Habari za Punde

Shukran Bi Amie Bishop kwa Msaada wako wa shilingi millioni 10


Mratibu wa Jumuia ya Maendeleo ya watu wa Mzuri (Mzuri kaja Development Society) ambaye pia ni msaidizi wa Makamo wa Pili wa Rais yuko Seattle kuhudhuria mkutano wa Wafanyabiashara. 

Pamoja na mambo mengine alikutana na Bi. Amie Bishop na familia yake kutoa shukrani za dhati kwa msaada wake mkubwa wa fedha zisizopungua millioni 10 ambazo zilitumika kujenga nyumba ya walimu iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein mwezi wa Machi mwaka huu. 

Wakati wa sherehe ya ufunguzi wa nyumba ya walimu Jumuiya ya Maendeleo ilitoa cheti cha shukrani kwa bi. Amie kwa msaada wake. Cheti hicho kilipokelewa na ndugu Muombwa kwa niaba yake kwani hakupata nafasi kuhudhuria sherehe hiyo. 

Aidha bi. Amie Bishop amemuelezea ndugu Muombwa kuridhika kwake na jinsi msaada wake alivyotumiwa na ameahidi kuisaidia tena Jumuiya ya Mzuri katika ujenzi wake wa maabara ya kisasa ya sayansi itakayoanza hivi karibuni. Jumuiya ya Maendeleo ya Watu wa Mzuri inawaomba wafadhili wengine kusaidia jengo hilo ambalo ramani yake inaonekana hapo chini.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.