Afisa Mdhamini wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Pemba Bi Jokha Khamis Makame,kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akimkabidhi vyakula msaidizi katibu wa Soba House iliyopo Mkanjuni wilaya ya Chakechake,vyakula vikiwemo Unga ngano,Mchele Mafuta na Tende na Mafuta ya kupikia,kwa ajili ya vijana walioachana na madawa ya kulevya.
Afisa Mdhamini wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Pemba Bi Jokha Khamis Makame,akitoa nasaka zake kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,baada ya kuwakabidhi vyakula vijana wa Soba House Mkanjuni wilaya ya Chakechake leo
Baadhi ya Vijana walioachana na madawa ya kulevya Sobar House No 1 Wete Pemba wakimskiliza Afisa Mdhamini wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Pemba Bi Jokha Khamis Makame,(hayupo pichani) alipozungumza nao kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,baada ya kuwakabidhi vyakula alipofanya ziara maalum ya kuwatembelea leo.[ Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
No comments:
Post a Comment