Habari za Punde

Rais Kikwete Atemblea na Kukagua Jengo la Bunge Mjini Dodoma Leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Oktoba 24, 2013 ametembelea na kukagua Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kujionea maandalizi ya jinsi Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba watakavyokaa katika Ukumbi wa Bunge hilo. Bunge hilo Maalum la Katiba litakuwa na Wabunge 600 tofauti ya Bunge la sasa lenye Wabunge 354 ambao ni pamoja na Wabunge 239 wa kuchaguliwa kutoka majimboni, Wabunge Wanawake Viti Maalumu 102, Wabunge wa kuteuliwa toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar 5, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wabunge 7 (kati ya 10) wa kuteuliwa na Rais.

 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akikaribishwa kutembelea Jengo la Bunge mjini Dodoma na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai leo 




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.