kukamilisha
Sheria ya kuanzishwa kwake na kuandaa mpango mkakati pamoja na kutayarisha
muongozo wa utaratibu wa utoaji wa elimu ya sekondari utakaokidhi mahitaji ya
Sera ya Elimu ya mwaka 2006.
117.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Taasisi
imepangiwa ruzuku ya T. Sh. 100,000,000/- kwa kazi za kawaida.
MAMLAKA
YA MAFUNZO YA AMALI
118.
Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Mafunzo ya Amali ina
majukumu ya kutoa, kusimamia na kuratibu shughuli zote za mafunzo ya amali hapa
Zanzibar .
119.
Katika
mwaka 2012/2013, jumla ya wanafunzi 784 (269 wanawake na 515 wanaume)
wanapatiwa mafunzo ya amali katika Vituo vya Mafunzo ya Amali Mkokotoni,
Vitongoji na Mwanakwerekwe. Wanafunzi hawa wanajifunza katika fani mbali mbali
za ufundi. Jadweli namba 40(a) inatoa ufafanuzi
zaidi.
120.
Mheshimiwa Spika, Mamlaka pia inaratibu shughuli mbali
mbali za maendeleo ya mafunzo ya amali ikiwemo Mitihani ya Taifa ya Uhasibu na
Biashara (NABE), mitihani ya ufundi stadi “Trade
Test” na “Competency Based Education
and Training” (CBET) inayotahiniwa na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi
(VETA) ya Tanzania Bara. Jumla ya wanafunzi 428 (102 wanawake na 326 wanaume)
walifaulu ikiwa ni sawa na asilimia 95. Wanafunzi 265 (wanawake 63) walifaulu
mitihani ya “Competency Based Education
and Training” kati ya vijana 302 (wanawake 73) waliofanya mitihani hiyo,
ikiwa ni sawa na asilimia 87.7. Jadweli namba 41 (c) na (d) zinatoa ufafanuzi
zaidi.
121.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2012/2013, Mamlaka
imeendelea kusajili vituo vinavyotoa mafunzo ya amali vya Zanzibar vya umma na binafsi. Jumla ya vituo vya amali 63 vimekaguliwa na
21 kati yao
vimesajiliwa katika hatua mbali mbali. Jadweli namba 40 (b) inatoa ufafanuzi
zaidi.
122.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Mamlaka ina
malengo makuu mawili ambayo ni kuimarisha Mamlaka ya Mafunzo ya Amali na
kuimarisha utoaji wa mafunzo ya amali. Katika kufikia malengo hayo, Mamlaka inakusudia
kuzipitia na kuzifanyia marekebisho Sera ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya 2005
na Sheria ya Mafunzo ya Amali namba 8 ya 2006 iliyofanyiwa marekebisho 2007.
Pia, inakusudia kuajiri wafanyakazi wapya, kuvipatia vituo vya mafunzo ya amali
vifaa na zana za kutendea kazi na kuongeza ujuzi na utaalamu wa walimu wake.
Aidha, Mamlaka inakusudia kuimarisha uzalishaji na uwekezaji kwa lengo la kuongeza
mapato yake.
123.
Mheshimwa Spika, Kwa mwaka 2013/2014, Mamlaka ya
Mafunzo ya Amali imepangiwa ruzuku ya T. Sh. 2,300,000,000/-.
TAASISI
ZA ELIMU YA JUU
124.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, zilikuwepo
jumla ya taasisi nne za elimu ya juu. Kati ya taasisi hizo, mbili zinamilikiwa
na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo ni
Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar na Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia na
taasisi binafsi ambazo ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani na Chuo Kikuu
cha Zanzibar .
CHUO
KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR
125.
Mheshimiwa Spika, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kimepata
mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka kumi na mbili iliyopita. Kwa sasa Chuo kina jumla ya wanafunzi 703 wa
shahada ya kwanza katika fani ya sayansi na ualimu, sanaa na ualimu na sayansi
na kompyuta. Kati yao
wanafunzi 365 ni wanaume na 338 ni wanawake. Vile vile, Chuo kina jumla ya
wanafunzi 892 katika ngazi ya Stashahada ya sayansi na ualimu, lugha na ualimu,
sayansi na kompyuta na habari na mawasiliano. Kati yao wanaume ni 340 na wanawake ni 552. Katika
mwaka wa masomo 2012/2013, Chuo pia kimeanzisha Stashahada ya kozi za jamii
ambapo wanafunzi 46 wamejiunga na kozi hiyo. Jadweli Namba 26(a) inatoa
ufafanuzi.
126.
Mheshimiwa Spika, Chuo kimefanya mabadiliko ya mfumo
wake kwa kuwa na skuli nne badala ya skuli moja na kuweka Idara na vitengo
mbali mbali. Skuli zenyewe ni Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu, Skuli ya
Elimu, Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni na Skuli ya Sayansi Asili na
Jamii. Chuo kupitia skuli ya elimu endelezi na utaalamu inatoa huduma za
kuwapatia elimu wananchi katika fani mbali mbali zikiwemo Ukutubi, Kompyuta,
Lugha ya Kiingereza na Kichina na masomo ya Benki.
127.
Mheshimiwa Spika, Chuo Kikuu cha Taifa kimeanzisha
kozi ya uzamivu ya Kiswahili (PhD) na kwa sasa wanafunzi wanane wamejiunga na
kozi hiyo. Pia, skuli inafundisha Kiswahili kwa wanafunzi wa kigeni ambapo kwa
mwaka wa masomo 2012/2013 jumla ya wanafunzi wageni 163 (wanaume 105 na
wanawake 58) wamejiunga kujifunza lugha ya Kiswahili.
128.
Mheshimiwa Spika, Chuo kilifanya mahafali yake ya
nane tarehe 22 Disemba, 2012. Katika mahafali hayo, Mkuu wa Chuo ambaye ni Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein
aliwatunuku shahada, stashahada na vyeti wahitimu 504, wanaume 233 na wanawake
261 katika fani mbali mbali. Miongoni mwao, wanafunzi 208 walitunukiwa shahada
ya sanaa na elimu, wanafunzi 46 walitunukiwa shahada ya sayansi na elimu,
wanafunzi 17 walitunukiwa shahada ya sayansi ya kompyuta. Vile vile wanafunzi
121 walitunukiwa stashahada ya mawasiliano na habari, wanafunzi 13 walitunukiwa
vyeti vya kompyuta, 23 vyeti vya ukutubi na 21 vyeti vya habari na mawasiliano.
129.
Mheshimiwa Spika, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kimehamishia
shughuli zake katika kampasi ya Tunguu. Uzinduzi wa kampasi hii ulifanywa na
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa niaba
ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi tarehe 20
Juni, 2013. Tunaishukuru Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar na BADEA
kwa michango iliyotolewa katika kufanikisha mradi huu na kukiweka Chuo katika
mazingira mazuri ya kufundishia, kujisomea na kufanyia kazi.
130.
Mheshimiwa Spika, kutokana na ushirikiano
ulioanzishwa kati ya Wizara na Wizara ya Elimu ya Juu ya Oman , Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar kimepata msaada wa ufadhili wa
masomo ya juu kupitia “Sultan Qaboos
Academic Fellowship (SQAF)”. Pia,
Wizara ya Elimu ya Juu ya Oman
imekubali kusaidia mafunzo ya walimu wa sekondari katika nyanja za Sayansi, Hisabati
na Kiingereza ambayo yataendeshwa na wataalamu wa Chuo Kikuu chetu.
131.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Chuo
kimeajiri wafanyakazi 35 kati yao 12 wanataaluma na 23 wafanyakazi wa
uendeshaji. Vile vile chuo kimeendelea kuwalipia ada za masomo wafanyakazi wake
56 ambao wapo masomoni kwa ngazi na fani tofauti.
132. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka
2013/2014, Chuo kina lengo ya kuanzisha skuli ya Tiba kwa kushirikiana na
Wizara ya Afya na wanataaluma kutoka Cuba. Pia kitaanzisha kozi mpya zikiwemo shahada
ya uzamili ya Kiswahili, shahada ya uzamili ya sayansi kemia na Stashahada ya
afya ya mazingira. Vile vile, chuo kitajenga kituo cha afya, kitafanya
ukarabati wa mkahawa na kuweka kituo kidogo cha Polisi huko Tunguu. Aidha, Chuo
kinakusudia kuyafanyia ukarabati majengo ya kampasi za Vuga na Nkrumah kwa
kuimarisha miundombinu ya maji na dakhalia za wanafunzi. Vile vile, Chuo kinakusudia kuanzisha TV
Channel (SUZA TV) kwa kutumia mfumo wa digitali kwa ajili ya kutoa elimu kwa
jamii.
133.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Chuo
kimetengewa ruzuku ya T.Sh. 4,900,000,000/- kwa kazi za kawaida
TAASISI
YA KARUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
134.
Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Karume ya Sayansi na
Teknolojia ni taasisi inayotoa huduma za kielimu za uhandisi katika ngazi ya
stashahada (NTA 6). Mafunzo ya uhandisi ambayo yanatolewa katika ngazi ya
stashahada ni uhandisi mitambo, uhandisi magari, uhandisi ujenzi na
usafirishaji, uhandisi mawasiliano ya anga, elektroniki na kompyuta na uhandisi
umeme.
135.
Mheshimiwa Spika, Taasisi ina jumla ya wafanyakazi
96, wakiwemo wakufunzi 51 (wanaume 31 na wanawake 20) na wafanyakazi wasiokuwa
wakufunzi 28 (wanaume 18 na wanawake 10). Pia kuna wafanyakazi ambao si wa
kudumu wakiwemo wakufunzi watano wa muda, wafanyakazi 10 wa mkataba na wawili
kutoka Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo.
136.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Taasisi
ilifanya usajili wa wanafunzi 272, kati yao wanaume 219 na wanawake 53 kwa
Idara zote, ambazo wanachukuwa stashahada ya uhandisi. Jadweli Namba 29 inatoa
ufafanuzi zaidi. Kwa upande wa mafunzo
ya kujiendeleza ya ufundi stadi, stashahada ya ICT, mafunzo ya Sayansi na
Hisabati kwa elimu ya msingi na kidato cha nne jumla ya wanafunzi 996 wanahudhuria
mafunzo hayo wakiwemo wanaume 798 na wanawake 198. Hali hii inafanya Taasisi ya Karume iwe na
jumla ya wanafunzi 1,215.
137.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Taasisi ilifanya
ukarabati wa miundo mbinu ya maji safi katika eneo lote la Taasisi, kukarabati
dakhalia za wanafunzi wa kike na kiume kwa kuweka vyoo vipya, wavu wa mbu na
vyandarua, kukamilisha ujenzi wa madarasa mapya matatu na ofisi mbili za
walimu. Pia, Taasisi, ilianzisha mafunzo mapya ya walimu wa Sayansi na Hisabati
ngazi ya msingi, mafunzo ya ICT, kuimarisha mafunzo ya matayarisho kwa
wanafunzi wa NTA na kuendeleza mafunzo ya amali. Pia Taasisi ilifanya tathmini
ya miaka mitano ya Taasisi juu ya utoaji wa huduma za elimu.
138.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Taasisi inakusudia
kutekeleza malengo makuu sita. Malengo hayo ni uendelezaji wa matengenezo ya
majengo ya Taasisi, kuongeza mashirikiano na Taasisi rafiki za elimu za ndani
na nje ya nchi, kuanzishwa kwa mafunzo mapya ya kuiendeleza Taasisi na yale ya
kuisaidia jamii kwa kutumia Sayansi na Teknolojia kama vile ya” business incubator” na kuwaendeleza
walimu wa Sayansi wa Sekondari, kuanzisha shughuli za utafiti, kuandaa mpango
kazi wa miaka mitatu ijayo na kufanya uhakiki wa mali za Taasisi (fixed asset valuation).
139.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Taasisi imetengewa
ruzuku ya T.Sh. 1,366,000,000/-.
CHUO
KIKUU CHA ZANZIBAR
140.
Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2012/2013, Chuo Kikuu cha
Zanzibar kilikuwa na jumla ya wanafunzi 1,297
kati yao
wanaume ni 659 na wanawake 638.
Wanafunzi 395 wanasomea shahada ya kwanza ya Sheria na Sharia, 317
Shahada ya Biashara, 333 Shahada ya Uongozi wa Umma, 132 Shahada ya Uchumi, 120
Shahada ya mawasiliano ya Kompyuta na Biashara. Pia wapo wanafunzi 554 wa
masomo ya ngazi za Diploma. Jadweli namba
28 inatoa uchambuzi zaidi. Chuo kina wahadhiri 39 wazalendo na 8 kutoka nchi za
nje. Wahadhiri wanne wazalendo wapo
masomoni katika kiwango cha shahada ya uzamivu na jitihada
zinaendelea kuwapeleka wahadhiri wengine masomoni kwa lengo la kukiwezesha chuo
kujitosheleza kwa wahadhiri wake. Wahadhiri wawili wamekamilisha masomo yao hivi karibuni na
tayari wamerejea na kuendelea na kazi.
141.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa masomo 2013/2014,
Chuo kitaanzisha mafunzo ya Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Umma na Sayansi
ya Uchumi na Fedha. Pia kinatarajia kuanza kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza
katika fani za “Islamic Banking and
Finance”, “Procurement and Logistics
Management” na “IT with Education” ili kuendana na kasi ya maendeleo ya nchi na
mahitaji ya wataalam
CHUO
KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU CHUKWANI
142.
Mheshimiwa Spika, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu
kiliopo Chukwani kinaendelea kuimarika katika kukuza taaluma na ujenzi wa
majengo mapya. Chuo kimekamilisha ujenzi wa jengo la madarasa na ofisi ya
ghorofa moja. Ujenzi wa jengo la kuishi wafanyakazi ambalo lina uwezo wa kuishi
familia sita umefikia asilimia 98 ya ukamilishaji wake.
143.
Mheshimiwa
Spika, Chuo kina jumla ya wanafunzi 1,523 wakiwemo wanawake 915 na wanaume 608.
Wanafunzi 1,328 wanasoma shahada ya kwanza ya ualimu na 195 wapo katika mafunzo
ya matayarisho (Pre-university course)
ya kujiunga na shahada ya kwanza. Jadweli Nmaba 27 inatoa ufafanuzi zaidi.
144.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa masomo 2012/2013, wanafunzi
242 wakiwemo wanawake 84 na wanaume 158 walihitimu masomo yao. Chuo kimekamilisha
taratibu mbali mbali za kukipandisha daraja ili kiwe Chuo Kikuu cha Kimataifa
cha Zanzibar (Zanzibar International University) badala ya kuwa tawi la Chuo
Kikuu cha Kimataifa kilichopo Sudan .
Taratibu zinaendelea kwa Chuo kupata kibali kutoka Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania .
145.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa masomo wa 2013/2014,
Chuo kimepanga kusajili wanafunzi 700 wa fani mbali mbali na kuajiri wahadhiri
sita ili kuondosha tatizo la kutumia wahadhiri wa muda. Pia, Chuo kimekusudia
kufanya matengenezo ya Kituo cha Afya ili kiweze kuimarisha huduma zake na
kuweka vifaa vya kisasa. Vile vile,
BODI
YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU.
146.
Mheshimiwa Spika, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
Zanzibar ni chombo kilichopewa jukumu la kuwapatia mikopo ya gharama za elimu
wanafunzi na wafanyakazi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu. Aidha Bodi hiyo
pia imepewa jukumu la kukusanya madeni kutoka kwa wanafunzi waliohitimu masomo yao kuanzia mwaka 2006 na
kuanza kazi.
147.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2012/2013,
Bodi iliwapatia mikopo wanafunzi wapya 881. Bodi pia imewalipia ada ya masomo
na posho la kujikimu wanafunzi 161 wanaoendelea na masomo katika vyuo vya nje
na wanafunzi 851 wanaoendelea na masomo kwa vyuo vya ndani ya Tanzania . Jumla ya wanafunzi waliohudumiwa
kwa mikopo kwa mwaka 2012/2013 ni 1,897. Jadweli namba 25(a) – (b) zinatoa
ufafanuzi.
148.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Bodi
inakusudia kutoa mikopo kwa vijana wapya 1,000, kati ya hao, 850 wa shahada ya
kwanza, 185 wa shahada ya uzamili na 15shahada ya tatu. Idadi hiyo ni sawa na
ongezeko la asilimia 25 ikilinganisha na wanafunzi 800 waliopangwa katika mwaka
2012/2013. Vijana 363 wanatarajiwa kumaliza masomo yao katika vyuo mbali mbali vya ndani na nje
ya nchi katika mwaka huu.
149.
Mheshimiwa Spika, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imeendelea
na kukusanya marejesho ya mikopo kutoka kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu
waliopatiwa mikopo. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013, jumla ya T. Sh.
105,167,000/- zimekusanywa kutoka kwa wanafunzi waliohitimu na kuajiriwa.
Kiwango hicho ni kikubwa ukilinganisha na makusanyo ya T.Sh. 8,200,000/-
kilichofikiwa katika mwaka 2011/2012. Katika mwaka 2013/2014, juhudi zaidi
zitachukuliwa kuongeza kasi ya marejesho ya madeni.
150.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Bodi
imepangiwa ruzuku ya T. Sh. 9,113,000,000/- kwa ajili ya udhamini wa wanafunzi
wapya na wanaoendelea pamoja na gharama za uendeshaji.
BARAZA LA MITIHANI LA ZANZIBAR.
151.
Mheshimiwa
Spika, Baraza la Mitihani la Zanzibar lina jukumu la kusimamia
shughuli zote zinazohusu mitihani ya SMZ ikiwemo utungaji, uchapishaji,
usimamizi na usahihishaji wa mitihani ya darasa la saba, kidato cha pili na
mafunzo ya Ualimu stashahada ya msingi na Dini na Kiarabu. Pia Baraza lina
jukumu la kutathmini mwenendo mzima wa malengo ya utowaji elimu pamoja na
kutathmini mwenendo wa mitihani hiyo.
152.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2012/2013, Baraza lilisimamia ufanyaji wa
mitihani ya SMZ ambapo jumla ya skuli za msingi 233 (114 Unguja, 74 Pemba)
zilifanya mitihani ya darasa la saba na skuli 188 (114 Unguja, 74 Pemba)
zilifanya mtihani wa kidato cha pili. Jumla ya wanafunzi 23,039 walifanya
mtihani wa darasa la saba katika mwezi Novemba 2012, kati yao wanafunzi 1,501
sawa na asilimia 6.5 walichaguliwa kuingia
mchepuo katika skuli mbali mbali za Zanzibar. Kwa upande wa mtihani wa kidato cha pili kati
ya wanafunzi 19,679 waliofanya mtihani wanafunzi 11,195 ikiwa ni sawa na
asilimia 56.9 walifaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo kidato cha tatu. Jadweli
namba 31 na 32 inatoa ufafanuzi zaidi.
153.
Mheshimwa
Spika, kwa upande wa mtihani ya Taifa wa kidato cha nne, kati
ya wanafunzi 13,051 wa skuli za Serikali na binafsi waliofanya mtihani huo
mwezi wa Oktoba 2012, wanafunzi 6,935 wamefaulu ikiwa ni sawa na asilimia 53.1.
Kiwango cha ufaulu kwa kidato cha nne kimeshuka ikilinganishwa na matokeo ya
2011 ambapo asilimia ya ufaulu ilikuwa 75.9. Aidha, kati ya wanafunzi
waliofaulu, wanafunzi 1,054 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika
skuli za Serikali mwaka 2013/2014, wakiwemo 719 kutoka skuli za Serikali, 60 wa skuli za binafsi na 275 wanafunzi
wa faragha. Jadweli namba 22 inatoa ufafanuzi zaidi.
154.
Mheshimiwa
Spika, kati ya wanafunzi 2,067 waliofanya mtihani wa kidato
cha sita mwezi Februari 2013, wanafunzi 1,636 sawa na asilimia 79.1 walifaulu.
Kiwango hiki cha ufaulu kimepanda ikilinganishwa na matokeo ya Februari 2012
ambapo asilimia ya ufaulu ilikuwa 74.0. Jadweli namba 6 (c) iii inatoa
ufafanuzi zaidi.
155.
Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa
mitihani ya Ualimu ya Juni 2012, kati ya wanafunzi 68 waliofanya mtihani wa
marudio ya Stashahada ya Ualimu Dini ya
Kiarabu na Stashahada ya msingi katika Chuo cha Kiislamu Mazizini, Chuo cha
Kiislamu Kiuyu Micheweni na Benjamin William Mkapa, wanafunzi 54 sawa na
asilimia 79.4% walifaulu na wanafunzi 14 hawakufaulu mitihani yao. Jumla ya wanafunzi 110 wamefanya mitihani ya
ualimu ngazi ya Stashahada ya
Sekondari ya Baraza la Mitihani la
Tanzania mwezi wa Mei 2013 na wanafunzi 263 wamefanya mitihani ya ualimu ya Stashahada
ya Msingi na Dini na Kiarabu ya Baraza
mwezi Juni, 2013.
156.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2013/14, Baraza limepanga kufanya tathmini
ya mtaala mpya wa elimu ya msingi ambapo wanafunzi wa darasa la nne watafanyiwa
mtihani wa pamoja ili kujua ufanisi wa mtaala husika. Katika kufanikisha
shughuli hii Baraza litaandaa mitihani ya masomo ya Hisabati, Kiingereza,
Kiswahili, Sayansi na Elimu jamii. Stadi zitakazopimwa kwenye tathmini hii ni kuangalia kwa
kiasi gani mwanafunzi anaweza kusoma, kuandika na kuhesabu.
157.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2013/2014, Baraza limekusudia kuimarisha
taratibu za usimamizi wa mitihani ya SMZ, ikiwemo kuendelea kuweka kumbukumbu
zote za wanaotarajiwa kufanya mtihani katika mfumo wa kompyuta na kuongeza
udhibiti wa mitihani hiyo. Pia, Baraza litakamilisha kanuni na miongozo ya uendeshaji wa mitihani kwa
mujibu wa Sheria ya Baraza.
158.
Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Baraza limetengewa ruzuku
ya T.Sh. 1, 570, 000,000/- kwa kazi za kawaida.
BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA
159.
Mheshimiwa
Spika, Bodi ya Huduma za Maktaba ni chombo kinachotekeleza
majukumu yake kupitia Shirika la Huduma za Maktaba. Chombo hiki kina jukumu la kuanzisha,
kusimamia na kusambaza huduma za maktaba Unguja na Pemba.
160.
Mheshimiwa
Spika, Shirika linaendelea kushajiisha na kutoa ushauri juu ya
kuanzisha maktaba katika maeneo mbali mbali yakiwemo maeneo ya skuli na maeneo
ambayo jamii zinaishi. Katika mwaka 2012/2013, skuli zilizomo katika mradi wa
maktaba za sanduku zimeongezeka kufikia 35 kutoka skuli 25 mwaka 2011/2012. Katika
mwaka 2013/2014, Shirika linategemea kuongeza skuli 20 nyengine zitakazoingia
katika mradi wa maktaba za sanduku.
161.
Mheshimiwa
Spika, Shirika kwa kushirikiana na jumuiya isiyo ya kiserikali
MJUKIZA limeanzisha utaratibu wa kuwa na maktaba za jamii. Maktaba hizi zinasaidia sana kutoa huduma kwa
jamii kwa ukaribu zaidi. Hadi hivi sasa,
ziko maktaba 8 za jamii katika maeneo ya Chumbuni, Welezo, Kiembesamaki, Mpapa,
Uzini, Fumba, Bweleo na Tumbatu. Aidha, Shirika linaendelea kugawa vitabu vya
kiada na ziada katika taasisi mbali mbali za elimu zikiwemo skuli za msingi,
sekondari, vyuo na vituo vya walimu.
162.
Mheshimiwa
Spika, katika jitihada za kuwasaidia watoto kuandika, kusoma
na kujifunza, Shirika linaendesha programu ya watoto ndani ya Maktaba Kuu ya
Maisara Unguja na Maktaba Kuu ya Chachani Chake chake Pemba. Aidha, programu hii huendeshwa katika skuli
husika, hususan kwa skuli ambazo ziko nje ya mji. Idadi ya wanachama imekuwa ikiongezeka siku
hadi siku. Kwa mwaka 2012/2013 idadi imefikia 18,360, kati yao 17,391 kwa
Unguja na 969 kwa Pemba .Kwa mwaka 2013/2014 Shirika linatarajia kuendesha
programu 80 nchini kote.
163.
Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka 2013/2014, Shirika limetengewa ruzuku ya T.Sh. 400, 000,000/- kwa kazi za kawaida.
KITENGO CHA UHASIBU
164.
Mheshimiwa
Spika. Kitengo kimesimamia ulipaji wa mishahara ya wafanyakazi
wote wa Wizara pamoja na mahitaji mengine ya Wizara. Kwa upande wa fedha za maendeleo, Kitengo
kimesimamia ulipaji wa fedha za wakandarasi na wazabuni wa ujenzi na wazabuni
wa vifaa na huduma mbali mbali. Kitengo kimekuwa na mashirikiano mazuri na Ofisi
ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo katika matumizi ya mtambo wa
IFMS ambao husaidia kwa kiwango kikubwa usimamizi wa matumizi kwa mujibu
wa bajeti ya Wizara na hivyo kuimarisha udhibiti wa fedha za umma.
165.
Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka 2013/2014, Kitengo kitaendelea kusimamia
matumizi yote ya fedha za kawaida na fedha za maendeleo kwa mujibu wa bajeti iliyotengwa. Aidha, Kitengo
kinakusudia kutoa mafunzo kwa wahasibu na wakuu wa vitengo kuhusu usimamizi wa
fedha. Kitengo pia kitatoa mafunzo kwa wakurugenzi na maofisa mipango wa Idara
zote za Wizara juu ya utayarishaji wa bajeti kwa mfumo wa “Medium Term Expenditure Framework” na Program Based Budgeting.”
Kwa mwaka
2013/2014, Kitengo kimepangiwa kutumia jumla ya T.Sh. 66, 000,000/- kwa kazi za
kawaida.
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA
UHUSIANO
166.
Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka 2012/2013, Kitengo cha Habari Elimu na
Mahusiano kiliendelea kutekeleza majukumu ya kuratibu shughuli za utoaji habari
za Wizara na mahusiano ya Wizara na taasisi na nchi mbali mbali katika nyanja
ya elimu. Miongoni mwa shughuli zilizotekelezwa katika kukuza na kuimarisha
mashirikiano na nchi mbali mbali ni kukutana na mabalozi wa nchi za nje waliopo
Tanzania pamoja na kuhudhuria mikutano na makongamano ya kimataifa.
167.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2012/2013 niliweza kukutana na na kufanya
mazungumzo na mabalozi wa Nigeria, Misri, India, Iran, Sudan, China, Uingereza
na Cuba. Kwa upande wa
mashirika ya Kimataifa ni USAID, UNICEF, UNESCO na Global Partnership for Education (GPE). Aidha, nilihudhuria
mikutano na makongamano mbali mbali, miongoni mwao ni “Education World Forum” huko London Uingereza na Mkutano wa Mawaziri
wa Elimu wa Nchi za Jumuiya ya Madola huko Mauritius . Pia, nilitembelewa na
Mheshimiwa Dk. Rawya Saud Al-Busaidi, Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman ambae alifanya ziara
ya siku sita hapa Zanzibar .
Katika ziara hiyo tumeweza kuzungumzia utelezaji wa mkataba wa maelewano baina
ya pande zetu uliotiwa saini mwaka 2012 nchini Oman
wakati wa ziara ya Mheshimiwa Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
pamoja na kuzindua mradi wa utoaji mafunzo wa SQAF. Pia niliweza kukutana na Mheshimiwa
Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Tanzania Bara na
kujadiliana masuala mbali mbali ya kuendeleza elimu katika sehemu zetu mbili za
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Napenda kumshukuru sana
kwa mashirikiano makubwa anayonipa.
168.
Mheshimiwa Spika, Kitengo kimeweza kutangaza maendeleo
ya Wizara kwa kupitia vyombo vya habari vya hapa nchini, pia kimeandaa kipindi
cha kusheherekea miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Vile vile kwa kushirikiana na BBC Swahili tumeweza kurusha kipindi cha kwanza
cha TV kiitwacho Haba na Haba.
169.
Kwa
mwaka wa 2013/2014, Kitengo kitaendelea kuratibu mashirikiano na kutoa habari
za maendeleo ya Wizara pamoja na kutayarisha programu maalum ya miaka 50 ya
maendeleo ya elimu Zanzibar .
Katika mwaka wa 2013/2014, Kitengo
kinatarajia kutumia jumla ya T.Sh. 50,000,000/- kwa kazi za kawaida.
KITENGO
CHA UNUNUZI NA UGAVI
170.
Mheshimiwa Spika, Kitengo cha Ununuzi na Ugavi kimeendelea
kufanya kazi zake vizuri. Katika mwaka
2012/2013, Kitengo kwa kushirikiana na Bodi ya Zabuni ya Wizara kilitayarisha,
kutangaza na kuzifanyia tathmini jumla ya zabuni 39 za manunuzi ya bidhaa,
huduma na kazi za ujenzi zenye thamani ya jumla ya T.Sh. 14,089,000,000/-.
171.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Kitengo
kinakusudia kutayarisha, kutangaza na kuzifanyia tathmini zabuni za ujenzi na
ununuzi wa vifaa. Pia kitengo kitatangaza zabuni za kutafuta washauri elekezi
kwa kazi mbali mbali za Wizara.
Katika mwaka 2013/2014, Kitengo
kinatarajia kutumia jumla ya T.Sh. 55,000,000/- kwa kazi za kawaida.
KITENGO
CHA UKAGUZI WA HESABU ZA NDANI
172.
Mheshimiwa Spika, Kitengo hiki kina jukumu la kukagua
hesabu zinazohusiana na matumizi pamoja na mapato katika Taasisi na Idara zote
za Wizara. Kitengo pia kinafanya ukaguzi
wa kuangalia michango yote inayotolewa na wazee na wanafunzi kwa skuli zote za
Unguja na Pemba . Kwa mwaka 2012/2013, Kitengo
kimeweza kukagua hesabu zote za fedha za kawaida na fedha za maendeleo kuanzia
Makao Makuu ya Wizara pamoja na kufuatilia vifaa vilivyopelekwa katika skuli
mbali mbali ambavyo hununuliwa kutokana na bajeti husika ya mwaka wa fedha na
pia fedha za miradi ya maendeleo kulingana na thamani halisi ya bidhaa
zilizopokelewa na ujenzi uliofanyika.
173.
Mheshimiwa Spika, Kitengo kimeweza kuzifanyia ukaguzi
skuli 194 zikiwemo 120 za Unguja na 74 za Pemba .
Pia Kitengo kimefanya ukaguzi wa Taasisi tano ambazo hupatiwa ruzuku. Taasisi
hizo ni Shirika la Huduma za Maktaba, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar , Mamlaka ya
Mafunzo ya Amali, Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia na Taasisi ya
Elimu Zanzibar. Kitengo i pia kilifanya
ukaguzi katika Ofisi ya Wizara Pemba. Aidha, Kitengo kinaratibu vikao vya
kamati ya ukaguzi wa hesabu za ndani (Audit
Committee) ambayo hupokea na kujadili ripoti za ukaguzi kwa kila robo
mwaka.
174.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Kitengo kitaendelea
kufanya ukaguzi wa mahesabu ya Taasisi na Idara zote za Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali pamoja na Taasisi na skuli zake mbali mbali za Unguja na Pemba . Pia kitengo kitaendelea na utaratibu wake wa kutoa
mafunzo ya uwekaji wa kumbukumbu za hesabu na uwekaji wa rekodi za vitabu
kwa wenyeviti wa kamati za skuli, walimu
wakuu wa skuli pamoja na washika fedha wa skuli ili kuwajengea uelewa kuhusiana
na kazi zao. Pia, Kitengo kitakagua
jumla ya skuli 200.
Katika mwaka 2013/2014, Kitengo
kinatarajia kutumia jumla ya T.Sh. 60,000,000/- kwa ajili ya kazi za kawaida.
KITENGO
CHA URATIBU WA ELIMU YA JUU
175.
Mheshimiwa Spika, Kitengo hiki kiliendelea na jukumu
lake la kuratibu maendeleo ya elimu ya juu na kuwa na mashirikiano ya karibu na
Idara ya Elimu ya Juu ya Tanzania Bara na taasisi nyengine za elimu ya juu.
Katika mwaka 2012/2013, Kitengo kimetangaza nafasi za masomo kutoka nchi za Oman , Jumuiya ya Madola ,
China , Egypt , Cuba ,
Russia , Misri na Algeria . Jumla ya wanafunzi 20 wamewasilisha maombi ya
masomo nchini Oman, wanafunzi 3 Jumuiya ya Madola, wanafunzi 20 nchini China,
Algeria 15, Cuba 9, Russia 2 na Misri 2.
Aidha, Kitengo kimeweka kumbukumbu za
wahitimu wanaorejea masomoni. Jumla ya wanafunzi 536 waliomaliza masomo katika fani
mbali mbali wameripoti wakiwemo wanaume 286 na wanawake 250. Wahitimu hao
wamepelekwa Tume ya Utumishi kwa ajili ya kutafutiwa ajira.
176.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Kitengo
kinatarajia kufanya mikutano na Taasisi mbali mbali za elimu ya juu ili
kujadili maendeleo ya mipango ya Taasisi hizo, kuendelea kuratibu nafasi za
masomo ndani na nje ya nchi na kuweka kumbukumbu za wahitimu wanaorudi
masomoni.
177.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Kitengo
kimepangiwa jumla ya T.Sh. 50,000,000/- kwa kazi za kawaida.
KITENGO
CHA ELIMU MJUMUISHO NA STADI ZA MAISHA
178.
Mheshimiwa Spika, Kitengo cha Elimu Mjumuisho na
Stadi za Maisha kimepewa dhamana ya kusimamia na kuhakikisha kwamba lengo la
Elimu kwa Wote linafikiwa kwa watoto wote kupata haki yao ya msingi ya
elimu wakiwemo wenye mahitaji maalum, kutoa ushauri nasaha,
kusimamia mapambano dhidi ya UKIMWI na madawa ya kulevya na kuwapatia stadi za
maisha walimu na wanafunzi.
Elimu
Mjumuisho
179.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2012/2013, Kitengo kilitoa
mafunzo mbali mbali kwa walimu wa skuli ili waweze kuwafundisha wanafunzi wenye
mahitaji maalum katika madarasa ya kawaida kwa ufanisi. Miongoni mwa mafunzo hayo ni ya maandishi ya
nukta nundu, lugha ya alama na mbinu mbali mbali za urekebishaji wa tabia za
wanafunzi. Jumla ya walimu 689 wa Unguja
na Pemba walifaidika na mafunzo yaliyotolewa.
Aidha, mafunzo ya elimu mjumuisho yalitolewa kwa walimu 176 wa skuli binafsi za
Unguja.
180.
Mheshimiwa Spika, Kitengo kilishirikiana na Kitengo
cha Elimu Maalum cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi cha Tanzania Bara
katika kutafsiri kivunge (Toolkit)
cha moduli sita ambacho kiliandaliwa na UNESCO kwa matumizi ya nchi za
Mashariki ya mbali. “Tool-kit” hiyo, ilifanyiwa marekebisho
ili iendane na mazingira ya Tanzania
na iweze kutumika katika kuandaa mazingira rafiki ya ufundishaji na
ujifunzaji. Pia, Kitengo kimefanya
ufuatiliaji wa skuli zinazotekeleza programu ya elimu mjumuisho kwa lengo la
kutathmini utekelezaji wake. Jumla ya skuli 35 (26 za Unguja na skuli 9 za Pemba ) zilihusika na ufuatiliaji huo.
181.
Mheshimiwa Spika, katika kuhamasisha na kuelimisha
jamii katika suala zima la elimu mjumuisho, vipindi kumi vya radio vilirushwa
kupitia Shirika la Utangazaji la Zanzibar
ambapo wananchi walipata fursa ya kuchangia kuhusu maendeleo ya elimu mjumuisho
katika skuli zetu. Aidha, Kitengo
kimefanya utafiti wa kupata takwimu za wanafunzi wenye mahitaji mbali mbali ya
kielimu, wakiwemo wenye ulemavu katika skuli 334 za Serikali za Unguja na Pemba kati ya skuli zote 420. Jumla ya wanafunzi 73,241
wamegunduliwa kuwa na mahitaji maalumu, miongoni mwao 37,152 wa kike na 36,089
wa kiume.
182.
Mheshimiwa Spika, Kitengo kinaendelea kuwapatia
mafunzo watendaji wake ili kuwajengea uwezo zaidi katika utendaji wa kazi zao.
Watendaji wawili na mwalimu mmoja wanaendelea na masomo ya shahada ya kwanza katika
Chuo Kikuu cha Kampala Uganda . Aidha walimu wawili pia
wanaendelea na masomo ya shahada ya kwanza ya fani ya elimu mjumuisho katika ‘Sebastian Kolowa
Memorial University ’, huko Lushoto Tanga.
Ushauri
Nasaha
183.
Mheshimiwa Spika, Kitengo kimefanya utafiti juu ya
idadi ya walimu washauri waliopata mafunzo ya ushauri nasaha kwa upande wa
Unguja. Kati ya walimu wote wa ushauri nasaha 350 (175 wanawake na 175 wanaume)
ni walimu washauri 119 tu ndio waliopatiwa mafunzo (59 wanaume na 60 wanawake).
Utafiti kama huo unatarajiwa kufanyika Pemba
katika mwaka 2013/2014.
184.
Mheshimiwa Spika, Kitengo kilifuatilia kesi 11 za udhalilishwaji wa wanafunzi na kwa
kushirikana na Idara ya Ustawi wa Jamii ilitoa mafunzo kwa wanafunzi wa skuli
walizotoka juu ya namna ya kujikinga na matokeo ya udhalilishaji na kuweza
kutoa taarifa pindi tatizo linapotokezea. Mafunzo kama hayo yataendelea
kutolewa katika skuli nyengine.
Mapambano
Dhidi ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya
185.
Mheshimiwa Spika, katika mapambano dhidi ya UKIMWI na
madawa ya kulevya, Kitengo kimetoa mafunzo ya stadi za maisha kwa walimu 140
(walimu 80 Unguja na 60 Pemba ). Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha walimu
kusimamia vyema shughuli za stadi za maisha katika klabu za afya za skuli. Aidha mafunzo mengine yalitolewa kwa
wanafunzi 300 (180 Unguja na 120 Pemba ).
Masuala
ya Jinsia
186.
Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha masuala ya
kijinsia, Kitengo kilishirikiana na FAWE Zanzibar kutoa mafunzo kwa walimu 40
(wanawake 22 na wanaume 18) kutoka katika skuli mbali mbali za Unguja na Pemba.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha walimu kuelewa mbinu mbali mbali za
ufundishaji kwa muitikio wa jinsia (gender
responsive pedagogy) na kuwapa ujuzi wakufunzi wa vyuo vya ualimu ili
waweze kutoa mafunzo kwa walimu wanafunzi juu ya ufundishaji kwa kuzingatia
muitikio wa kijinsia.
187.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Kitengo kitaendeleza masuala ya elimu
mjumuisho na stadi za maisha kutoa
mafunzo ya mbinu za ufundishaji katika elimu mjumuisho kwa walimu zaidi,
kuhamasisha jamii kuhusu haki ya elimu kwa watoto wote hasa wale wenye mahitaji
maalum, kutoa mafunzo ya stadi za maisha kwa walimu na wanafunzi ili waweze
kupambana na changamoto mbali mbali, kufanya utafiti kwa skuli 86, kutoa
mafunzo kwa walimu washauri nasaha na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Kitengo.
Kwa mwaka 2013/2014, Kitengo
kimepangiwa kutumia jumla ya T. Sh. 99,000,000/- kwa kazi za kawaida.
KITENGO
CHA URAJIS
Baraza
la Elimu
188.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Baraza la
Elimu lilifanya kikao kimoja ambacho wajumbe walijadili na kupitisha ada mpya
za leseni za walimu na usajili wa skuli za binafsi. Pia, wajumbe wapya walielimishwa kuhusu Sera
ya Elimu ya 2006 na Sheria ya Elimu pamoja na kupitia mtaala mpya wa Stashahada
ya Ualimu ya Msingi.
Leseni
za Walimu
189.
Mheshimiwa Spika, jumla ya walimu 383 walipatiwa
leseni za kusomeshea. Kati ya walimu hao 251 waliosomea na 132 wasiosomea. Pia,
maofisa wa Kitengo walitembelea skuli za serikali 47 na binafsi 39 kuhakiki na
kukagua leseni za walimu, usajili wa skuli, sera, sheria, kanuni na miongozo ya
kazi na mambo mengine yanayohusu skuli.
Vile vile, Kitengo kinaendelea kushirikiana na wakaguzi wa elimu katika kukagua
skuli za binafsi na Serikali ili kufuatilia utekelezaji wa kazi.
Maombi
ya Usajili wa Skuli za Serikali na Binafsi
190.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Wizara
ilisajili skuli 29 za Serikali na skuli 20 za Binafsi. Katika mwaka 2013/2014,
Ofisi ya Mrajis wa Elimu itaendelea kushughulikia maombi ya usajili wa skuli na
leseni za walimu kutoka skuli zote za serikali na binafsi.
Kesi
za Ujauzito na Ndoa za Wanafunzi
191.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, kesi 18 za
ujauzito wa wanafunzi ziliripotiwa, ambapo kesi moja ilikuwa ya mwanafunzi kwa
mwanafunzi. Kesi 4 kati ya hizo zilijadiliwa na wanafunzi watatu walikubali
kuendelea na masomo.
192.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki kesi 23 za ndoa
za wanafunzi ziliripotiwa na kati ya kesi hizi moja ilikua baina ya mwanafunzi
kwa mwanafunzi. Kwa mujibu wa Sheria ya Elimu namba 6 ya mwaka 1982 kifungu cha
20 (3), wanafunzi 23 wa kike na mwanafunzi mmoja wa kiume walifukuzwa
skuli. Katika mwaka 2013/2014, Kitengo
cha Urajis kitaendelea kushughulikia kesi za ujauzito na ndoa na pia kuwapatia
elimu juu ya umuhimu wa elimu kwa wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa skuli.
Kwa mwaka 2013/2014 Kitengo
kimepangiwa jumla ya T.Sh. 60,000,000/- kwa kazi za kawaida.
KITENGO
CHA MICHEZO NA UTAMADUNI
193.
Mheshimiwa Spika, Kitengo cha Michezo na Utamaduni
kimeundwa ili kusaidia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya michezo Zanzibar ndani ya skuli na
kukuza vipaji vya watoto ili kupata wanamichezo bora.
194.
Mheshimiwa Spika, katika kufufua vugu vugu la michezo
lililokuwepo zamani katika skuli zetu zote sambamba na kuhamasisha vijana
katika shughuli za michezo, Wizara yangu imeshirikiana kwa karibu sana na Wizara ya Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo. Mikutano mbali mbali imeandaliwa baina ya
viongozi wa Wizara hizi mbili ili kupanga mikakati ya pamoja katika kuinua
michezo katika skuli. Katika kuendeleza ushirikiano huo, Baraza la Michezo la Zanzibar , limeipatia
Wizara yangu mipira 20,000 kwa ajili ya kuendeleza michezo ya mpira wa miguu na
netboli kwa skuli zote za Serikali na binafsi. Napenda kutoa shukrani zangu za
dhati kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo na Baraza la Michezo
la Zanzibar kwa
msaada huo na mashirikiano makubwa na Wizara yangu. Kitengo kiliandaa
mashindano ya riadha kwa mbio za nyika (cross
country) kwa wanafunzi wa skuli za sekondari na msingi ambapo jumla ya
wanafunzi 400 walishiriki. Mbio hizi za
“Elimu cross country”
zilizoshirikisha pia, wanafunzi kutoka skuli ya Filbert Bai ya Kibaha. Kitengo
kinakusudia kuyaendeleza mashindano ya “Elimu
cross country “kila mwaka na kuzishirikisha skuli zaidi kutoka nje ya Zanzibar ili kuleta hamasa
kubwa zaidi.
195.
Mheshimiwa Spika, timu zetu zilishiriki katika
mashindano ya UMISSETA huko Kibaha Tanzania Bara. Timu zilizoshiriki ni mpira wa miguu (wanaume
na wanawake), mpira wa kikapu, mpira wa wavu, netiboli, mpira wa mikono,
riadha, mpira wa meza na bao. Katika mashindano hayo, tumeweza kuwa mshindi wa
kwanza katika mpira wa kikapu na mchezo wa bao, mshindi wa pili katika mpira wa
miguu na mpira wa mikono na mshindi wa tano katika riadha. Zanzibar imekuwa watano kati ya kanda kumi na
mbili zilizoshiriki.
196.
Mheshimiwa Spika, Kitengo kimeendelea kutoa mafunzo
mbali mbali ya michezo kwa kushirikiana na taasisi nyengine zinazojishughulisha
na michezo hapa Zanzibar na Tanzania kwa jumla. Kwa
kushirikiana na “British Council”
kupitia mradi wake wa “International
Inspiration” ilitoa mafunzo kwa walimu 90 kutoka skuli mbali mbali za
Unguja kwa michezo ya mpira wa wavu (30), riadha (30) na mpira wa miguu kwa
wanawake (30). Mradi huo unaotekelezwa hivi sasa katika Mkoa wa Mjini Magharibi
katika skuli ya Regezamwendo, Langoni na SOS utakuwa wa miaka mitatu ambao
umekuja kufuatia nchi ya Uingereza kuteuliwa kuandaa michezo ya Olimpiki mwaka
2012. Kabla ya kuteuliwa kwake Uingereza iliahidi kutoa mafunzo kwa wanamichezo
millioni 23 katika kipindi cha miaka mitatu duniani.
197.
Mheshimiwa Spika, Kitengo pia kiliendelea kutoa
mafunzo kwa walimu wa skuli za msingi wanaofundisha somo la michezo kwa darasa
la kwanza na la pili katika Wilaya za Mkoani na Micheweni ili kupata wataalamu
na wanamichezo bora wenye uelewa wa masuala ya
michezo. Jumla ya walimu 60 wa
madarasa hayo walipatiwa mafunzo ambayo yatawasaidia kupata mbinu mbali mbali
za kufundisha somo la michezo kwa ufanisi.
198.
Mheshimwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Kitengo kina
lengo la kuendelea kuwapatia taaluma ya michezo walimu wa fani mbali mbali za
michezo katika skuli zetu za Unguja na Pemba
kwa kushirikiana na taasisi nyengine za michezo ndani na nje ya nchi yetu
kadiri hali ya kifedha itakavyoruhusu. Pia, Wizara itaendelaea kuandaa
mashindano ya michezo maskuli na kushiriki katika michezo itakayoandaliwa na
umoja wa michezo na sanaa skuli za sekondari Tanzania (UMISSETA) na na
Shirikisho la Michezo ya skuli za sekondari Afrika ya Mashariki (FEASSSA) kwa
lengo la kuibua, kuinua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wetu na kuitangaza
Zanzibar kupitia midani za michezo nje
ya mipaka yake.
Kwa mwaka 2013/2014, Kitengo
kimepangiwa jumla ya T.Sh. 120,000,000/- kwa kazi za kawaida.
MAPATO
199.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Amali ilikadiriwa kukusanya T.Sh. 22,500,000/- kutoka
vianzio vya ada za leseni za walimu pamoja na uandikishaji wa skuli binafsi.
Hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2013, jumla ya T.Sh. 30,192,900/- zilikusanywa na
kuwasilishwa ikiwa sawa na asilimia 134.2 ya makadirio. Kuongezeka kwa makusanyo kunatokana na mabadiliko
ya ada ya leseni na usajili wa skuli binafsi na kupatiwa leseni walimu wapya.
Katika mwaka 2013/2014, Wizara inakusudia kukusanya jumla ya T.Sh. 15,000,000/-
ikiwa ni mapato ya usajili wa skuli za binafsi na leseni za walimu na
kuziwasilisha Hazina.
SHUKRANI
200.
Mheshimiwa
Spika, napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa washirika
wote wa sekta ya elimu wakiwemo wananchi, nchi wahisani na mashirika ya misaada
ya kimataifa kwa kutuunga mkono katika jitihada zetu za kuendeleza elimu.
Napenda kutoa shukrani zetu za pekee kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China , Serikali ya Oman ,
Serikali ya India , Serikali
ya Nigeria , Serikali ya
Marekani, Sweden
na Uingereza. Pia, napenda kuyashukuru mashirika mbali mbali yakiwemo Sida,
British Council, USAID, UNICEF, UNESCO, GPE, VSO, Peace Corps, JICA na KOICA.
Pia shukrani zetu ziende kwa Aga Khan Foundation, Benki ya Dunia, Benki ya
Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika na Benki ya Maendeleo ya Afrika. Pia napenda
kuyashukuru mashirika yasio ya kiserikali ya FAWE, Takotof, Save the Children
Fund, Sazani Associates na Book Aids International.
JUMLA
YA GHARAMA ZA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI.
201.
Mheshimiwa Spika, ili Wizara yangu iweze kutekeleza
majukumu yake iliyojipangia katika mwaka wa fedha 2013/2014 kwa ufanisi,
naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe matumizi ya jumla ya T.Sh.
115,747,619,000/-. Kati ya fedha hizo T.Sh. 80,200,000,000/- ni kwa matumizi ya
kawaida, T.Sh. 5,350,000,000/- za SMZ na T.Sh. 30,197,619,000/- za washirika wa
maendeleo kwa matumizi ya miradi ya maendeleo. Jadweli namba 46 na 47 zinatoa
uchambuzi.
Mheshimiwa Spika,
naomba kutoa hoja.
KIAMBATISHO
(Takwimu za Maendeleo ya
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Kwa Kipindi cha 2008 - 2013 na Hali
Halisi ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa Mwaka
2013)
No comments:
Post a Comment