Habari za Punde

Warioba ataka mabaraza ya Katiba yasiingiliwe

9767 2Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba akiongea na waandishi wa Habari (hawamo pichani) jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kuundwa kwa mikutano ya mabaraza ya katiba yanayotarajia kuanza kufanya kazi  Julai 12, 2013. wariobaMwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji  Mstaafu Joseph Warioba akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu  mikutano ya mabaraza ya Katiba inayotarajiwa kuanza  Julai 12 mwaka huu kwa ajili ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Rasimu ya katiba ilitolewa 3 Juni 2013.Kulia ni Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Assaa Rashid. (Picha zote na Lorietha Laurence Maelezo)
……………………………………………………………
Na Belinda Kweka- MAELEZO
 
TUME ya Mabadiliko ya Katiba imeandaa mfumo wa uendeshaji wa mikutano ya Mabaraza kuanzia Julai 12 hadi 2 Agosti mwaka huu, ambao utatoa ushiriki mpana kwa kila mjumbe kuchangia na kutoa mawazo yake kwa uhuru na uwazi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba amesema mkutano hiyo ni ya kujadili na kutoa hoja za msingi kwa maslahi ya Taifa na si kupiga kura au kutetea maslahi ya kundi au watu fulani.
 
Jaji Mstaafu Warioba alisema wajumbe wa mabaraza hayo hao wa mabaraza kushiriki na kutoa mawazo yao kwa uhuru bila kuingiliwa na taasisi au mtu yoyote ili kupata Katiba yenye maslahi na taifa.
 
“Napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa kila mjumbe  atapata fursa ya kushiriki kwa kutoa maoni bila ya kuingiliwa na mtu yoyote kwa kuzingatia taratibu ambazo zitawekwa na Tume katika kuendesha na kusimamia mikutano hiyo” alisema Jaji Mstaafu Warioba.
 
Aliongeza kuwa Wajumbe wa Mabaraza takribani 20,000 wamepata  Rasimu  hiyo ya katiba pamoja na mashirika, ambapo alisema Tume hiyo imepanga kuanzia julai 12 mwaka huu itaanza kugawa Rasimu hiyo katika kila kijiji ili kuweza kuifikia nchi nzima.
 
Pia amesema Tume itatumia siku 54 katika kuendesha mabaraza ya katiba ya wilaya kwa nchi nzima na imejigawa katika makundi 14 na kila kundi litaendesha mikutano hiyo katika mamlaka za Serikali za mitaa 12 au 13.
 
Jaji Warioba pia alifafanua kuhusu hoja ya Serikali tatu na kusema kwamba hayo ni maoni yalitolewa na wananchi wenyewe na si yeye binafsi na suala hilo lipo takribani miaka 30 nchini hivyo si geni kwa Serikali.

2 comments:

  1. Anasema Mabaraza ya Katiba yajadili mambo ya Msingi ambayo yana maslahi ya TAIFA... Namuuliza Jaji Warioba kwani Walioungana ni Nani?

    Kama Katiba inaitwa ya Muungano, Muungano huu umefanywa na Mataifa 2 Huru. Hivo Unaposema watu wasijadili kuhusu kundi fulani au Watu fulani. Inamaana Unawanyima Wazanzibari haki yao yakuamua ni aina gani ya Muungano wanautaka.

    Wazanzibari wamechoka kulazimishwa Muungano uliokua hauna faida kwa Jamii zote 2, jamii ya Tanganyika na ile ya Zanzibar.

    Kukataa matakwa ya Taifa la pili lilounda Muungano huu. Nikulazimisha Utawala wa Kimabavu. Kura ya Maoni kwa Zanzibar ni lazima. Hata kama Shuweni hatatoa Fursa Wazanzibari wana haki hiyo. Tumechoka Usanii wa Ukoloni Mambo Leo.. Ambao unaitwa Muungano.

    ReplyDelete
  2. Jaji Warioba bado yupo sahihi juu ya anayoyasema, na hii ni kwa kuzingatia ukweli kwamba sio sote wenye 'vision' ya kujua faida na hasara za baadhi ya maamuzi.

    Ukweli utabaki tu kuwa wengine lazma tupate watu kama Jaji Warioba watutahadharishe juu ya maamuzi yetu.

    Tumechoka kuishi kwa majuto, bado tunakumbuka mwaka 1963 namna viongozi wa wakati ule walivyoendesha siasa za kihafidhina mpaka wakatuingiza shimoni.

    Naamini haya tunayoyaona leo yasingetokea kama wangekua na mawazo kama ya Warioba...wao wenyewe wamekufa na kuzikwa ughaibuni

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.