Habari za Punde

PBZ yakabidhi Fulana kwa Ajili ya Sherehe.

Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Seif Suleiman kulia akimkabidhi Fulana Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi.wanaidi Saleh,  fulana hizo kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya Elimu bila ya Malipo Zanzibar huadhimishwa kila mwaka Septembe 23, kutimia miaka 49 Elimu Bila ya Malipo Zanzibar. makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ya Katibu Mkuu Mazizini Unguja.

Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Seif Suleiman, akimkabidhi fulana Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazamiaji na Uokozi Zanzibar Bwa.Faki Mbarouk Faki, kwa ajili ya kuadhimisha mwaka mmoja wa Jumuiya hiyo tangu kuazishwa jumuiya hiyo kwa ajili ya kusaidia Jamii wakati wa maafa ya baharini na nchi kavu.Jumuiya hii ilitowa msaada mkuwa wakatin wa ajali ya kuzama kwa Meli miaka miwili iliopita na kutowa msaada mkubwa kwa jamii. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazamiaji na Uokozi Zanzibar Faki Mbarouk Faki, akitowa shukrani kwa PBZ kwa msaada wao na kuona umuhimu wa kusaidia jamii kwa nyanja mbalimbali za maendeleo ili kufanikisha malengo yao katika kusaidia jamii, na kusema amezitaka taasisi nyengine kuiga mfano wa PBZ kuwa karibu na Jamii katika kutowa misaada ya hali na mali.     

2 comments:

  1. Jamaa hawa pbz vipi naona matumizi yao kilasiku wanazo hizo pesa au hizo za watu wakiziona nyingi wanafikiria zao, meneja angalia vizuri pesa zilowekwa humo sio pesa za PBZ, pia mabenki nayo hufilisika kuwa muangalifu baba

    ReplyDelete
  2. Naona ndio kwanza wana kurupuka sas kusaidi taasisi za kijamii walikuwa wana kulatu, tangu kuja hizi kampuni za bara kuwazina jishughuli na wao wanai ga japo kido pia sihaba kuliko kukosa kabisa

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.