Na Abdi Suleiman, Pemba
WATOTO 562 wanaoishi katika mazingira magumu kisiwani Pemba, wametambuliwa na kupatiwa vifaa mbali mbali vya skuli.
Vifaa hivyo vimetolewa na Jumuiya ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu (PIRO).
Wilaya zilizofaidika na vifaa hivyo ni Wete, katika shehia ya Kangagani ambako kuna watoto 125, Mjini Kiuyu (watoto 125), na shehia ya Micheweni mjini (watoto 187) na Majenzi yenye watoto 125 katika wilaya ya Micheweni.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mtunza Takwimu kutoka PIRO, Said Mohammed, alisema watoto hao wanaishi katika mazingira magumu na wako katika hatari ya kutumikishwa.
Alisema watoto wanaotumikishwa hawapati elimu kutokana na uwelewa mdogo wa watu wanaoishi nao kwa kushindwa kuwahimiza kwenda skuli badala yake kuwaachia kuwenda kufanya kazi.
“Baada ya kuwapatia vifaa hivyo vya skuli, watoto wengine hurudi skuli kuwendela na masomo yao, lakini kabla ya hapo walikuwa wahajuwi nini wanachokifanya,”alisema.
Akizungumzia jinsi walivyoweza kuwatambua watoto hao, alisema mwanzo waliunda mabaraza ya watoto katika shehia hizo, kwa kutumia watoto na watu wazima wanaokubalika katika jamii.
Hata hivyo aliwataka wananchi na mashirika mengine kuendela kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto wao na kuacha kuwatumikisha.
Mashallah. May God bless you.
ReplyDeleteHaji Rajab Haji.