Na Hafsa Golo
WAKULIMA wa kilimo cha mpunga cha umwagiliaji maji wa bonde la Mwenge na Mwachalale wilaya ya magharibi wameanza kukata tamaa kufuatia kupanda kwa gharama za uendeshaji wa kilimo hicho.Hali hiyo imeendelea kuathiri kipato chao kutokana na changamoto hizo kwa vile hawataweza kufidia gharama hizo kuendeleza kilimo hicho.
Wakizungumza na gazeti hili wakulima mbali mbali kwa nyakati tofauti walisema pamoja na serikali kuhamasisha wakulima kuendeleza kilimo, gharama zitawasababisha kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali ya kupambana na umasikini.
Mkulima Jamali Haji Ramadhan alisema wakulima wanalazimika kulipia shilingi 20,000 kwa huduma ya umwagiliaji maji kwa robo moja ya konde, mbali na ununuzi wa mbolea, hali ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu.
Mkulima Salama Ramadhani wa bonde la Mwenge alisema msimu wa masika hawakuweza kufanikiwa mavuno, kwa sababu ya ukosefu wa maji katika bonde hilo kufuatia uharibikaji pampu.
“Sijui tena msimu wa vuli hali itakuwaje maana hadi sasa bado matengenezo na maandalizi yanatarajiwa kuanza tarehe 15 mwezi huu”, alisema mkulima.
Msaidizi wa kituo cha umwagiliaji maji bonde la Bumbwisudi, Adam Khamis, alisema pamoja na kuanza kwa msimu lakini hofu na woga umewakabili baadhi ya wakulima wa umwagiliaji maji kwa kutokuwepo ufumbuzi wa pampu hizo kuendelea kupoteza nguvu zao bila ya mafanikio.
Aidha, aliishauri serikali kusimamia kwa kina kilimo cha umwagiliaji maji katika mabonde ambayo tayari yamekuwa yakitumia taratibu hizo na sio kuanzisha sehemu nyengine wakati hayo yakiwa yanayumba kiutendaji.
“Hatuwezi kufikia malengo kwani pale palipoanzishwa utaratibu huo kumekuwa kukirudi nyuma isiwe tunaandika namba 100 kumbe nyuma kuna namba tumefuta kweli itakuwa 100”, alihoji.
Mtaalamu wa kilimo, wa wilaya ya magharibi eneo la Mwakaje na Bumbwisudi, Hamid Ali Machu, alisema kumekuwa na changamoto kadhaa katika kilimo cha mpunga cha umwagiliaji maji ikiwemo ukosefu wa maji, kupanda kwa gharama siku hadi siku.
“Wakulima wa umwagiliaji,kuchimba kwa ngombe shilingi elfu 15,kuburuga elfu 10,na kuchangia umeme elfu 20 kwa robo konde.”alisema.
Mkurugenzi wa umwagiliaji maji, Bakar Ased, akijibu madai hayo alisema zaidi ya shilingi milioni mia moja, serikali imefidia deni la wakulima wa kilimo hicho ambapo zilikuwa zikidaiwa na shirika la umeme.
“Serikali deni la nyuma waliokuwa wakidaiwa wakulima kwa ajili ya umeme, imefidia ambapo inalilipa kidogo kidogo shirika la umeme”, alisema
Aidha, alisema suala la matengenezo ya pampu zilizoharibika ni miongoni mwa mambo yaliyopewa kipaumbele na Wizara ya Kilimo na Maliasili mara baada ya kingizwa fedha.
Aliogeza kuwa kupitia wizara ya kilimo inathamini suala zima la kilimo hivyo imekuwa ikifanya jitihada kadha ili kuhakikisha malengo ya mapinduzi ya kilimo yanafikiwa ambapo hivi sasa wizara imenunua pampu mpya kwa ajili ya bonde la Mtwango.
Ukweli ni kwamba Z'bar hakuna kilimo cha mpunga, kinachoendelea ni mazoea tu.
ReplyDeleteNatoa changamoto kwa wizara ya kilimo na kwa mtu yeyote aniambie ni tani ngapi tunavuna kwa mwaka?
Binafsi nimemshauri mama yangu mzazi aachane na kilimo cha mpunga baada ya kuona mavuno yake kwa mwaka hayazidi kl.200.
Tungekua na uongozi makini na ulio tayari kubadilika, tungewashauri wakulima kuyatumia mabonde kulima mboga mboga kwa vile tuna soko la uhakika ktk mahoteli yetu.
Ndugu yangu, sio kuwa kilomo cha mpunga hakilipi, bali smz, haina mpango, wakuwasaidia wakulima, bibi yangu alinambia, wakoloni, walieka mabwana shamba, kila wilaya kuwaelekeza wakulima, wakivuna mpunga wana panda kunde ili ele ardhi ipate rutuba, wao wamejazana darajani na kizimbani wanangoja semina na kuoneshana hina miguuni, mambo ya wakulima na wakwezi hayo, kuhusukilimo cha mbogamboga tulitakiwa tujipange kabla huuutalii,sisi kazizi yetu kulaumu hat pasio kulaumika
ReplyDelete