WATU watatu wamefariki dunia katika matukio tofauti, wakiwemo msichana aliekufa baada ya kunywa sumu ya panya.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Augustino Ollomi alisema tukio hilo limetokea
hilo limetokea Agosti 13 katika kijiji cha Kwambani wilaya ya Kati.
Alisema
msichana huyo mwenye umri wa miaka 18, aligombwa na wazazi wake kwa madai
kwamba alikutwa na mwanamme na ndio alipokasirika na kuchukua uamuzi.
Alisema
msichana huyo alifariki dunia wakati akikimbizwa hospitali.
Katika tukio
la pili, Maria Hassan Ali (30) mkazi wa Paje aliuawa kwa kupigwa mapanga
kichwani kwa kumpa hifadhi mke wa mtuhumiwa alietajwa kwa jina la Elizabeth
Michael Masamba.
Kamanda
alimtaja mtuhumiwa wa mauaji huyo kuwa ni Silvesta Robert Masharo (42).
Alisema chanzo
cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia kati ya mtuhumiwa na mkewe ambao
walikuwa wakiweka fedha kwenye kibubu.
Alisema siku
ya kuvunjia kibubu hicho, fedha walizokuwa wakichanga hazikuonekana ndipo kila
mmoja alipomtuhumu mwenzake kuiba fedha hizo.
Alisema
mtuhumiwa alitoa kauli ya kutishia kumuu mkewe kama hatarejesha fedha, ndipo
mwanamke huyo alipoamua kwenda kuweka ripoti kituo cha polisi Paje na mtuhumiwa
akachukuliwa akawekwa ndani.
Alisema baada
ya siku tatu majirani zake wakaenda kumchukulia dhamana na alipotokana
alimtafuta mkewe nyumbani lakini hakumkuta ndipo alipomkuta kwa shoga yake
amejihifadhi.
Kamanda Ollomi
alisema mtuhumiwa ndipo alipochukua uamuzi wa kumshambulia kwa mapanga shoga wa
mkewe na kusababisha kifo chake.
Pia
alimshambulia vibaya mkewe ambae anaendelea na matibabu katika hospitali kuu ya
Mnazimmoja na mtuhumiwa amekimbia.
Alisema tukio
la tatu linamuhusu mpanda vespa Ramadhan Sham Ali (21) ambae alikuwa baada ya
kuanguka katika mpito wa Mwambuani Muyuni.
Alisema
marehemu akiwa na rafiki yake walikuwa wakirejea Mchangamle.
No comments:
Post a Comment