Makamo wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi apokelewa kwa Shangwe na Watanzania wanaoishi Seattle pamoja na wafanyabiashara wa Zanzibar waliofika hapa kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara kutoka nchi mbali mbali.
Makamo wa pili wa Rais kesho anategemewa kufungua mkutano huo akiwa mgeni rasmi. Wafanyabiashara waliofuatana na Makamo wa pili wanategemewa kukutana na wafanyabiashara wenziwao kwa lengo la kushirikiana kibiashara.
Miongoni mwa wafanyabiashara maarufu waliokuja hapa Seattle Marekani ni ndugu Ahmada (kushoto katika picha) ambaye anamiliki skuli ya kisasa ijulikanayo SHA. Miongoni mwa malengo yake ya kuja hapa ni kutafuata muwekezaji atakayeshirikiana naye katika ujenzi wa nyumba nafuu kwa wananchi wa Zanzibar pamoja na kuleta vifaa vya kisasa katika ujenzi wa nyumba za kisasa. Picha na maelezo kutoka kwa ndugu Mohamed Muombwa
No comments:
Post a Comment