Na Mwandishi Wetu Dar.
Mwanamme mmoja, ambaye amekuwa akiongozana na maaskari polisi wawili, amekuwa akigawa fedha za bure kwa watu mbalimbali jijini Dar.
Kijana huyo wa makamo, ambaye kwa wiki hii nzima amekuwa akitajwa kwenye radio mbalimbali, aliwalipia bili wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa hospitali ya Mwanyamala na Muhimbili, wodi ya wanawake.
Akizungumza na mwandishi wetu,mmoja wagonjwa wa hospitali ya Muhimbili, Subira Juma alisema kijana huyo alikuja hospitali na kuuliza wangapi wanadaiwa halafu akawalipia bili zao na kisha kuondoka zake bila kujitambulisha.
‘Kwa kweli hata mimi sifahamu kijana huyu katokea wapi, lakini sijwahi kuona mtu akitoa hela bila kujuana, na kisha kuondoka bila kusema lolote’ alisema Subira.
Wakati huo huo, wasafiri wa daladala nao, hasa ziendazo Mbagala nao wametajwa kunufaika na mgawo huo, ambapo wamekuwa wakilipiwa nauli mara kadhaa na mtu huyo.
Mbali na kulipia watu usafiri, kijana huyo pia anatajwa kuwanufaisha madereva boda boda na bajaji kwa kuwawekea mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri.
No comments:
Post a Comment