Habari za Punde

Ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe.Jaji Kazi Kutembelea na Kukagua Vifaa vya Upigaji Kura 2025

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)Jaji George Joseph Kazi akiwa pamoja na Wajumbe wengine wakimsikiliza Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini A Miza Pandu Ali walipokua katika ziara ya kutembelea na kukagua Vifaa vya Upigaji Kura katika Wilaya zote za Unguja.

Na Rahma Khamis Maelezo. 7/10/2025

Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC imesema imejipanga vyema kuhakikisha zoezi la Upigaji wa kura nchini linakwenda vizuri kama linavyopangwa.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Goerge  Joseph Kazi ameyasema hayo Ofisini kwake Maisara mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea na kukagua Vifaa vya kupigia Kura katika Wilaya zote za Unguja

Amesema vifaa hivyo tayari vimeshawasili katika Wilaya zote ambapo Tume tayari imeanza zoezi la kupita kuvikagua ili kujiridhisha na kuangalia kama viko salama.

Aidha amewataka wahusika waliokabidhiwa vifaa hivyo kuviangalia kwa uangalifu, kuhifadhi na kuvilinda muda wote ili vibaki salama.

Msimamizi Uchaguzi Wilaya ya Kati Bakari Muhammed Suleiman amesema kuwa tayari vifaa vyote vimeshafika ikiwemo masanduku na vituturi vya kupigia kura kilichobaki kwa Sasa ni kusubiria zoezi la uchaguzi lifike ili vianze kutumika.

Nao Miza Pandu Ali Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini A' na Mwanamkuu Gharib Mgeni Afisa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini B' wamesema kuwa maandalizi ya Uchaguzi yote yameshakamilika kwa asilimia tisiini ambapo usalama wa vifaa hivyo upo wa kutosha kwani wamejipanga vyema kuhakikisha vifaa hivyo vinakuwa salama muda wote.

Aidha wamewasisitiza watendaji wenzao kujenga mashirikiano ili kuhakikisha Uchaguzi unafanyika kwa Salama, Amani na Utulivu

Wilaya zilizokaguliwa Vifaa hivyo ni Wilaya ya Kusini Unguja, Wilaya ya Kati, Wilaya ya Kaskazini A' na B' Unguja, Wilaya ya Magharibi A' na B' pamoja na Wilaya ya Mjini.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)Jaji George Joseph Kazi akiwa pamoja na Wajumbe wengine wakiangalia Vifaa vya Upigaji Kura na kupata maelezo kwa  Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kati Bakari Burhani Suleiman walipokua katika ziara ya kutembelea na kukagua Vifaa hivyo  katika Wilaya zote za Unguja.

Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini A Miza Pandu Ali akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Vifaa vya Upigaji Kura walipokua  katika ziara na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jji Giorge Joseph Kazi na Wajumbe wengine kutembelea na kukagua Vifaa vya Upigaji Kura katika Wilaya zote za Unguja.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)Jaji George Joseph Kazi akiwa pamoja na Wajumbe wengine wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Aziza Iddi Suwedi walipokua katika ziara ya kutembelea na kukagua Vifaa vya Upigaji kura   katika Wilaya zote za Unguja.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)Jaji George Joseph Kazi akiwa pamoja na Wajumbe wengine wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Aziza Iddi Suwedi walipokua katika ziara ya kutembelea na kukagua Vifaa vya Upigaji kura   katika Wilaya zote za Unguja.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)Jaji George Joseph Kazi akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea na kukagua Vifaa vya Upigaji Kura katika Wilaya zote za Unguja.

Vifaa vya Upigaji kura katika Wilaya ya Mjini kama vinavyoonekana Vikiwa Tayari kwa Zoezi hilo Zanzibar.
PICHA NIA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR.07/10/2025.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.